Sizielewi taasisi zinazohusika na kipindi hiki cha uchaguzi, hasa dhidi ya Lissu

edwardbm

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2016
Posts
292
Reaction score
254
Matendo yanayofanywa na Taasisi za serikali, hasa NEC na Polisi, yanamuongezea Mh. Tundu Lissu mgombea Uraisi kupitia CHADEMA Umaarufu wa kisiasa.

Wananchi na Raia wengi kwa ujumla wanafuatilia Kampeni za Uchaguzi mkuu huu wa 2020.

Kwenye kufuatilia wanaona/tunaona namna wagombea wanavyofanya Kampeni na kujinadi

Kwenye macho yetu Raia tunatarajia kuona wagombea woote wakipewa nafasi sawa na wakitendewa kwa usawa na Taasisi zenye kusimamia na kuhudumia taratibu na mienendo yoote ya Kampeni na Uchaguzi, Bila kujali mgombea anatokea Chama gani. Ama ni Nani. Maana tunaamini hata Viongozi ambao kwa mijibu wa katiba bado wapo madarakani watakua kua wamezingatia ratiba ya Uchaguzi na hivyo kuheshimu kanuni Sheria na taratibu zikizowekwa, ama walizoziweka.

Ila katika kipindi Cha takribani wiki mbili kabla ya Leo hii kumeonekana mgombea mmoja wa Uraisi, kwa Jina Tundu Lissu wa Chama CHADEMA, akifuatiliwq kwa namna ya kubughudhiwa aidha na Wafuasi wa Chama pinzani na Chake.

Ambapo Hadi imefika wakati pia ameanza kufuatiliwa maafisa wa usalama na ulinzi(polisi) na kutokea kinachoonekana Ni kuingia nao kwenye malumbano ya maneno na mahala pengine wafuasi ama wananchi walio simama barabarani wa msabahi ama kusikia neno kutoka kwake wakitawanywa na Polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.

Kwa ufupi kunaonekana matendo yasiyo ya usawa kwa wagombea wanaoongoza kwa Umaarufu msimu huu wa Kampeni.

Jambo Hilo Raia wanaliona, Na kwa ninavyoamini litaleta Hisia za kufanya anayeonewa bakubalike zaidi na Raia.
Ni asili ya binadamu hasa raia wa kawaida kuvutiwa ama kujiunga upande wa yule anayeonewa au wa mdogo" underdog".

Kwa maana hiyo vitendo vya kubaguliwa ama kutotendewa kwa usawa kwa mgombea wa CHADEMA ukilinganisha na mpinzani wake mgombea wa CCM, kunamuongezea Umaarufu na Wafuasi Tundu Lissu ,mgombea wa CHADEMA.

Sifahamu Kama CCM na Taasisi husika wanafahamu hili.
Mtazamo wangu unaniambia wanafahamu. Hivyo je, wanafanya Makusudi?
Ama ni Mimi ndio Nina mtazamo usio sawa.

Vyovyote vile inawapasa wajue kutotendewa kwa usawa kwa mgombea huyo kunamuongezea Umaarufu
Na litakalo tokea Ni Raia kuanza kuwabagua na kuwapinga Hadharani wagombea wa CCM Kama kulipiza kisasi

Hata Kama hawatatumia nguvu Kama ambavyo Polisi Wana uwezo wa kutumia. Kitendo tu Cha kuwakataa Hadharani wagombea wa CCM kitawaumiza zaidi Wagombea hao.

Serikali msiendelee kumpatia Umaarufu mgombea wa Upinzani.
Waachieni Raia wenyewe waamue.
Hata hivyo hamna kitendo chochote kilichofanywa na mgombea yeyote chenye kuleta uvunjifu wa amani, ama kuhatarisha amani.
 
Tatizo ni muungano wa CDm na Act wa 3/10/2020 ,wanajua huo unahatima yao hapa nchini kwahiyo Ccm wanajitahidi usifanyike
 
Wacha Lissu azidi kuwa maarufu na watashangaa sana kwa jinsi mambo yanavyokuwa.
 
Back
Top Bottom