Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dharau wadogo zako...Surviving, kazi yoyote twende, chakula chochote kula, malazi magumu rekebisha, discipline ya hela, kujiamini, don't waste time for nothing, tembea na kimbia kiukakamavu, alywas kuwa smart, sikiliza zaidi kuliko kuongea, kabla ya kuongea chochote kifikirie kama ni madini au pemba, heshima kwa wakubwa zako...
Biashara isiyo na faida utamuelekezaje mtu aifanye. Hapa natoka Kariakoo kununua vitu kwa kutumia hela yake, boom nililopokea wiki kama tatu zilizopita hata sijalitumia bado liko benki natumia hizihizi hela za Forex. Mimi naweka na kutoa sio kuhold kwa muda sijui ikue izae pesa nyingi.Ume Tongue Twist sana hizi paragraph mbili kiasi nashindwa kuelewa. By the way! Kimakadrio (Maana hufahamu kiasi ulichoweka) unadhani umetengeneza faida, balance au hasara.
$100 = 231,000
Safi, fanya mipangilio vyema na tengeneza nidhamu fedha. Naamini unaweza kukusanya vyema na kutengeneza mradi/miradi zaidi kutanua uwekezaji nje ya forex.Biashara isiyo na faida utamuelekezaje mtu aifanye. Hapa natoka Kariakoo kununua vitu kwa kutumia hela yake, boom nililopokea wiki kama tatu zilizopita hata sijalitumia bado liko benki natumia hizihizi hela za Forex. Mimi naweka na kutoa sio kuhold kwa muda sijui ikue izae pesa nyingi.
Sijawahi piga hesabu ya jumla kama nimeweka kiasi gani na kutoa kiasi gani, mara ya mwisho kuchoma ni mwaka jana February taarifa za corona zilikuwa zinabadili market ghafla utasikia Boris Johnson kalazwa, ghafla yuko anaongea, kidogo yuko ICU, mara Paris imetangaza lockdown. Wakati huo niko na exams, siku OPEC+ wakashindwa kukubaliana bei ya mafuta, jambo ambalo sijawahi shuhudia ndio nikachoma dola 150 ambayo ndio hela nyingi kuchoma. Kabla ya hapo nishachoma mara mbili, tokea hapo sichomi ni either market isumbue niondoe hela kwa hasara ya transaction fee na exchange rate (kama elfu 15 haizidi) au nipate faida.
Muda mrefu nilipumzika baada ya iPay Africa na Templer kukata mkataba. Sina VISA wala NIDA wala kadi ya mpiga kura. Mawakala walipoanza nikajivuta kwanza kusikia kama kuna vilio nikaona ni safe kuingia.
Hela nyingi nilizitumia na mademu huwezi nambia nikuoneshe nini ninamiliki. Sasa ujinga nimeacha, ila bado Fx sio sehemu yangu ya kutafuta maisha. Hili ni boom binafsi
Dancers wa mtaani kwetu wananiita tajiri niwatoe buku wana mechi jioni. Wakihisi njaa wanapiga mziki kwenye vile vi-Bluetooth device is ready to pair na kupigiana makofi kisha wanatandaza kitambaa chini uku tiyari washachora tangazo kuwa jioni wana mechi (mechi hewa). Huwa nawapa hela kwa vile niwakabaji, mara chache huwa narudi usiku.Skills ya Dancing,
Kuna Singeli na Bongo fleva