"Social Economic Empowerment Program" Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi

"Social Economic Empowerment Program" Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi

Shida ya JF ya nyakati hizi kuna watu wako huku kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu bila hata kuhoji na kueleweshwa.

Siasa zimeharibu sana hiki kizazi.
Wamekaririshwa kuwa kila kitu kitakachofanywa na mtu asiyekuwa wao hakifai.
Lazima tuondoe hii notion Tanzania itaendelezwa na watanzania wenyewe, hebu mambo ya dini tubaki nayo mioyoni mwetu.
Maendeleo hayana dini wala chama.
 
Hivi kwa maelezo hayo mtu unaweza ukaelewa kweli nini kusudio la huo mradi? Hebu jaribu kutoa maelezo ya kutosha mtu aelewe na siyo hivyo ulivyoandika. Halafu mbona ukishaweka mabandiko yako unapotea halafu ukirudi kile ulicholeta awali unasema hakikuwa na mafanikio?
 
Vitendo Saccos haijafanikiwa kabisa kuendelea kwa kukosa uongozi na zaidi ni kwa kanuni na shria za ushirika ambazo zunalazimisha kuwe na riba kwenye saccos. Sisi tukashindwa kutilia mkazo kwa hilo kwani vitabu vya dini zetu vinatukataza kula riba. Pia . Ilikuwa ni one man show na jambo kubwa na zito kama hilo lilikuwa linahitaji watu wazoefu wenye mawazo chanya wa kuliendesha. Ni wazo jema sana
"Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha."


Mbona jibu lako hapo linatofautiana na haya maelezo yako uliyoyatoa kuhusu mkutano wenu wa hiyo Saccos 2017?
 
Na ile shule imefikia wapi kwa sasa ili tuje kwenye ujenzi wa nyumba zetu
Hilo lilikuwa baada ya uchaguzi.

Huo uongozi uliochaguliwa ndio ulishindwa kutimiza wajibu wake.
"Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yalioji
 
Hivi kwa maelezo hayo mtu unaweza ukaelewa kweli nini kusudio la huo mradi? Hebu jaribu kutoa maelezo ya kutosha mtu aelewe na siyo hivyo ulivyoandika. Halafu mbona ukishaweka mabandiko yako unapotea halafu ukirudi kile ulicholeta awali unasema hakikuwa na mafanikio?
Uliza ambacho hujaelewa, tutakuelewesha.
 
Mkuu hapo kwenye ujenzi wa tsh 2500 ungefafanua kiupana zaidi ili tukuelewe vizuri.
 
"Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha."


Mbona jibu lako hapo linatofautiana na haya maelezo yako uliyoyatoa kuhusu mkutano wenu wa hiyo Saccos 2017?
Sioni yanapopingana.

Hayo yalikua maelezo ya mkutano wa kwanza wa kuanzisha saccos. Waliochaguliwa hawakuwa watendaji na hawakuwa na shauku ya kujifunza. Wakashindwa.
 
Hahahaaaaa

Dah,kuna kipigo hapa.....

Hii dunia hii,maajabu kabisa...na funny thing is,wanadamu hua wanaamini hizi nonsense,thats the saddest part!
Una fikra potofu.

Watu wameshaanza kufaidika, wewe kalia kuponda tu.

Huu ni mpango wa kipekee Tanzania, hii waachie wenye uelewa waendelee kufaidika.
 
Mkuu hapo kwenye ujenzi wa tsh 2500 ungefafanua kiupana zaidi ili tukuelewe vizuri.
i very simple, unaanza ujenzi kwa kuanzia na Shillingi 2,500 tu. Tunakushauri uje kwetu ujionee wengi walioanza kufaidika. Tumeanza na hapa hapa tulipo, wanaotuzunguka.
 
Shule ipi unaiongelea?

