Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Soko jipya lililopo Mbagala Zakhiem limejengwa kwa gharama ya sh. 2Billion, ujenzi uliofanyika umeweka vifremu vidogo vidogo ambavyo havikidhi mahitaji ya wafanyabiashara.
Fremu nyingi wamegawiwa watu ambao hawakuwepo awali japo mkuu wa mkoa aliahidi wafanyabiashara wa mwanzo ndio watakaopewa nafasi za mwanzo lakini mambo yamekwenda kinyume. Awali mkuu wa mkoa aliahidi kusimamia ugawaji wa fremu ili haki itendeke kwa walengwa kupata nafasi lakini amebadili msimamo na hivi sasa kumezuka mgogoro ambao utahitaji kutatuliwa kwa busara.