"ghiriba" ndio nini? Au ulitaka kuandika "ghilba"? Kasome kwanza uelewe kuandika vizuri Kiswahili, maana neno usilolielewa kuandika hata maana yake inaonesha huielewi, umejiandikia tu mradi na wewe uonekane waamo.Hebu turudi nyuma, tusome hila na ghiriba zako. Je twaruhusiwa?
Hao ni kijiba tu cha roho, achana nao hao. Tuachie sisi tunaelewa hizo lugha zao za kiroho mbaya. Usongo tu umewashika.Sujakuelewa hiyo "Je twaruhusiwa?"
Unakusudia nani kuruhusiwa au nani asieruhusiwa?
Weka namba tuanze kutuma hiyo 2,500 faster tujengewe nyumbaUmeelewa lakini huamini.
Ndio, kwa Shillingi ,2500 (elfu mbili na mia tano) tu unaanza ujenzi wa nyumba yako tena, yenye ubora wa hali yajuu na ghorofa juu.
Umefufuka ngariba wa JF"ghiriba" ndio nini? Au ulitaka kuandika "ghilba"? Kasome kwanza uelewe kuandika vizuri Kiswahili, maana neno usilolielewa kuandika hata maana yake inaonesha huielewi, umejiandikia tu mradi na wewe uonekane waamo.
Au ndio kijiba cha roho?
Kwanza napenda kukufahamisha kuwa hatupokeai pesa mpaka ufike kwetu tukubaliane namna ya kuwezeshana na tuwe na mkataba.Weka namba tuanze kutuma hiyo 2,500 faster tujengewe nyumba
TakbiirMzingatie na elimu dunia pia.
Hongera kwa kazi nzuri ndugu.
Ujue kuna utaratibu ambao hardware nyingi hutumia ambao mteja hununua vifaa vya ujenzi kidogokidogo ukifikia lengo unachukua mzigo na kupeleka site kwa ujenze.
Je, huu utaratibu wako wa 2,500/- ni kama huu yaani mtu anatoa pesa wee hadi itimie gharama ya matofali kadhaa ndio anafata ama inakuaje hasa..?
Hebu funguka juu ya hili maana haMingii akilini mtu atoe 2,500/- tu hapohapo na muanze kumjengea.
Of course vifaa vya ujenzi, iunatoa 2,500 unapata kifaa cha ujenzi. Kama hauna pa kukiweka tunakuwekea, vikitimia kumi tunakuja kuanza kukujengea. Unadunduliza kidogo kidogo.
Huu ni mpango wa kipekee, haujwahi kutokea. Si lazima uwe na mamilioni ndio uanze kujenga, unaanza kwa Shillingi 2,500 tu...
View attachment 1735662
Hivyo vifaa vya mtu anadunduliza.
Tofari zetu zenye mwnya kati zina kazi nyingi tofauti na zina faida nyingi tofauti na zipo za aina tofauti.Naomba kufahamu kuhusu hizo tofali Zenye mwanya katikati, 1. Je matumizi ya cement wa Kati wa ujenzi ukilinganksha na za kawaida. 2. Dhumuni la mwanya katikati ni kufanya bei ya Tofali ipungue ama ile nafasi inamatumizi maalum? Na nini maana ya Reinforcement concrete blocks?
Tofari zetu zenye mwnya kati zina kazi nyingi tofauti na zina faida nyingi tofauti na zipo za aina tofauti.
Kwanza naomba ufahamu kuwa tofari zetu zote ni za zege (cement, mchanga na kokoto) na zina kazi zaidi ya moja.
Zenye mwanya (hollow) kwa sasa zipo za aina tatu tofauti na zote zina kazi zaidi yamoja. Zipo za nchi 12 ambazo ni kazi yake ya kwanza ni kujengeaa nguzo (colums), zipo za nchi 8 kazi yake kuu ya kwanza ni kujengea chini ya ardhi (msingi) wa ukuta au basements. Za nchi nne kazi yake kuu ni kukatia kuta za juu ya ardhi (partitions) na hata kupandishia kuta za nje.
Kazi za ziada za tofari za nchi nane zemye "mwanya' ni kuwa unaweza pia kupandishia ukuta juu au zikawa ni floor slab hali kadhalika kwa zile za nchi 4.
Faida zake, kwanza ni ngumu sana, pili, hazipitishi na hazinywi maji maji kupandisha maji kwenye ukuta. Tatu, ule mwanya unasaidia kuifanya nyumba isipate joto la jua mchana na usiku inafanya usiipate baridi kwa haraka. Ule uwazi ni insulation.
Faida yake nyingine kuu ni unapozitumia kwenye msingi, unakuwa huna haja wala kuingia gharama za mbaoya mbao, misumari au fundi mbao. Na kwa misingi mingi ambayo haizidi kina cha meter moja kwenda chini na hakuna udongo wa kumomomnyoka basi hauhitaji nondo kwenye msingi wako.
