Sheria yetu ya usalama barabarani (Road Traffic Act, 1973) hailazilimishi dereva kusimama bila uwepo wa mvukaji. Sheria inamtaka dereva kusimama endapo kuna mwenda kwa miguu anataka kuvuka.
Hata hivyo kuna baadhi ya vivuko vya waenda kwa miguu vyenye alama au mchoro unaosomeka "STOP', hapa ni lazima kusimama hata kama hujaona mvukaji anataka kuvuka. Alama hizi zinawekwa sehemu yenye waenda kwa miguu wenye changamoto kama watoto au wenye ulemavu na kwenye mazingira yenye uoni hafifu.
Pia sheria haitamki gari kuzuiliwa endapo dereva kafanya kosa. Kinachofanyika ni kuzuia gari ili liwe kama dhamana, lakini sheria haitamki hivyo.
Makosa yanayofanywa na askari yasichukuliwe kama madhaifu kwa sheria. Hata hivyo kuna haja ya kuipitia upya RTA ili kurekebisha mambo yaliyopitwa na wakati.
Hata hivyo ili kuleta ufanisi kuna haja ya kufanya mabadilko kwa kikosi cha usalama barabani ili kiwe na askari wenye weledi wa sheria wanayosimamia.
Sent using
Jamii Forums mobile app