Soma hapa ujumbe mzito wa Rais Samia kwa Waislamu wote Nchini

Soma hapa ujumbe mzito wa Rais Samia kwa Waislamu wote Nchini

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Taifa letu linaendelea kuwa lenye baraka na Neema kwa sababu linaongozwa na kiongozi Mwenye hofu ya Mungu, kiongozi Mcha Mungu,kiongozi mnyenyekevu, kiongozi mwenye kuishi Maisha yenye kumpendeza Mungu, kiongozi mwenye mikono safi na matendo safi ,kinywa safi na matendo safi.

Tanzania ni tulivu ,yenye amani ,usalama ,umoja na mshikamano kwa sababu ya kuongozwa na kiongozi mwenye kuumizwa na kuguswa na shida za watu,kiongozi mwenye Moyo wa Huruma na upendo kwa watu wote. Huyu Ni daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.

Soma Pia: Mufti na Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir: Mwezi haujaonekana, mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza Jumapili March 02,2025

Katika ujumbe wake alioutoa usiku huu ametoa na kuzungumza maneno mazito sana na yenye kubeba hisia kali sana ya uzalendo na upendo kwa Taifa hili na watanzania kwa ujumla wake. Kwa hakika Mama analipenda sana Taifa hili na anawajali na kuwatanguliza mbele watanzania katika kuwaombea na kuwatakia mema.

Embu Soma hapa Mwenyewe alichokiandika Mama
Screenshot_20250301-221921_1.jpg
Screenshot_20250301-221932_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Hayo maneno mazito tusio na hizo habari za dini ni uzushi mtupu.

Anawezaje kusema anamuabudu huyo mungu asiyemuona huku binadamu anayemuona anaruhusu auwawe ?

Tangu September alipoagiza uchunguzi wa mauaji ya huyu mzee imebaki danadana hata alivyokwenda Tanga bila aibu mkoa alipozikwa huyo mzee familia bado ipo kwenye sintofahamu juu ya mauaji ya kikatili ya mzee wao.

Mwisho wa siku akaishia kusema kifo ni kifo tu.

IMG_20250213_134836.jpg
 
UNAFIKI.UTAMPENDAJE MUNGU AMBAYE HUMWONI?WAKATI WATANZANIA WENGI WANATEKWA NA KUUWAWA NA YUKO KIMYA?BAYA ZAID MATUKIO YOTE POLICE(SERIKALI) WANAHUSISHWA
 
Huu uchawa wa kumhusisha Mungu ni hatari sana Sheikh wangu. Mungu hapendi kulitumia jina lake kufanya unafiki.

Una uhakika tukikusimamisha mbele ya familia ya Mzee Kibao utaweza kuongea kuhusu Tanzania tulivu yenye amani?
 
Askofu bagonza adai watu wanatekwa na kupotea kama sindano nchini.

Muombee sindano zote zisitekwe.
 
Back
Top Bottom