Soka la Tanzania limekua au soka la Afrika limeshuka?


Uwekezaji umeongezeka maradufu kwenye soka la TZ.

Wafadhili wakiingia mtini soka letu litarejea kule kule kwa zamani.
 
Hamasa ilikuwepo tangia zamani, ishu ilikuwa ni uchumi, kampuni kama ya Bakhressa na Azam Tv, ambao kwa kiasi kikubwa ndio wamechangia havikuwepo
Makampuni ya kamari kama Sportspesa na M bet, havikuwepo
Pia sera za TFF na serikali kubadilika na kuruhusu wachezaji wengi wa kigeni kusajiliwa tofauti na zamani,
 
Kuna kitu hutaki kuelewa sababu ya hisia zako dhidi ya watu fulani.

Kama umefuatilia kwa makini sasa kuna kundi la watu ambao walikuwa hawaendi viwanjani au hawafuatilii sana michezo lakini wanaenda viwanjani na kushabikia sana michezo. E.g. wanawake, watoto na wazee jinsia zote.

Hii inatokana na hamasa za hao unao kataa hawana mchango ktk ukuaji huu wa ubora wa soka letu.

NB: Nimetumia neno michezo sababu pia ngumi nao Wana Anza kupanda juu kama soka.

Media zina mchango mkubwa sana. Na media zinategemea watu kama wachambuzi, wasemaji, wahamasishaji, waongoza vipindi, waandaaji wa vipindi, n.k.

Wadhamini wanajitokeza wanapoona wanaweza kujitangaza kupitia wafuatiliaji wa hao watu kwenye media na viwanjani.
 
Uwekezaji umeongezeka maradufu kwenye soka la TZ.

Wafadhili wakiingia mtini soka letu litarejea kule kule kwa zamani.
Kuna wafadhiri na wadhamini, wafadhiri ni wachache sana ila wadhamini ni wengi na wanafaidika na udhamini wao so usitegemee kuwa wataondoka.
 
Nyie ndio mna hisia za mahaba na hao waropokaji kiasi cha kuwapaisha kuwa eti ndio wameinua mpira wa Tanzania....kama wanaweza kuinua mpira kwa hamasa kwa nini walishindwa kufanya hamasa kwa Taifa Stars? Timu kongwe ikifanya vizuri lazima itapendwa tu sababu ina base ya mashabiki tangu zamani
 
Ibaki hivyo Mkuu!
 
Na usemi wa umekutana na timu dhaifu utaishia hapo hapo
 
Yes mkuu,kwa muda mfupi huu tumesogea sana,hofu yangu uwekezaji endelevu?au boss akinuna bakuli linatembea
Mleta Mada kachambua vizuri. Hata hivyo naomba nimsahihishe kidogo. Timu ya Kwanza kutoka Tanzania kucheza Makundi ya CAF Champions League ni Yanga, ilifanya hivyo mwaka 1998. Nakubaliana na wewe kuhusu uwekezaji ambao si endelevu kwani tumekuwa tukitegemea mtu badala ya Timu kuendeshwa kama Taasisi. Ndio maana kuana wakati kwenye mitandao huwa kunachafuka ukisikia Mo anasema bora awekeze kwenye Benki. Suala jingine nakubaliana kuwa kuna mchango wa Azam TV na makampuni mengine ya Azam kwenye promotion na uwezeshaji kwenye Ligi yetu.
 
Unafikiri Taifa Stars imefuzu AFCON kwa makosa au bahati pekee?
Imefika pale kutokana na uzoefu au mafanikio yatokanayo na wachezaji toka klabu mbalimbali zinazofanya vizuri ambazo zimefaidika na hizo hamasa na kadhalika.
 
Unafikiri Taifa Stars imefuzu AFCON kwa makosa au bahati pekee?
Imefika pale kutokana na uzoefu au mafanikio yatokanayo na wachezaji toka klabu mbalimbali zinazofanya vizuri ambazo zimefaidika na hizo hamasa na kadhalika.
Point yangu haikuwa hiyo, pointi yangu kwenye mfano wa Taifa stars nilitoa nj kuwa, hamasa huwa haisadii kama hakuna uwekezaji kwenye quality ya wachezaji, management na ufundi kiujumla

Kwa kuwa kuna kipindi hao wahamasishaji walipewa kazi na serikali ya kuhamasisha stars lakini haikuzaa matunda, stars haikufanya vizuri na mashabiki hawakuwa wanaenda uwanjani kwa sababu stars haifanyi vizuri

So uhamasishaji wenye impact ya kweli ni ule unao improve quality ya team, hapo mashabiki wa soka lazima waende tu uwanjani

Nikutolee mfano wangu binafsi, nilikuwa sitazami sana mechi za Yanga kama kukiwepo mechi ya Simba au timu kubwa ya nje inacheza, lakini juzi ilibidi nitazame mechi ya Yanga kwa sababu ya quality, beauty, inayoonyeshwa uwanjani, sio kwa sababu wakina Ali Kamwe au Manara wameniambia bali kwa sababu ya quality niliyoiona kwenye mechi zao za awali
 
Nadhani shukrani zianzie Azam media ndo imeleta mabadiliko yote tunayoyaona zile kauli sisi ndo watu wa Mpira zimepungua tangu mpira huanze kuoneshwa hivyo kuleta ushindani unaosaidia ligi yetu iache janja janja ya kusajili magalasa toka nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…