Kuna Abraar Nursery School ambayo ujenzi umenza tayari. Kuna shule ya sekondari ya Vitendo, ambayo ni shule ya Serikali lakini Abraar tumejitolea kuwajengea darasa moja la la vifaa vya kisasa na pia kuna Shule ya Abaraar Mkuranga ambayo ipo kwenye upimaji.

Unaongelea ipi kati ya hizo?
Kwahiyo shule zote zipo kwenye mipango ya kuanza? Nafikiri hilo la shule ya vitendo libaki kuwa mmetoa msaada tu
 
Blah blah blah

Una kibali cha kukusanya hela za wananchi namna hii (uwezekezaji) au unajisahaulisha sheria za nchi?

Hakuna kitu cha maana hapo...anything linked with religion and then linked na "unaweka pesa kidogo tu" halafu blah blah blah...

So sad stupid human beings wanawaaamini....so sad
Njoo ututembelee, unasubiri nini? Hatuna siri. Jionee watu wanavyofaidika...

20210313_103924.jpg




Wewe hutaki kuleta zako uanze kujenga kwa Shillingi 2,500 tu? Mwenzako juu huyo ni mwana mama huyo, tumeanza kukusanya zake vyema kabisa. Ma shaa Allah.

Unakaribishwa, tupo mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha, Pwani. Tanzania na ukipotea nipigie namba zangu 0625249605, namba hizo kwa jina langu. Naitwa "Abdul" Ghafur.

Usiandikie mate na wino upo.
 
Kwahiyo shule zote zipo kwenye mipango ya kuanza? Nafikiri hilo la shule ya vitendo libaki kuwa mmetoa msaada tu
Mbili zimeshaanza na moja tayari, hii hapa, moja ipo kwenye upimaji.

Sisi hatutoi msaadaa kwa shule, tunajisaidia sisi wenyewe tukijenga shule na tukiwawezesha watu kujikomboa kimaisha.

WhatsApp Image 2021-03-19 at 19.32.19.jpeg


Jionee kitu hicho, Ma shaa Allah...
 
Hahahaaa

Eti kujenga kwa 2500/=,nigga are you insane?

Kibali cha kukusanya hiyo 2,500/= kutoka kwa wananchi unacho?Huna

Unajua kinatoka wapi?BOT

Unajua hata BOT ni nini?Hujui

Upo hapa unadanganya majinga menzako na hii ponzi scheme eti nyumba zinajengwa kwa 2,500/=

Acha ukichaa
Huwa hatuandikii mate na wino upo...
jumaa mubarak 2.jpg
 
KWahiyo picha ndio wino?

Hii ni ponzi scheme,the late contributors will suffer the loses

Hata hujui maana ya ponzi scheme,such an idiot aiseee

Yaani mnafanya crime sababu ya ignorance,na kwenye court of law ignorance sio sababu unapigwa mvua za kutosha

You are just clueless kabisa.....

Halafu sad enough huu wizi mmeu-link na dini ili kuupa legitimacy...as always,stupid people are the victims here,so so sad yaani!
Kwa hiyo ulitaka nikuletee nini zaidi ya picha? Si uje ujionee mwenyewe? Ya nini unajificha nyuma ya keyboard na kuponda usiyoyaelewa?

Ponzi wanauza reinforced Concrete Blocks? Na wanakujengea?

Mambo hayoooo...

IMG-20210310-WA0003.jpg


Njoo tu ufaidike, usione tabu kwa kuwa tu huamini macho yako kwa unachokiona na ubongo wako bado hauna uelewa wa kutossha. Tupo kwa ajili ya kuwezesha binaadam wenzetu.

Au tatizo lako ni kuwa ubunifu kama huu unafanywa na watu wa Madrassa? na ni wa kipekee Tanzania, could be duniani. Amazing. Sikuelewi elewi.
 
Na picha ndio udhibitisho?

Kama umepiga mradi wa mtu?ndio udhibitisho?

Wewe mzima kweli?

Nipoteze muda wangu kuja kuangalia mataahira?

