Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

Mkuu nakushauri umuone psychiatrist, atakupa anti depressants,ukizitumia kama alivyokuelekeza hilo tatz linaisha chap.
Anti depressant hizi ni barbiturates akizi abuse hizi Dawa zinaweza kusababisha kifo ndani ya dakika 15.
 
Mbona kama nina vitu hivyo vya hisia
 
ahsante sana mkuu kwa kitabu hiki kizuri.. be blessed
 
Mkuu naomba kiweke upya
 
Maiti,

Fortunately, una tatizo ambalo linaweza tibia hospital
1) Psychotherapy
2) Anti-Depressants(anti-anxienty): Amitryptilline au Fluoxetine

The only place utapata msaada trust me ni hospital na kama upo Dar watafute ma psychologist na ma psychiatrist unaweza mpaka kuomba private sessions kama hauwezi kwenda hospitali

Kikubwa uwe na Good insight kukubali kuwa unaumwa na ugonjwa wako unawezwa ponywa na maelezo niliyoyatoa!
 
Mkuu Nina tatizo Kama lako,

Siwezi kukaa kwenye makundi ya watu wengi, muda mwingine unajilazimisha kupiga stori na watu unaona kama hawakusikilizi unaona isiwe tabu naondoka zangu ila nikifika kwangu nakua na amani zaidi, Basi hapo nitacheza games nitaangalia movie nitasikiliza album za Eminem karibu zote mara giza lishaingia, alafu usingizi hauji kwahiyo nitapitapita Jamii Forums mpaka saa 8 ndio najaribu kulala, halafu naamka mapema kama ni wikiendi ni mwendo wa muvi yaani bandika bandua.

Nina marafiki wachache sana Ila hata ukiwaambia watakuona wa ajabu unanyamaza kimya sababu hakuna atakaye kusikiliza akakuelewa, muda mwingine unajaribu kuwa normal Kama wale ili uendane na mazingira lakini wapi tabia yako itabaki palepale,

Nikajua peke yangu ndio naishi hivi kumbe tupo wengi, ila Mimi sitojaribu kujiua never
sababu naona kawaida japo watu wananiona Kama nalinga Mara huyu kaka mpole Sana, ila watu wakiniambia nalinga roho inaniuma sana sema nawapotezea tu , ila wakati mwingine Hali hii inachosha mpaka unajiuliza kwanini mimi.

Ushauri wangu
Kwakua hupendi kuishi hivyo huna budi kujitoa, ila Mimi imeshindikana nimeamua kujikubali nilivyo maisha yanaenda.
 

asante sana mkuu kwa ushauri ntafanyia kazi
 
POLE SANA ,, nakushauri ujitahidi kujumuika na vijana wengine katika shughuli mbalimbali kama vile michezo,burudani na hata milo ya pamoja , hii itakusaidia kubadili mtazamo wako na pia kukupunguzia msongo, pia jitahidi kuwashirikisha watu unaowaamini( you are an introvert but try to change that attitude) kufunguka kutakusaidia sana. Jitahidi pia kurudisha imani yako kwa MUNGU' Naamini hakuna kinachoshindikana
 
Nashukuru mkuu ni wachache sana wenye kuelewa hili tatizo wengi wanachukulia simple sana sababu hawajakumbana nayo na hawajui how i feel it. Ni bora kuishi na mguu mmoja huku ukijua kabisa niko na mguu mmoja and am proud of it kuliko kuwa na hayo matatizo ni zaidi ya kutokuwa na miguu yote!
 
Ni kweli kabisa.
Pole sana mkuu Ushajaribu meditation.
Kama bado au ulishindwa...
Kama ni ngumu nenda kaokoke tu uwe mlokole..ukahubiri injili ya vikundi vijijini ukutane na mikiki mikiki huko uta recover polepole.

Naskia huko ndo mwisho wa tatizo kama lako.
 
Kuna mtu alinishauri hiko kitu nimejaribu na naendelea kujaribu mkuu sema kwa sasa kila nikifanya meditation nahisi akili yangu haitulii yani haifocus kwenye kitu kimoja labda kwa kuwa bado ni mwanafunzi kwenye meditation sijui? Ila kama hii njia inafanya kazi basi labda after 3 months ndo ntaona matokeo. Pia mi imani yangu sio ya kikristo. Asante kwa ushauri wenye busara.
 

Ok
Pitia hapa upate twisheni kidogo.

 
Hiki kitabu Ni kizuri sana yaaani nilipata kukisomaa baada changamoto flani hv kili nisaidia Sana nikiwa ughaibuni huko
 
Avriel, Asilimia ya 80% ya ushauri uliotolewa humu unahusu kusoma vitabu na mimi sio mpenzi wa kusoma vitabu nahitaji practical zaid kuliko kukremisha vitabu
 

Maiti Hii itakusaidia kuyafikia malengo yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…