Ukiangalia kule China kwenye chimbuko la Korona, wamepambana wenyewe hadi kufanikiwa kuudhibiti huu ugonjwa kwa asilimia 90. Ukienda kule Urusi, ndiyo amekuwa DONOR wa kutoa misaada ya madawa ya Korona na vifaa kwa asilimia kubwa, hadi kutuma watalaamu wake na vifaa vyote vya TIBA kuwanusuru Waitaliano.
Chukulia Cuba kwa upande mwingine ndiyo amekimbia kwenda Ulaya kumpa Mtaliano msaada bila kujali kuna NATO wala Jumuiya ya Ulaya, hakuna aliyekuwa na msaada wa kumsaidia mwenzake hadi baba lao Marekani limepiga magoti kwa Urusi na China.
Ukija hapa Afrika utaikuta Tanzania ukumbuke nayo ilikuwa kwenye mifumo hiyo hiyo huko siku za nyuma na rafiki wa hizo nchi tatu tajwa hapo juu. Nimebaki najiuliza huu ugonjwa kuna mkono wa hizi nchi za Ki - Socialist?
Mbona zenyewe tayari zilikuwa na vifaa, mbona kwa Tanzania WATU waliambiwa wasihofu na waendelee kupiga kazi na inaonekana maambukizi yamekuwa hayana nguvu saana ukilinganisha na nchi zingine zilizoko kwenye ukanda mmoja na Tanzania? Hadi kuna baadhi ya majirani walifunga mipaka mapema tu, lakini ndo hilo gonjwa likazidi kusambaa zaidi.
Je, kuna siri ndani yake kuhusu hizi nchi za mlengo wa Ki - Socialist (CHINA, RUSSIA, CUBA na Tanzania kwa Mbali)? Ilikuwaje wakawa na dawa na vifaa vya kuhudumia Dunia nzima huku wengine kwa ukanda wetu huku wakiambiwa WASIHOFU na waendelee tu KUCHAPA KAZI?
Sent using
Jamii Forums mobile app