Smart phone yako ya kwanza kutumia ilikuwa aina gani?

Smart phone yako ya kwanza kutumia ilikuwa aina gani?

Umenikumbusha mbali, nilificha simu ya sister akatafuta siku nzima mpaka akakata tamaa, akanunua nyingine kesho yake. Nilivyohakikisha amerenew mpaka line nikaitupa chini ya fridge mama akaiona akampa Ila ikawa Haina kazi Tena nikamuomba kwa unyenyekevu mkubwa akanigawia mtaa ulinikoma.
 
Sikumbuki maswala ya Model maana enzi hiyo nlikua sijui hizo mambo za model mimi.

1.Siemens

Haikua yangu nili irithi toka kwa bi mkubwa nakumbuka alinyeshewa na mvua ikaloana akaisusa, nikaishi nayo mara pap natoka shule hyo siku kitu kinawaka. Ndio ikawa yangu tena.

2.Motorola

Sijui maswala ya model narudia najua tu jina, ilikua ndio kitu yangu ya kwanza kutoa hela mfukon ilikua Nyembamba mithili ya Nokia Express Music, nilinunuaga sijui sh ngap ila it costed me kwa kipindi ile nilisumbua mno mno mno.

Nikiweka Memory yangu ndani tunasikiliza mziki Dom zima, Enzi hzo simu natumia kwa mziki tu.

mana sijawahi kupgiwa simu tangu ninunue simu,kwanza nani anipigie.
Mmeulizwa smartphone mnataka kutuonyesha mmeanza lini kutumia simu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
LG L3 E400 ilikuwa mwaka 2013 ndio nimeanza chuo first year, nakumbuka kwa darasa letu kipindi cha orientation nilikuwa na smartfone peke yangu na huyo dada alikuwa na samsung min pocket kale kadogo.
 
Miaka hiyo... Unanunua vocha hakuna kujiunga ni kupiga tuu.... Wakaja Voda na utaratibu wa kujiunga ila inakubid uamke saa tisa usiku kuunga bando na linaanza kutumika asubuh mpaka saa 11 jion linakata tena mpaka saa nne usiku ikifika saa sita bando linaexpire.... Those days tulikuwaga na Nokia moja amazing sana na kwa kuwa ndg na rafik wenye sim walikuwa wacheche tukaanza mchezo ikifika usiku na dakika bado zipo tunaanza kubuni namba na kupiga hovyo....
Katika hiyo hali ya kupiga piga sik moja tulipiga sim na akapokea mdada mmoja iv alikuwa anaish Tanga na si tuko Sumbawanga katika stor stor bro akamtongoza na ndio mke wake mpaka leo toka mwaka 2007
 
Nilikuwa na HTC fulani ina roho ya paka ngumu sana yaani 😂😂mpaka kioo kiliweka spider kwa kuanguka still screetouch ipo vizuri na inanipa ushirikiano kwa vile nilinunua kwa jamaa nami nikauza jamaa akaenda kubadili kioo mbele.

Nikahamia Tecno H5 ilikuwa na kibabe yaani hata iphone 3&4 zilikuwa zinaonekana za kishamba ,jamaa wa iphone walikuja kupindua meza hayo matecno yakawa takataka kuaniza iphone 5 ilikwua balaa na Samsung walianza balaa samsung s4 hapo..
 
Back
Top Bottom