Siwezi kwenda msibani na ndevu

Siwezi kwenda msibani na ndevu

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,174
Reaction score
16,794
UKIPENDA BOGA PENDA NA UA LAKE:

Alifika mwanaume akiwa ana hema ametoka kazini kabla ya muda wa kawaida,akamwambia mke wake Jiandae haraka tuna safiri kwenda mbeya,

Mke akamuuliza kuna nini?? Akajibu mama amefariki..

Mke akamwambia mi siwezi kwenda kilioni nikiwa hivi, akaenda saluni akaweka nywele vizuri na kubandika kope za macho, aliporudi akaanza kupanga nguo, akamuuliza mmewe hv mama yako amefariki na nini??

Mume wake akamwambia mama yangu hana kitu nimetoka kuongea nae sasa hv...

Mke akahamaki si umeniambia kuwa kuna msiba?? Akajibiwa kuwa mama yako ndio kafariki, mke akaanza kugalagala na kupiga kelele, niwahishe haraka nyumbani nikamzike mama nisije kuta wamezika.,

Mume wake akamwambia siwezi kwenda msibani nikiwa hv..subiri nikanyoe ndevu...
 
Jamaa alisahau kuzima simu akiwa msikitini anaswali GHAFLA simu ikaita akaingiza mkono ili aikate, kwa bahat mbaya akaminya cha kupokelea, alipohangaika kuzima akajikuta kaminya laudspika ikasikika sauti 'ETI HONEY UMESEMA NIWEKE KITIMOTO KIASI GANI? 😄😄😄🙆🙆🙆🙆
 
Kali mnoo maana me. nilikua nimenuna zangu nimejikuta nasmile loh@zee la nyeti
 
Jamaa alisahau kuzima simu akiwa msikitini anaswali GHAFLA simu ikaita akaingiza mkono ili aikate, kwa bahat mbaya akaminya cha kupokelea, alipohangaika kuzima akajikuta kaminya laudspika ikasikika sauti 'ETI HONEY UMESEMA NIWEKE KITIMOTO KIASI GANI? 😄😄😄🙆🙆🙆🙆

Hhhhhhaa mkuuu nimecheka mpaka machozi duuuu
 
Back
Top Bottom