Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

concordile 101,

Asante sana mkuu wangu kwa ushauri mzuri ulionipa. Moja ya vitu navyovikwepa kwa sasa ni kwenda bar maana najua nitashawishika kunywa bia na hapo ndipo kwa mara ya kwanza katika maisha yangu kuanza kuwa mlevi wa kupindukia.

Kwa sasa hata wine sinywi kama nilivyosema hapo awali kuwa naogopa nikitumia kilevi cha aina yoyote sitaacha. So kama unanishauri niende bar au nianze kunywa wine ili nipone taratibu sawa ntajaribu nifanye hivo na nitaleta mrejesho what happened after that.
 
Pole sana kwa mitihani inayokuandama, ila futa hio dhana kichwani mwako kwamba wewe ni binadamu wa ajabu, wewe sio wa ajabu wala hujaonewa, I know it hurts ila you have to be Strong, matatizo tumeumbiwa wanadamu. Kila mmoja ana majanga yake tukianza kuelezea matatizo yetu kila mmoja yanamshinda mwenzie, kuwa na Subira na umlilie Mungu wako akuondolee mitihani inayokukabili.

Asante sana mkuu wangu kwa kunipa moyo. Ubarikiwe.
 
Tatizo dogo sana hilo bwana Maiti
Kwa mtu ambae haelewi hilo tatizo liko vipi hawezi kukupa ushauri utaokuridhisha. Ila mimi hilo tatizo lilinitesa more than 20 years ila niliwin kirahisi mno hadi sasa mimi ni next level kabisa.

Najua humu umelileta na wako wanaokushauri utafute watu uwaelezee it all means kwamba umfate mtu umueleze how u feelin? Kwa hilo tatizo nakuapia hutaweza kumfuata mtu ukamwambia kwa hofu mtu atakuonaje au atakuhisi vibaya.

Ila mimi kuna dokta anaishi Chicago ndio alinisaidia sana kwa kutumia chatting tuu za Yahoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu. hiyo ni moja ya sababu kubwa inayonifanya nikae kimya. na nivyokuwa mkimya zaidi ndipo nazidi kuathirika anxiety inakuwa kubwa zaidi naishia kujifungia nyumbani.

Watu wengi sana Duniani wanasumbuliwa na Anxiety Disorder, Zikichangiwa na Stress, Traumatic Experiences, pole sn naelewa unavojiskia, na inachouma zaidi ni kwamba watu wako wa karibu hawakuelewi unavojisikia. Lakini ni vizuri ulivojigundua kama una tatizo hili na upo tayari kulitaftia ufafanuzi na tiba. Kuna watu wengine hata hawajui kama ni wagonjwa. I hope utapata msaada kwa Dr. Wansegamila
 
What if watu wanaomzunguka sio wasiri? Yaani akiwaelezea matatizo yake wanaweza kuyatangaza kwa wengine.. Una ushauri gn juu ya hilo?
That's why nilimshauri aende hospitali tu yoyote, aingie chumba cha daktari yoyote tuu, aweze kuongea nae (kwa sababu huyo daktari atakua hafahamiani nae) ila alionyesha kutoamini hospitali kwamba ziko after money.
 
Mama Sabrina, kiukweli naamini sana kwa wanawake katika kumbadilisha mtu ila nikuulize hivi, ni mwanamke gani anaeweza kuishi na man ambaye hajiamini? Ni mwanamke gani anayeweza kuishi na man ambaye amekata tamaa ya kimaisha, sipo tayari kumpa mzigo mwanamke yeyote ambaye hastahili kwa hilo. Huwa nakaa nawaza kuwa kwa maisha nayopitia sasa sitathubutu mwanangu aishi nilivyo/navyoishi sasa incase Mungu akanibariki niwe na mahusiano.
 
adden, Shukran mkuu wangu kwa ushauri wako ila nikukumbushe tu kwamba binadamu tupo tofauti sana, wewe ulisaidiwa through chatting ila mimi naamini kwangu maongezi ya ana kwa ana ni bora zaidi kuliko maandishi/messaging
 
Mama sabrina, kiukweli naamini sana kwa wanawake katika kumbadilisha mtu ila nikuulize hivi, >>> ni demu gani anaeweza kuishi na man ambaye hajiamini? ni dem gani anayeweza kuishi na man ambaye amekata tamaa ya kimaisha, sipo tayari kumpa mzigo mwanamke yeyote ambaye hastahili kwa hilo. Huwa nakaa nawaza kuwa kwa maisha nayopitia sasa sitathubutu mwanangu aishi nilivyo/navyoishi sasa incase Mungu akanibariki niwe na mahusiano.
Unatakiwa ujichanganye kwanza ,kama unajipenda na unataka ubadilike la sivyo wewe mwenyewe ndio unajiletea shida ,au badili mazingira hama kwa muda hapo unapokaa nenda mji mwingine inasaidia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
That's why nilimshauri aende hospitali tu yoyote, aingie chumba cha daktari yoyote tu, aweze kuongea nae (kwa sababu huyo daktari atakua hafahamiani nae) ila alionyesha kutoamini hospitali kwamba ziko after money.

Huenda amesema hivyo kwakuwa amejielezea kwamba yy hana kazi wala ajira rasmi labda anaogopa hizo hospitali zitahitaji atoe hela nyingi na yeye hatoweza kumudu na kuendelea kufuga tatizo lake. Labda umsaidie kwa Kurecommend hospitali gani ambayo anaweza akapata msaada kwa bei nafuu.
 