View attachment 1765246
Mfano hizo juu zinatumika kama tofari za msingi kabla hazijaongezewa zege kuuimarisha msingi. Na hapa chini zimeongezewa zege...
View attachment 1765248
Tumezoea kuzoea mazoea, kuna wakati tunabidi tufikirie nje ya sanduku, kwanza tuache kuitana majina mabaya, kwani jina baya humuua mbwa, halafu tuwe na dhana njema kwa kila mmoja wetu, ikiwa unadhani kuna mtu anaweza kudhulumu au kudhulumiwa katika mradi huu basi jaribu kuelewana na muhusika ili upate kujihakikishia ukweli, utekelezaji na uhalisia wa mradi wenyewe huenda ukawa na fikra bora zaidi za kuboresha mradi huu kwani nia ya mradi ni mtu kupata makazi kwa gharama nafuu, kutoa elimu ya ujenzi bora na wa gharama nafuu na kutoa ajira, kwa kweli ikiwa tutaweza kuungana mkono bila shaka hatatokea mtanzania mwenye kukosa nyumba ya kuishi.Sisemi kufundishwa kujenga ni vibaya. Hata wamisionari walitufundisha elimu lakini haikutusaidia kitu ikilinganishwa na ukoloni waliouwezesha. Hizi dini zimeua mila na namna yetu ya kuishi na kutufanya mafala tunaotegemea pepo katika umaskini wa kutengenezwa nazo. Kwanini sisi tusiende kuwasaidia hao waarabu na wairani au wazungu wakati tumejaliwa raslimali nyingi kuliko wao? Blessed is the hand that giveth than the one that taketh mwanangu.
Ikiwa unatokea Dar mjini, unapanda basi la kuja Mbezi Mwisho, hapo utapata mabasi ya kwenda Mlandizi. Unapanda basi la kwenda Mlandizi, unashuka kituo kinaitwa Miyomboni shule au Misugusugu shule ya Msingi, usishuke Misugusugu check point.Asante sana kwa ufafanuzi naamini ninaweza kuwa na mengi ya kujifunza ila nimeridhika kwa kiasi fulani je unaweza kuelekeza jinsi ya kufika ofisini kwenye maana sipajui misugusugu ni wapi labda na panda basi la wapi nashukia wapi?
Unakaribishwa kuja kujioneaa huo unaouita "ugaidi" na tunakuomba baada ya kututembelea na kujionea yaliopo urudi hapa kutangaza ulichokikuta. Ruksa kuja na camera kupiga picha zetu, za tunachokifanya na au za chochote utachokikuta hapa. Kwa sharti tu urudi hapa kukiandika ulichokikuta.Sisemi kufundishwa kujenga ni vibaya. Hata wamisionari walitufundisha elimu lakini haikutusaidia kitu ikilinganishwa na ukoloni waliouwezesha. Hizi dini zimeua mila na namna yetu ya kuishi na kutufanya mafala tunaotegemea pepo katika umaskini wa kutengenezwa nazo. Kwanini sisi tusiende kuwasaidia hao waarabu na wairani au wazungu wakati tumejaliwa raslimali nyingi kuliko wao? Blessed is the hand that giveth than the one that taketh mwanangu.
Samahaniii hiyo nauli- kutoka kibaha Hadi hapo madrasa ni 10000 kwa pikipiki au umekosea kuandika ulimaanisha 1000Unakaribishwa kuja kujioneaa huo unaouita "ugaidi" na tunakuomba baada ya kututembelea na kujionea yaliopo urudi hapa kutangaza ulichokikuta. Ruksa kuja na camera kupiga picha zetu, za tunachokifanya na au za chochote utachokikuta hapa. Kwa sharti tu urudi hapa kukiandika ulichokikuta.
Achana na fikra hasi, hazitakuendeleza wewe wala wanaokuzunguka.
Kwa kukujulisha zaidi; Kuna vija zaidi ya 25 waliofaidika na kumaliza mafunzo ya awali ya mwezi mmoja. Wengine wameamua kuendelea na mafunzo ya ziada (kupata uzoefu). Kuna mafundi waliojifundisha ufundi kivyao na waliokuwa wakifanya kazia zao za ufundi, kwa miaka mingi, waliojiandikisha mafunzo yetu, wameamua kubaki hapa hapa na kufundisha wanaokuja wapya.
Tunashukuru tumefanikiwa vizuri sana katika miezi yatu miwili ya mwanzo, kiasi sasa tuna wanafunzi wapya wanajiandikisha kwa uwiano wa mwanafunzi mmoja mpya kila siku. Mpaka inabidi wengine wasubiri na inabidi tuongeze madarasa na shifts za kufundisha ili kila mmoja afaidike kwa wakati.
Kumbuka, hapa kwetu ni mafunzo kwa vitendo, sio kwa porojo.