"Social Economic Empowerment Program" Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi

Shida ya JF ya nyakati hizi kuna watu wako huku kazi yao kubwa ni kupinga kila kitu bila hata kuhoji na kueleweshwa.

Siasa zimeharibu sana hiki kizazi.
Wamekaririshwa kuwa kila kitu kitakachofanywa na mtu asiyekuwa wao hakifai.
Lazima tuondoe hii notion Tanzania itaendelezwa na watanzania wenyewe, hebu mambo ya dini tubaki nayo mioyoni mwetu.
Maendeleo hayana dini wala chama.
 
Hivi kwa maelezo hayo mtu unaweza ukaelewa kweli nini kusudio la huo mradi? Hebu jaribu kutoa maelezo ya kutosha mtu aelewe na siyo hivyo ulivyoandika. Halafu mbona ukishaweka mabandiko yako unapotea halafu ukirudi kile ulicholeta awali unasema hakikuwa na mafanikio?
 
"Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yaliojiri mtajionea mkanda wa video.

Baada ya semina ukaanza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa muda. Ulioendeshwa na kusimamiwa na Afisa Ushirika kama sheria zinavyotaka.

Hatimae tukapata kamati ya uongozi wa muda ya uanzilishi wa Vitendo SACCOS Ltd., kwa mujibu wa Sheria na chini ya usimamizi wa Afisa Ushirika wilaya ya Kibaha."


Mbona jibu lako hapo linatofautiana na haya maelezo yako uliyoyatoa kuhusu mkutano wenu wa hiyo Saccos 2017?
 
Na ile shule imefikia wapi kwa sasa ili tuje kwenye ujenzi wa nyumba zetu
Hilo lilikuwa baada ya uchaguzi.

Huo uongozi uliochaguliwa ndio ulishindwa kutimiza wajibu wake.
"Yalizuka maswali mengi kiasi na hususan lilipoongelewa suala la kuendesha saccos kwa riba.

Hatimae kila mtu akaelewa kuwa hakuna tatizo kubwa isipokuwa ni namna tu ya mfumo wa uendeshaji SACCOS bila riba utavyofanyika.

Hilo na mengine yalioji
 
Uliza ambacho hujaelewa, tutakuelewesha.
 
Mkuu hapo kwenye ujenzi wa tsh 2500 ungefafanua kiupana zaidi ili tukuelewe vizuri.
 
Sioni yanapopingana.

Hayo yalikua maelezo ya mkutano wa kwanza wa kuanzisha saccos. Waliochaguliwa hawakuwa watendaji na hawakuwa na shauku ya kujifunza. Wakashindwa.
 
Hahahaaaaa

Dah,kuna kipigo hapa.....

Hii dunia hii,maajabu kabisa...na funny thing is,wanadamu hua wanaamini hizi nonsense,thats the saddest part!
Una fikra potofu.

Watu wameshaanza kufaidika, wewe kalia kuponda tu.

Huu ni mpango wa kipekee Tanzania, hii waachie wenye uelewa waendelee kufaidika.
 
Mkuu hapo kwenye ujenzi wa tsh 2500 ungefafanua kiupana zaidi ili tukuelewe vizuri.
i very simple, unaanza ujenzi kwa kuanzia na Shillingi 2,500 tu. Tunakushauri uje kwetu ujionee wengi walioanza kufaidika. Tumeanza na hapa hapa tulipo, wanaotuzunguka.
 
Kwahiyo shule zote zipo kwenye mipango ya kuanza? Nafikiri hilo la shule ya vitendo libaki kuwa mmetoa msaada tu
 
Njoo ututembelee, unasubiri nini? Hatuna siri. Jionee watu wanavyofaidika...





Wewe hutaki kuleta zako uanze kujenga kwa Shillingi 2,500 tu? Mwenzako juu huyo ni mwana mama huyo, tumeanza kukusanya zake vyema kabisa. Ma shaa Allah.

Unakaribishwa, tupo mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha, Pwani. Tanzania na ukipotea nipigie namba zangu 0625249605, namba hizo kwa jina langu. Naitwa "Abdul" Ghafur.

Usiandikie mate na wino upo.
 
