Sokomoko la zawadi ya gari ya Rais mstaafu Mwinyi

Kutokana na yaliyo andikwa kwenye Kitabu chake Mzee Mwinhi, inaomekana katika Marais walio pata taabu sana ktk uongozi kuanzia alipo teuliwa kuwa waziri basi ni Huyu Mzee wetu Mwinyi.

Pamoja na kuwa mwadilifu na mtiifu lkn bado alichukiwa sana na alifanyiwa fitina za hali ya juu mpaka akajiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani lkn badae alirudishwa tena ulingoni lkn bado alipigwa fitina na kubabaishwa kuwa eti ni mdini anapendelea waislamu n.k, ama hakika walimyumbisha sana lkn kutokana na uadilifu wake na ucha Mungu alibakia kuwa Imara na Hatimaye Mungu alimsaidia.

Hakika kuna mafunzo mengi sana ya kujifunza ktk kipindi cha utawala wake.

tujirekebishe kwa wale wote wenye chuki binafsi na uchu wa vyeo, tuache tabia za kuivuruga nchi yetu, tuwe wazalendo wa kweli.

tuache kutafuta vyeo kwa uchawi au kwa kuhadaa/unafiki kwani cheo/uongozi hutoka kwa Mungu.

Tusibaguane wala kuchukiana au kufanyiana fitina kisa ni mkristo au mwislamu, sisi sote walio na dini na wasio na dini tunaunganishwa na MAMA Tanzania.

tusibaguane kwa makabila au ukanda kwani sisi sote ni watanzania, hivyo yatupasa kudumisha Amani, Upendo na Utulivu kwa masilahi ya nchi yetu.
 
Asante Nyani umehoji vizuri na umemakiza vizuri.
Kwa ufahamu wangu mdogo nijuavyo, rais hupewa gari kuwa lake binafsi pamoja na ulinzi unagharamiwa na serikali.
Ikiwa majaji wastaafu hupewa gari jipya kwasasa VXR, kwanini rais mstaafu asipewa gari bora zaidi?
Huyu ni raia lakini aliyetumikia nafasi ya juu zaidi ya uongozi, hivyo anastahili zaidi.
 

Kawawa na matatizo yake ya Afya mpaka anatangulia hakuwahi kupewa Benzi pamoja na ufupi wake, hii inaonyesha kitu kimoja tu nacho ni taifa kutokuwa na standards za namna ya kuwalea wastaafu wetu kitu ambacho kinachagizwa na katiba mbovu inayompa madaraka makubwa Rais ambayo yanamfanya kuamua vile anavyotaka na kupendezewa..TATIZO NI KATIBA MBOVU
 
Mie binafsi kuna baadhi ya wastaafu hawatakiwi kupata chochote hata pensheni wanatakiwa wasipate, hii inatokana na jinsi walivyotumikia taifa, yaani walikula kabisa heshima ni sahihi kuwapati ila kuwaongezea mali si sawa, nakumbuka kipindi kile Mrema anashika dhahabu airport, maelezo yake hadi leo hamna, labda yapo kwenye kitabu cha ruksa, na kama hayapo, basi kitabu akijatimia!
 
Naamini raisi ana fungu lake kila mwezi kwa ajili ya kufanya mambo ambayo JPM alikuwa anayafanya! Sio kwamba hela hazikuwa na maelezo!
 
Kikwete naye apewe au kwakuwa yeye ni wa bara!
Kikwete alizopiga bandarini na kwenye cheque za safari za nje zinamtosha wala haihitaji mgao wenu! Pia dili ambayo alimtoa kafara besti yake ile ilimpa hela ndefu sana pamoja na sign za mikataba ya ajabu ya kuuza rasilimali na wanyama! Jamaa anae hela ndefu wala hana haja na kabenzi ka million 100
 
Huyo Mzee hastahili lawama, kikwetu ni ukosefu wa adabu kukataa zawadi, hata angepewa muhogo angetakiwa kuupokea.
 
Kwa kodi zetu au pesa zake kama ni zake sio shida
 
Ni roho mbaya tu za umaskini wa baadhi ya wa Tz.Rais kasema mzee wetu now anapata tabu kupanda hilo li SUV apatiwe sedan matata ajabu watu wanachonga ngenga tu.Heko kwa mama samia.After all hayo magari inasemekana yako mengi na tulipewa kama zawad isipokuwa kuna mtu alifanya kama yake.
Kuna sehemu pia nilisikia tetesi kuwa number 1 mwenyewe eti ni biological daughter wa mstaafu😂😂
 
Hiyo subiri serikali ukatayo iunda wewe
Mkuu ila kwa sasa hiyo sahau

Ova
 
Kuna wazee wastaafu wengi tu wanapata shida kwenye usafiri wa umma mara mia ya anavyopata Mwinyi kupanda "vieite" lake.

Naishauri serikali iwape msamaha wa kodi wastaafu wote kwenye kuagiza gari at least moja.

Hii nchi ni yetu sote!
 
Huu ni ujinga mno kuhoji mtu aliyetumikia nchi kupewa kigari cha milioni kadhaa. Huyu mama angeweza kumpa kimya kimya kabisa. Umasikini ni mbaya.
 
Neno ''zawadi'' ndilo limeleta picha hasi ambayo imepelekea kuwapo na maswali mengi!

Kisiasa tunasema, amejipiga risasi mwenyewe mguuni(shoot herself in the foot)
 
Kuna wazee wastaafu wengi tu wanapata shida kwenye usafiri wa umma mara mia ya anavyopata Mwinyi kupanda "vieite" lake.

Naishauri serikali iwape msamaha wa kodi wastaafu wote kwenye kuagiza gari at least moja.

Hii nchi ni yetu sote!
Hakuna kitu kama hicho kinaweza kutokea
Lazima wawepo watu wenye shida,matatizo,wanyonge

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…