Siyatambui mapinduzi Guinea, Rais Conde namtambua kama Rais bado waliomteka nyara wamrudishe upesi

Siyatambui mapinduzi Guinea, Rais Conde namtambua kama Rais bado waliomteka nyara wamrudishe upesi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Bunge la Guinea kwa Vikao vyake halali kabisa lilijiongezea posho na kupitisha kuwa Raisi aliyepo Raisi aliyepo ruksa kugombea tena

Kikosi kimoja cha makomandoo bila kushirikisha vikosi vingine vya jeshi wakaenda kumteka Raisi Condé na kumficha wanakojua wao.

Mimi bado namtambua Rais Conde kama Rais halali wa Guinea na nautaka umoja wa Afrika usimtambue huyo jambazi Mamady Doumbouya na Kikosi chake cha majambazi makomandoo waliomteka Rais halali na kujitia eti wamempindua.

Vikosi vingine nendeni mkalipindue hilo jangili. Mamady Doumbouya arudishwe Rais Conde

Naitaka jumuiya ya kimataifa ilaani huo utekaji nyara na hilo Jambazi linalojiita limepindua liuawe chap chap

Kwa mujibu wa katiba ya Guinea hakuna njia ya Jeshi ya kumuondoa Raisi aliyepo madarakani. Jambazi Mamady Doumbouya kavunja katiba
 
Kikubwa tuliona raia wakiwa wanasherekea mapinduzi. Kuna njia mbalimbali za watu kuingia madarakani kama uchaguzi, kurithi na kupindua Serikali iliyopo. Mazingira ndio huleta chaguo la njia ipi itumike, kwa dizani ya maraisi walioweka bunge mfukoni, basi mapinduzi ni njia sahihi kabisa. Tena walipaswa wampe kazi ngumu kama kumlimisha kwenye mashamba kama mwezi ili ajue aina ya maisha ya raia aliokuwa anawaongoza.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
hizi ndoto zimejaa majinamizi tupu
 
Hakuna kitu kibaya kama kunywa uji wa mapumba ya mahindi na chumvi kama chakula kikuu cha siku.

Ukute mtoa mada ni muhitimu wa chuo fulani tangu 2013 hana ajira, kakaa kwa shemeji imeshindikana akajiunga na forever living anatembea na vipeperushi kila siku kazi kuhudhuria mikutano ya motivational speakers tu kila alhamisi na anasali kwa Gwajima. Unaweza kuelewa ni mtu wa aina gani
 
Bunge la Guinea kwa Vikao vyake halali kabisa lilijiongezea posho na kupitisha kuwa Raisi aliyepo Raisi aliyepo ruksa kugombea tena

Kikosi kimoja cha makomandoo bila kushirikisha vikosi vingine vya jeshi wakaenda kumteka Raisi Condé na kumficha wanakojua wao

Mimi bado namtambua Rais Conde kama Rais halali wa Guinea na nautaka umoja wa Afrika usimtambue huyo jambazi Mamady Doumbouya na Kikosi chake cha majambazi makomandoo waliomteka Rais halali na kujitia eti wamempindua

Vikosi vingine nendeni mkalipindue hilo jangili. Mamady Doumbouya arudishwe Rais Conde

Naitaka jumuiya ya kimataifa ilaani huo utekaji nyara na hilo Jambazi linalojiita limepindua
Peleka kitolea hewa kule
 
Kikubwa tuliona raia wakiwa wanasherekea mapinduzi
Yale ni maigizo kama maigizo mengine. wanashangilia kuvunjwa katiba ya Guinea?

Katiba inatamka wazi kuwa katika njia za kumuondoa Raisi madarakani hiyo ya mapinduzi haimo kwenye katiba

Raisi Conde ni Raisi halali wa Guinea hadi saa hii kwa mujibu wa katiba ya Guinea siyo hilo Jambazi Mamady Doumbouya
 
Jana bwana Doumbouya alimquote Jerry Rawlings alisema "if the people are crushed by their elites, it is up to the army to give the people their freedom."
Kwenye katiba ya Guinea hiyo statement haimo. jeshi halitajwi kama njia mojawapo ya kumuondoa Raisi madarakani. hilo Jambazi Mamady Doumbouya lazima lifungashwe virago
 
Naomba Mama Samia Tanzania tuwahi haraka kutangaza kuwa hatuitambui serikali ya huyo jambazi Mamady Doumbouya aliyeingia madarakani kinyume cha katiba ya Guinea
 
Naomba Mama Samia Tanzania tuwahi haraka kutangaza kuwa hatuitambui serikali ya huyo jambazi Mamady Doumbouya aliyeingia madarakani kinyume cha katiba ya Guinea
Shughulika na matatizo ya nchi yako acha kiherehere ndugu.
Nchi yako watoto wanakalia matofali wakiwa darasani, kuna sehemu maji hakuna, kuna hospital hata panadol ni shida.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
hizi ndoto zimejaa majinamizi tupu
Mimi uzuri huwa post zangu sipost kutafuta likes ! !! ! Hii mada iko juu mno ya uwezo wako hii ni ya kimataifa sio ya ndani ya hoja ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi mada ambazo wewe unaziweza kidogo! ! ! Hapa niko anga za kimataifa
 
Shughulika na matatizo ya nchi yako acha kiherehere ndugu.
Nchi yako watoto wanakalia matofali wakiwa darasani, kuna sehemu maji hakuna, kuna hospital hata panadol ni shida.
Wakizalisha wakimbizi watatusumbua. Guinea ilishazalisha wakimbizi wakaja Tanzania ndio maana tuna hadi mtaa wa Guinea uliokuwa Zaman umejaa wakimbizi wa Guinea. hatutaki historia ijirudie hilo Jambazi Mamady Doumbouya lifungashwe virago
 
Mimi uzuri huwa post zangu sipost kutafuta likes ! !! ! Hii mada iko juu mno ya uwezo wako hii ni ya kimataifa sio ya ndani ya hoja ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi mada ambazo wewe unaziweza kidogo! ! ! Hapa niko anga za kimataifa
pumba Kama hizi Kama ni mada na hoja basi tuna vilaza wengi JF we ndo kiongozi wao
 
Back
Top Bottom