Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 259
Hivi ushawahi kujiuliza ni kwa nini ukifika mwezi mtukufu wa Ramadhan ligi zote za soka Zanzibar zinasimama?
Ipo hivi; kila mwaka, kipindi cha mfungo wa Ramadhan, soka visiwani Unguja na Pemba halichezwi.
Wenyewe wanasema ipo hivyo kwa sababu ya kutoa fursa kwa wanaofunga kuitumia ibada vizuri.
Lakini ukweli wa hilo jambo haupo hivyo, leo nimepata kitu kipya ambacho nimejaribu kukiweka vizuri akilini, kimekaa.
Hebu jiulize, mbona hao wachezaji wanaotoka Zanzibar wanacheza soka Tanzania Bara hata muda wa mfungo na mambo yanaenda freshi tu. Kuna kitu wanaficha.
Leo katika kupiga stori na mchezaji mmoja anayecheza soka Zanzibar ameniambia ukweli wa hilo jambo.
Jamaa anadai kwamba soka la Zanzibar uchawi mwingi sana.
Mwenyewe anakiri kwamba Zanzibar kuna vipaji vingi kushinda Tanzania Bara, lakini soka lao linaharibiwa na uchawi.
Sasa hapo kwenye uchawi, kinapofika kipindi cha mfungo wa Ramadhan, kila mmoja anaogopa kujihusisha nao, ndiyo maana wakaamua bora ligi zisichezwe hadi kipindi hicho kipite.
Kama mnavyofahamu, mwezi wa Ramadhan mambo mengi ya ovyo huwekwa kando, licha ya kwamba hayatakiwi kufanyika kabisa, lakini watu wanauheshimu mwezi huo, ukipita, wanarudia madudu yao.
Kipindi cha Ramadhan walevi wanaacha pombe, wazinzi wanaacha zinaa, wachawi wanaacha uchawi, wakimaliza mwezi, kazi inaendelea.
Kwa kifupi, hicho ndicho nilichokipata leo.
Hebu jiulize, kwa staili hii soka la Zanzibar litaendelea kweli?