Siziamini takwimu za idadi ya waliouliwa kwenye maandamano

Siziamini takwimu za idadi ya waliouliwa kwenye maandamano

Iko hivi….

Kwa kawaida serikali nyingi duniani, hususan hizi za kwetu huku kwenye hizi jamhuri za ndizi, huwa hazitoi takwimu sahihi za wahanga wa majanga asili au majanga yasababishwayo na watu.

Sasa jana huyo Chande kasema tume yake imehesabu watu 518 ndo waliouliwa.

Naamini huo ni uongo. Naamini idadi kamili ni kubwa sana kuzidi hiyo ya 500 na ushee.

Lakini kwa vile ushahidi wa mauaji yao upo nwingi, ni dhahiri, na usiopingika, wameshindwa kabisa kukana kuwa hakuna mtu aliyeuliwa.

Pia, naamini kwamba, baada ya kushindwa kukana kuwa hakuna mtu aliyeuliwa, imewabidi tu waje na idadi flani ambayo haitowashitua sana wananchi.

Hivyo, ndo wakafikia uamuzi wa kuja na hiyo idadi ambayo haitishi sana wala kushitua kivile.

Idadi ya waliouliwa naamini ni kubwa sana kuizidi hiyo iliyotangazwa.

Na msinielewe vibaya, roho za watu 518 si chache hizo. Tunazungumzia binadamu hapa.

Kwa jinsi walivyojaribu, imewawia vigumu sana kulikwepa hili suala zima la wauaji. Wamebaki kujiumbia tu takwimu wazijuazo wao wenyewe.

ICC karibuni sana Tanzania. Sina shala mtapokelewa vizuri sana na Watanzania wote wapendao haki na mtapata ushirikiano wa kutosha kabisa kutoka kwa Watanzania.
Tawala za kiafrika!!
 

Attachments

  • IMG_20211029_105959.jpg
    IMG_20211029_105959.jpg
    15.5 KB · Views: 10
Si mlisema kwanzia tume hamuiamini vipi sahivi mnajadili report ya tume ambayo hamkuikubali tangu mwanzo? Au sahivi tume mmeiamini ila report yake ndo hamuiamini?
Tulipokuwa hatuukubali ubaguzi wa rangi huko Africa kusini, tuliacha kuujadili?
 
Unaweza ukaja na za kwako Ili utimize matakwa ya bwana zenu.
Mabwana wanaanzia wakati gani, maana kama ni serekali nayo inashinda huko huko ikitembeza bakuli.. Au nyie ni wake mliochika na hao mabwana?
 
100% correct!.
We mtu anakuambia watz wanatekwa kwasabb za madeni, mapenzi, kusafiri, ushirikina na upuuzi mwingone LAKINI sio sabb za kisiasa...nikaachia hapo kumsikiliza!.
Ile nguvu kubwa waliotumia kumzima Humphrey Polepole asiongee mpaka kuzima mpakq internet, kutuma machawa wao kumshambulia kwa maneno Polepole Leo hii Jaji Chande anakuja kutuambia sababu za kutekana eti ni za kimapenzi sijui madeni hata kama umekubali kuwa muongo jitahidi uwe smart
 
Report ya Chande imepikwa na watu wasiojua hesabu


Wamesema kuna vifo 518 nchi nzima
Wakasema vimetoka mikoa ya


Dar. 182
Mwanza 90
Mbeya. 80
Arusha. 53


Jumla 405


Hii ni tofauti na 518 kwa 113 , hili gap ni kubwa sana ina maana namba ilitugwa tu


Kisha wakasema kuhusu maiti ni 518


Maiti zilizotambulika. 485
Ambazo hazikutambulika. 9
Jumla. 494


Kuna tofauti ya 518 - 494 = 24


Ina maana maiti 24 zimepotea ni gap kwenye report


Hii ni report wamekaa nayo kwa siku 153 inatoka ikiwa na makosa makubwa hivi


Hii ni ishara wametengeneza report tena bila umakini wowote
Hao wote hesabu ziliwashinda wakajikita kwenye simulizi za mambo ya kale!
 
Report ya Chande imepikwa na watu wasiojua hesabu


Wamesema kuna vifo 518 nchi nzima
Wakasema vimetoka mikoa ya


Dar. 182
Mwanza 90
Mbeya. 80
Arusha. 53


Jumla 405


Hii ni tofauti na 518 kwa 113 , hili gap ni kubwa sana ina maana namba ilitugwa tu


Kisha wakasema kuhusu maiti ni 518


Maiti zilizotambulika. 485
Ambazo hazikutambulika. 9
Jumla. 494


Kuna tofauti ya 518 - 494 = 24


Ina maana maiti 24 zimepotea ni gap kwenye report


Hii ni report wamekaa nayo kwa siku 153 inatoka ikiwa na makosa makubwa hivi


Hii ni ishara wametengeneza report tena bila umakini wowote
Kama walipika takwimu za uchaguzi walishindwa nini kupika takwimu za waliouawa.
 
Iko hivi….

Kwa kawaida serikali nyingi duniani, hususan hizi za kwetu huku kwenye hizi jamhuri za ndizi, huwa hazitoi takwimu sahihi za wahanga wa majanga asili au majanga yasababishwayo na watu.

Sasa jana huyo Chande kasema tume yake imehesabu watu 518 ndo waliouliwa.

Naamini huo ni uongo. Naamini idadi kamili ni kubwa sana kuzidi hiyo ya 500 na ushee.

Lakini kwa vile ushahidi wa mauaji yao upo nwingi, ni dhahiri, na usiopingika, wameshindwa kabisa kukana kuwa hakuna mtu aliyeuliwa.

Pia, naamini kwamba, baada ya kushindwa kukana kuwa hakuna mtu aliyeuliwa, imewabidi tu waje na idadi flani ambayo haitowashitua sana wananchi.

Hivyo, ndo wakafikia uamuzi wa kuja na hiyo idadi ambayo haitishi sana wala kushitua kivile.

Idadi ya waliouliwa naamini ni kubwa sana kuizidi hiyo iliyotangazwa.

Na msinielewe vibaya, roho za watu 518 si chache hizo. Tunazungumzia binadamu hapa.

Kwa jinsi walivyojaribu, imewawia vigumu sana kulikwepa hili suala zima la wauaji. Wamebaki kujiumbia tu takwimu wazijuazo wao wenyewe.

ICC karibuni sana Tanzania. Sina shala mtapokelewa vizuri sana na Watanzania wote wapendao haki na mtapata ushirikiano wa kutosha kabisa kutoka kwa Watanzania.
Sijui idadi hiyo wamepewa na nani, polisi au nani!? ni ngumu polisi waue watu halafu wakupe idadi kamili ya walio uawa. Na ukitaka kujua kwamba walitumia taarifa za wauaji, kwenye utekaji wameishia kusema sababu ya utekaji ni mapenzi, maneno ambayo siku zote mulilo ndo alikuwa anayatumia kujitetea. Ndo maana mimi naamini ikiwa kusema uongo au kudanganya ni dhambi kama misaafu inavyosema basi huko peponi hukuna mtumishi wa umma atakayefika.
 
Back
Top Bottom