Joshua Mbezi
JF-Expert Member
- Oct 18, 2024
- 1,994
- 4,446
Mimi na rafiki yangu mmoja tulienda sokoni wote na kila mmoja alikuwa na shughuli yake japo wote tuliambatana katika safari
Tulipofika sokoni tuliamua kila mmoja wetu amsindikize mwenzake sehemu anapoenda
Wakati tukiendelea na mizunguko yetu tulikutana na rafiki yetu mwingine anayeuza viatu
Rafiki yangu akawa amevutiwa na kiatu fulani akajaribisha na kikamtosha vizuri kabisa
Muuzaji kwakuwa tunajuana akamwambia rafiki yangu Kuwa anaweza kwenda nacho sehemu tunapoenda na iwapo atakipenda jioni wakati tunarudi atalipia
Mimi na mwenzangu tukaondoka ila wakati wa kurudi jamaa yangu akabadilisha maamuzi akasema kiatu kile sio kizuri hivyo hajakifurahia na kweli tuliyofikia akaghaili kukilipia kile kiatu tukaondoka
Baada ya wiki mimi nikarudi nikakikuta kile kiatu bado kipo nikaongea na muuzaji tukakubaliana na mimi nikalipia kile kiatu
Sasa siku moja nikiwa nimevaa kile kiatu jamaa yangu akakiona na kukikumbuka Kuwa ndo kile alichokikataa
Tangu siku hiyo jamaa yangu akanisusa na kusema nisijuane naye tena na akaanza kunisema vibaya kwa washkaji wengine
Je mimi hapo nina hatia?😌
NB
Soma kwa umakini kabla ya kujibu😎