Huenda amesema hivo kwakua amejielezea kwamba yy hana kazi wala ajira rasmi labda anaogopa hizo hosptl zitahitaji atoe hela nyingi na yy hatoweza kumudu na kuendelea kufuga tatizo lake. Labda umsaidie kwa Kurecommend hosptl gn ambayo anaweza akapata msaada kwa bei nafuu.
I can do that. Naweza kurecommend hospitali na hata daktari ambae anaweza kwenda kuongea nae bila kuchajiwa hata senti moja. LAKINI, He has to be ready for it; na yeye mwenyewe aamini kwamba atasaidika. Yeye mwenyewe ndio inabidi a initiate hicho kitu. Otherwise itakua kama kumpeleka ng'ombe mtoni, uamuzi wa kunywa maji unabaki ni wa kwake. min92
 
I can do that. Naweza kurecommend hospitali na hata daktari ambae anaweza kwenda kuongea nae bila kuchajiwa hata senti moja. LAKINI, He has to be ready for it; na yeye mwenyewe aamini kwamba atasaidika. Yeye mwenyewe ndio inabidi a initiate hicho kitu. Otherwise itakua kama kumpeleka ng'ombe mtoni, uamuzi wa kunywa maji unabaki ni wa kwake. min92

Nakuja pm mkuu.
 
Maiti,
Hapana sikushawishi uwe mlevi. Kwenda bar kuna vinywaji vingi tu unaweza tumia na usilewe, njia ya kwenda bar ni ili kukufanya uanze kupata uzoefu na watu. Maana sioni sehemu ambayo ningekushauri uende ambapo utakutana na watu wengi.

Kanisani ndio utaenda lakini, huko zaid ya kusikiliza huwezi pata ongea. Wewe inahitajika ukutane na watu ambao watakufanya uongee, na sio ukienda ufike na akili ya kunywa tu, unaweza fika pale ukaagiza kinywaj letsay sweet wine yenye kiwango kidogo sana cha ukevi.

Tuchukulie mfano Dodoma au St. Anna ukawa unakunywa huku unacheck mpira labda au uko kwa net. Ukishachangamka mwili. Piga zako rapa home kulala ukifanya mwezi lazima utapata marafiki tu Muhimu kwako sio kila mlevi awe rafiki
 
I can do that. Naweza kurecommend hospitali na hata daktari ambae anaweza kwenda kuongea nae bila kuchajiwa hata senti moja. LAKINI, He has to be ready for it; na yeye mwenyewe aamini kwamba atasaidika. Yeye mwenyewe ndio inabidi a initiate hicho kitu. Otherwise itakua kama kumpeleka ng'ombe mtoni, uamuzi wa kunywa maji unabaki ni wa kwake. min92

Mungu akubariki Doctor kwa roho yako nzuri na utu👏👏
 
Dah.. I feel you brother, yaan umezungumza mambo 95% nnayopitia pia.

It really hurts and disturbs you internally, in addition kwa upande wangu hata kusalimia watu barabarani ni mziki, na ni majirani zangu!

Hapa nilipo, I'm on a verge of dropping my university studies, nikisikia presentation au group discussion dah naishiwa pozi kabisa.. Na hata nikishiriki hua siwezi kabisa kuchangia mada hata kama majibu ninayo kichwani!

Natamani nipate kazi nikakae huko mbali na nyumbani, nisionane na watu mara kwa mara, at least I can reach a certain level of comfortability nikiwa peke yangu..

Kukiwa na sherehe au nikiagizwa kwenda sehem yenye mikusanyiko wa watu, yan natamani hata niumwe ili nisiende..

Inakwaza sana, kuna siku nilionana na mjomba wangu (my favorite uncle honestly), tulikaa for more than 4 hours muda wote huo nilikua kwenye debate kali kichwani mwangu, "nimwambie au nisimwambie?, nikimwambia atanichukuliaje?, what if atanijibu tu nipamambane na hali yangu bila kuchukulia hii hali yangu kwa " uzito" unaostahili? " mpaka tunaondoka eneo lile sikusema lolote kuhusu shida yangu..

Dah hili ni janga jaman, mtu ukimwambia anachukulia simple, anakwambia" we jichanganye na watu tu utapona" hua natamani ingekua rahisi kama mnavyosema..

Maiti
 
SHOOyaKIBABE,

Kweli mkuu wangu, wengi hawaamini hii hali wanahisi ni simple sana ila tunapambana na vita moja kubwa sana katika maisha yetu. Kiukweli nimeshindwa kuongea na my relatives kwa sababu most of them wanaonekana hawaamini kwenye hili tatizo pia hawana msaada kwangu.
 
Nimewahi kupitia changamoto kama hiyo; suluhisho kama wewe ni mkristo tafuta kanisa lenye wokovu ambalo unaweza kusikilizi habari njema; sikilizi audio za watumishi na watu wanaotia moyo kwenye Youtube zipo nyingi sana, hakikisha muda wote unasikiliza habari njema tu, ukiona mtu anakuchanganya au anakusema vibaya mpuuze kabisa, hakikisha unavaa vizuri kama mtoto wa mfalme; vaa uvutie hasa, ukipata nafasi ya kwenda out nenda sehemu kama jangwani beach clubs
Unacheza mziki hata kama hunywi we jichanganye tu utazoea.

Hakikisha chumba chako ni kisafi na kuna muziki mzuri na kama unaweza kuwa na tv nzuri na vitu vingine vya ndani vizuri kuwa navyo automatic hapo utapata mwanamke anayefanana nawe; utaanza kupata mtu wa kumsikiliza then hakikisha unapata chalula kizuri unachopenda hapa nakushahuri wekeza kwenye ulaji wa matunda na asali pia; kwa hayo tu naamini wasiwasi utaisha kwa asilimia kubwa
 
Back
Top Bottom