Soko jipya la Mbagala Zakhiem halikidhi haja, limejengwa chini ya kiwango pia wafanyabiashara wa mwanzo wamenyimwa fremu.

Soko jipya la Mbagala Zakhiem halikidhi haja, limejengwa chini ya kiwango pia wafanyabiashara wa mwanzo wamenyimwa fremu.

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Soko jipya lililopo Mbagala Zakhiem limejengwa kwa gharama ya sh. 2Billion, ujenzi uliofanyika umeweka vifremu vidogo vidogo ambavyo havikidhi mahitaji ya wafanyabiashara.
Fremu nyingi wamegawiwa watu ambao hawakuwepo awali japo mkuu wa mkoa aliahidi wafanyabiashara wa mwanzo ndio watakaopewa nafasi za mwanzo lakini mambo yamekwenda kinyume. Awali mkuu wa mkoa aliahidi kusimamia ugawaji wa fremu ili haki itendeke kwa walengwa kupata nafasi lakini amebadili msimamo na hivi sasa kumezuka mgogoro ambao utahitaji kutatuliwa kwa busara.
 
Soko hili limevhukua muda mrefu sana kufanya uamuzi wa kulifungua na hata lilipofunguliwa mkuu wa mkoa hakufika hapo kwenye soko, alilifungua akiwa kwenye viwanja vya Zakhiem ambavyo viko mbali na soko! Alifikia huko akafungua huko na akaondokea huko huko, ni kama alilazimishwa kulifungua kwa alipokuja mwezi wa nane alikataa kulifungua na aliahidi makubwa ambayo wafanyabiashara walimsifu, leo kaigeuka ahadi yake.
 
Poleni sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...
 
Back
Top Bottom