Kwahiyo shule zote zipo kwenye mipango ya kuanza? Nafikiri hilo la shule ya vitendo libaki kuwa mmetoa msaada tu
Mbili zimeshaanza na moja tayari, hii hapa, moja ipo kwenye upimaji.

Sisi hatutoi msaadaa kwa shule, tunajisaidia sisi wenyewe tukijenga shule na tukiwawezesha watu kujikomboa kimaisha.



Jionee kitu hicho, Ma shaa Allah...
 
Huwa hatuandikii mate na wino upo...
 
Kwa hiyo ulitaka nikuletee nini zaidi ya picha? Si uje ujionee mwenyewe? Ya nini unajificha nyuma ya keyboard na kuponda usiyoyaelewa?

Ponzi wanauza reinforced Concrete Blocks? Na wanakujengea?

Mambo hayoooo...



Njoo tu ufaidike, usione tabu kwa kuwa tu huamini macho yako kwa unachokiona na ubongo wako bado hauna uelewa wa kutossha. Tupo kwa ajili ya kuwezesha binaadam wenzetu.

Au tatizo lako ni kuwa ubunifu kama huu unafanywa na watu wa Madrassa? na ni wa kipekee Tanzania, could be duniani. Amazing. Sikuelewi elewi.
 
Tena kuna jingine ambalo linawatesa Watanzania wengi, wazee wa Madrassa tumekuja na solution ya kipekee.

Unakumbuka Jangwani Dar, na mabondeni watu wanahamishwa wakati wa mvua? Sasa hata wewe una ufumbuzi kama una kiwanja cha bondeni. Au tumia fursa hii nunua kiwanja cha bondeni wasichokitaka watu, tuje tukujengee kwa ujenzi wetu wa kipekee, kuanzia Shillingi 2,500 tu...




Unangoja nini kijana? Piga 0625249605 Abdul Ghafur tukuelekeze kama hauujui mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha Pwani. Uje kufaidika. Fursa hii ni ya muda tu, wahi, backlog ya ujenzi imeshaanza kufika mwezzi wa kusubiri.
 

Kuhusu hili la tahadhari ya Benki Kuu, madrassa inasemaje mkuu

https://www.ippmedia.com › node
BoT yawabana wakopeshaji binafsi, Vicoba - IPPMEDIA
10 Jan 2020 — BENKI Kuu ya Tanzania (BoT ), imevitaka vikundi, kampuni au mtu ... "BoT inatoa onyo kwa mtu, kikundi au taasisi yoyote.... : Soma zaidi bofya link: Source: BoT yawabana wakopeshaji binafsi, Vicoba

Abdul Ghafur said : Unaanza kwa kudunduliza kwetu kidogo kidogo, kwa maana ukijiunga tayari inakuwa umenunua kifaa cha ujenzi kimoja, nalo ni jiwe lako la msingi la ujenzi wa kisasa, ujenzi wa gharama nafuu na wenye ubora wa hali ya juu
 
Madrassa haikopeshi wala haikopi. Utakopesha sadaka ndugu yangu? Majanga hayo. Sisi tunawezesha. Sijui wapi ulipata wazo au ulipasoma kuwa tunakopesha hata ukaja na huo waraka wa BOT?

Empowermment ni kuwezesha watu, na jambo ambalo wengi hawalifahamu, empowerment ya kwanza kwa binadam ni kisaikolojia. Kama hujamwezesha mtu kujihisi na kuamini kuwa anaweza basi hata umpe mamilioni hatoweza kuyafanyia kitu.

Cha kwanza tunachofanya Madrassatil Abraar ni kutoa mafunzo, amma kwa anaetaka kujifunza ujenzi au kutengeneza vifaa vya ujenzi, au anaeweza kufundishika akajijengea mwenyewe.

Tuna vifaa na teknolojia ambayo, yeyote mwenye nia, anaweza kujifunza ndani ya mwezi mmoja akawa tayari anajenga mwenyewe. Mradi awe na nia tu.

Kazi yetu kuu ni kufundisha, kama tunavyomfundisha huyo kijana hapo juu.

Hakopeshwi mtu kwetu wala hatuchangisgishi pesa ya mtu.

Mafunzo yetu tunayatoa bure na posho ya chakula Madrassa imejitoleaa kuwapa wanaokuja kujifunza. Ma shaa Allah. Haijwahi kutokea Tanzania mipango hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…