Soda zimeisha mtaani!

Soda zimeisha mtaani!

Yaani ni balaa[emoji28][emoji28] soda zikishushwa mnaanza kugombea aah maji yenyewe uhai yameadimika, afya naomyo adimu
Geita kama unanunuaga crates za soda basi tegemea kampuni ya Pepsi tu, coke adimu wakati mwingine
 
Chupa zote za soda, bia, konyagi na K Vant hutengenezwa Kioo Ltd chupa zipo kibao.
Kwanza soda huuziwi kama huna chupa, iweje ziadimike?
Nadhani hujaelewa lengo la hii thread

Ngoja wadada watakuja kukuelewesha...

Navyojua mimi viwanda vimejikita kutafuta kemikali bora zaidi ya kuosha chupa
 
Nadhani hujaelewa lengo la hii thread

Ngoja wadada watakuja kukuelewesha...

Navyojua mimi viwanda vimejikita kutafuta kemikali bora zaidi ya kuosha chupa
Haah haha haha hahah au ngomosi zinamaliza chupa kwa ajili ya friction?
 
Tatizo la soda sio dar ni Tanzania nzima,
mm ni agent mkoa fulani kwa kipindi cha nyuma tulikuwa tunapewa kreti 1500 kwa siku ila kwa sasa ni kreti 3000 kwa wiki na hapo unategemea kuhudumia zaidi ya stockist 10 wa eneo hilo.
 
Nimezunguka kwenye depots zaidi ya tatu nimekosa kabisa soda kwa ajili ya biashara.

Wenye depots hata wao hawajui adimiko la soda linatokana na nini, licha ya kwamba viwanda viko mkoa huu huu.

Kwa siku za karibuni tumeona mahisimu wa mama wakitoa kelele mbalimbali ili tu mama aonekane ameshindwa kusongesha jahazi.

Mahasimu hao wasije fanya hiana na michezo michafu kama ilivyoeahi kutokea awamu ya tano wafanyabiashara walipoficha sukari
Ukome kabisa maana ulishangilia sana kifo cha Magufuli
 
Unaposema viwanda vipo mkoa huuhuu unamanisha mkoa gani?
 
Kuna shida mahali. Hapa ifakara mwezi sasa kuna uhaba mkubwa wa soda tena wa kampuni zote. Coca na pepsi. Siku zikija wauzaji wanatulazimisha kununua kila creat mbili ununue na novida moja.

Juzi na jana ndio sijaelewa kabisa. Maji nayo yamekuwa adimu japo hapa kuna viwanda viwili vinazalisha maji. Udzungwa na kiombero. Tulikuwa tunawategemea Afya drinking water nao haweleweki. Yaani shida tupu.
Sasa naona ni mwendo wa maji ya 1000 na yale madogo ya 300.

Kuna hujuma mahali.
 
Wazushi wanasema eti tatizo ni umeme... Kwani bia, Konyagi na K Vant viwanda vyake vinatumia mabetri?

Muda si mrefu utasikia Serengeti lite na Castle lite zimeadimika

Hapa kwenye castle lite wajitahidi bana
 
Back
Top Bottom