Tofari zetu zenye mwnya kati zina kazi nyingi tofauti na zina faida nyingi tofauti na zipo za aina tofauti.
Kwanza naomba ufahamu kuwa tofari zetu zote ni za zege (cement, mchanga na kokoto) na zina kazi zaidi ya moja.
Zenye mwanya (hollow) kwa sasa zipo za aina tatu tofauti na zote zina kazi zaidi yamoja. Zipo za nchi 12 ambazo ni kazi yake ya kwanza ni kujengeaa nguzo (colums), zipo za nchi 8 kazi yake kuu ya kwanza ni kujengea chini ya ardhi (msingi) wa ukuta au basements. Za nchi nne kazi yake kuu ni kukatia kuta za juu ya ardhi (partitions) na hata kupandishia kuta za nje.
Kazi za ziada za tofari za nchi nane zemye "mwanya' ni kuwa unaweza pia kupandishia ukuta juu au zikawa ni floor slab hali kadhalika kwa zile za nchi 4.
Faida zake, kwanza ni ngumu sana, pili, hazipitishi na hazinywi maji maji kupandisha maji kwenye ukuta. Tatu, ule mwanya unasaidia kuifanya nyumba isipate joto la jua mchana na usiku inafanya usiipate baridi kwa haraka. Ule uwazi ni insulation.
Faida yake nyingine kuu ni unapozitumia kwenye msingi, unakuwa huna haja wala kuingia gharama za mbaoya mbao, misumari au fundi mbao. Na kwa misingi mingi ambayo haizidi kina cha meter moja kwenda chini na hakuna udongo wa kumomomnyoka basi hauhitaji nondo kwenye msingi wako.
View attachment 1765246
Mfano hizo juu zinatumika kama tofari za msingi kabla hazijaongezewa zege kuuimarisha msingi. Na hapa chini zimeongezewa zege...
View attachment 1765248