Kwa maana wewe upo mbele ya keyboard?

Maana concrete blocks ndio zinauzwa 2,500/=?

Acha ponzi scheme wewe kiazi,fanya kazi halali,acha kukusanya vi 2,500/= vya wananchi eti unatoa ahadi ya nyumba

This is bonafide ponzi scheme,wachangiaji wa mwanzo watafaidika,hasara wanakuja kubeba wachangiaji wa mwisho,

Hiyo ndio ponzi scheme

Acha utaahira!
Tena kuna jingine ambalo linawatesa Watanzania wengi, wazee wa Madrassa tumekuja na solution ya kipekee.

Unakumbuka Jangwani Dar, na mabondeni watu wanahamishwa wakati wa mvua? Sasa hata wewe una ufumbuzi kama una kiwanja cha bondeni. Au tumia fursa hii nunua kiwanja cha bondeni wasichokitaka watu, tuje tukujengee kwa ujenzi wetu wa kipekee, kuanzia Shillingi 2,500 tu...

IMG-20210314-WA0019.jpg



Unangoja nini kijana? Piga 0625249605 Abdul Ghafur tukuelekeze kama hauujui mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha Pwani. Uje kufaidika. Fursa hii ni ya muda tu, wahi, backlog ya ujenzi imeshaanza kufika mwezzi wa kusubiri.
 
"Social Economic Empowerment Program,." Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshana Kiuchumi, Kwa mara ya Kwanza Tanzania. Haujawahi kutokea, duniani.

Ni mpango uliobuniwa na Madrassatul Abraar, iliopo mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha, Pwani Tanzania.

Mpango ulianzishwa nakuasisiwa na Abdul ghafur kwa kujiwezesha kifamilia na marafiki wa karibu kutatua tatizo la kujipatia nyumba za kuishi kwa gharama nafuu.

Kwa kuwa mpango huo umekuwa ni mwema sana, na wenye mafanikio, tukaona kwanini tusiufikishe kwa jamii, tufaidike sote.

Mpango umeleta mafanikio mazuri kuanzia mwanzoni, nyota njema huonekana alfajiri, na umezaa mipango mingine midogo midogo ya kuwezeshana kijamii.

Kwa Sasa mipango tuliyonayo nafanya vyema sana ni kama ifatavyo:

1) Abraar Bricks Nyumba kwa wote.

Mpango huu upo, unaendelea vizuri, unaendeshwa na Madrassatul Abraar chini ya usimamizi wa muasisi, Abdul Ghafur. Nadiriki kusema hili ni wazo la kipekee Tanzania, pengine na duniani. Binafsi sijawahi kuliona wala kusikia wapi limefanyika kama hili. Kama kuna walioliona na au lipo basi wanirekebishe na wanielimishe zaidi.

Kwa Sasa mipangotuliyonayo na inafanya vyema sana ni Abraar Bricks Nyumba kwa wote. Hii ipo na inasimamiwa na kuendeshwa na Madrassatul Abraar chini yangu.

Hili ni wazo la kipekee Tanzania, pengine na duniani. Sijawahi kuona wapi limefanyika kama hili.

Madrasaatul Abraar katika mpango huu, inakuwezesha wewe kujenga kwa kuanzia kwa Shillingi 2,500 tu.

Unaanza kwa kudunduliza kwetu kidogo kidogo, kwa maana ukijiunga tayari inakuwa umenunua kifaa cha ujenzi kimoja, nalo ni jiwe lako la msingi la ujenzi wa kisasa, ujenzi wa gharama nafuu na wenye ubora wa hali ya juu

2) Mafunzo ya kuunda vifaa vya ujenzi na ujenzi wa kisasa.

Mpango huu unawezesha vijana na kina mama kujifunza kazi za ujenzi kuanzia kuunda vifaa vya ujenzi mpaka kujengea. Mafunzo yanatolewa bure na chakula posho ya chakula inatolewa kwa wanafunzi wote wanaojiunga na mpango huu.

Kwa wale ambao tayari mafundi ujenzi, tunawapa ujuzi wa ziada na tunawafundisha kutumia bidhaa mpya za ujenzi, tunawafundisha nidhamu za kazi za ujenzi. Kiufupi, tunawanyanyua kutoka mafundi wa kawaida na kuwa mafundi bora. Bure na posho ya kujikimu kwa siku, kwa siku watazokuwa wanapata mafunzo.

Mafunzo yetu ni ya muda mfupi sana na yenye matokeo chanya na mema sana kwa yeyote mwenye nia ya kujifunza ujenzi au kuongeza ujuzi wa ujenzi3.

Viwanja vya gharama nafuu kwa malipo yasiokuwa na riba.

Kwa mara ya kwanza sasa tunawezesha jamii kujipatia viwanja vya gharama nafuu kwa malipo nafuu yasiokuwa na riba.


Kama u muandishi wa habari au umeguswa japo kidogo na hayo ya juu, unaweza kutupigia simu 0625249605 Abdul Ghafur, kwa maelezo na ufafanuzi wa ziada.

Kuhusu hili la tahadhari ya Benki Kuu, madrassa inasemaje mkuu

https://www.ippmedia.com › node
BoT yawabana wakopeshaji binafsi, Vicoba - IPPMEDIA
10 Jan 2020 — BENKI Kuu ya Tanzania (BoT ), imevitaka vikundi, kampuni au mtu ... "BoT inatoa onyo kwa mtu, kikundi au taasisi yoyote.... : Soma zaidi bofya link: Source: BoT yawabana wakopeshaji binafsi, Vicoba

Abdul Ghafur said : Unaanza kwa kudunduliza kwetu kidogo kidogo, kwa maana ukijiunga tayari inakuwa umenunua kifaa cha ujenzi kimoja, nalo ni jiwe lako la msingi la ujenzi wa kisasa, ujenzi wa gharama nafuu na wenye ubora wa hali ya juu
 
Kuhusu hili la tahadhari ya Benki Kuu, madrassa inasemaje mkuu

https://www.ippmedia.com › node
BoT yawabana wakopeshaji binafsi, Vicoba - IPPMEDIA
10 Jan 2020 — BENKI Kuu ya Tanzania (BoT ), imevitaka vikundi, kampuni au mtu ... "BoT inatoa onyo kwa mtu, kikundi au taasisi yoyote ...
Madrassa haikopeshi wala haikopi. Utakopesha sadaka ndugu yangu? Majanga hayo. Sisi tunawezesha. Sijui wapi ulipata wazo au ulipasoma kuwa tunakopesha hata ukaja na huo waraka wa BOT?

Empowermment ni kuwezesha watu, na jambo ambalo wengi hawalifahamu, empowerment ya kwanza kwa binadam ni kisaikolojia. Kama hujamwezesha mtu kujihisi na kuamini kuwa anaweza basi hata umpe mamilioni hatoweza kuyafanyia kitu.

Cha kwanza tunachofanya Madrassatil Abraar ni kutoa mafunzo, amma kwa anaetaka kujifunza ujenzi au kutengeneza vifaa vya ujenzi, au anaeweza kufundishika akajijengea mwenyewe.

Tuna vifaa na teknolojia ambayo, yeyote mwenye nia, anaweza kujifunza ndani ya mwezi mmoja akawa tayari anajenga mwenyewe. Mradi awe na nia tu.

Kazi yetu kuu ni kufundisha, kama tunavyomfundisha huyo kijana hapo juu.

Hakopeshwi mtu kwetu wala hatuchangisgishi pesa ya mtu.

Mafunzo yetu tunayatoa bure na posho ya chakula Madrassa imejitoleaa kuwapa wanaokuja kujifunza. Ma shaa Allah. Haijwahi kutokea Tanzania mipango hii.
 
Back
Top Bottom