Soma kwa makini: Dalili zinaonesha kuwa huenda mkataba wa bandari ukasababisha vifo vya watu

Wenzio hawamjui Mungu ndio maana kwa zaidi ya miaka 50, wao wanatafuna na kufanya anasa kupitia mabilioni ya bandari yetu. Huku mamilioni ya watanzania wanaoambiwa kuwa nchi yetu ina bandari wakishindia uji tu.
Mm sio muumini wa chama chochote ila kwa hili la DP wamwache mama alifanye tuu sababu hata kama ni wao wangefanya hivyo hivyo isipo kuwa kwenye swala la hisa hapo liwekwe wazi ili watanzania wote wanufaike hata wale ambao hawajawahi kutumia bandari kuagiza chochote nao wanufaike pia. Tumpe nafasi mama tufanye kama vile tunapo kuwa tumboni kwa mama tunakuwa hatuna uwezo wa kuchagua baba.
 
Mkuu kwa comment ya kichovu hivi usitegemee kutumiwa bando hata la mia 5, mana bado haujakidhi vigezo. Ongeza juhudi tu za kuponda, utakuta vocha yako tayari huko PM.
Mm hata hizo bando sihitaji ila wacha DP achukuwe aisee awabane panya buku wote na wengine wapate
 
Watanganyika wenzako wepi?
 
Pumbavu
 
Mkuu hakuna Kitu kama hicho. Mwekezaji Siku ZOTE anaangalia madhaifu ya Sheria.

Hawezi kuja Mwekezaji akaacha kushirikiana na watawala Wala rushwa na kuwaacha wananchi wakilia .

Loliondo Wamasai wamefukuzwa kwenye Ardhi Yao Kwa sababu ya Mwekezaji ámbaye YUPO Kwa zaidi ya miaka 30 Sasa na hakuna faida ya wazi wanayoipata watanzania zaidi ya wanyama kuhamishiwa Dubai na viongozi wanaotembelea kule kuhongwa Mapesa na hakuna anayejua nini kinatoka na kinaingiza shilingi ngapi?

Watakaa pale Bandarini watazima mitambo watalipisha makontena Milioni Moja watakusanya bilioni mia mbili watakaa na kuwapa watanzania rushwa ya bilion Kumi watawaambia andikeni kuwa makontena yaliyolipiwa ni laki mbili .
Watachota mabilioni ya pesa na kwenda zao Dubai.

Kama tumeshindwa kuwadhibiti watanzania Wenzetu waoga wasio na historia ya kumiliki Mali Kwa Hata miongo minne tutawezaje kuwadhibiti Wageni ?

Geita maelfu ya Tani za dhahabu na makontena ya mchanga WENYE Madini mengine yanatoroshwa kushirikiana na wawekezaji iweje kwenye pesa taslimu za iubadilisha tarakimu tu ishindikane pale Bandarini eti Kwa sababu ni Mwarabu. Waarabu na Wahindi Wana viwanda vingi sana Lakini wanaihujumu Hii nchi Kwa kiwango kikubwa sana.
Kuna Wahindi wameajiri Mpaka watu Wa IT kutoka nje kuingilia mifumo ya mapato Ili tu kukwepa Kodi.
Achaneni kabisa na nchi Hii inayoongozwa na Mafisadi Wa CCM wasiojali Kitu Zaidí ya kuteuana kufamilia.

Hiví unaamini Kabisa kuwa Rais ameshindwa kusafisha bandari.

Kuna ugumu Gani kuwafukuza wafanyakazi wote Wa bandari na kuajiri wapya bila kujali rangi ,Dini,kabila,Wala jinsia,?

Wanawaajiri watu wao na Sasa wanaona wameshaiba sana wanaona waepuke lawama.
Fukuza kuanzia walinzi mpaka Mkurugenzi . Kisha fuatilia Mali anazomiliki Kama haziendani na mishahara wake kamata Tupa Ndani?
Dubai na nchi za kiislama Zina Sheria Kali NDIO Maana wamefanikiwa. SIO eti wao Wana akili kuliko, hapan,wao Wana usimamizi mkali Wa Sheria na kuwakataa wanaohujumu mapato ya nchi.

MAGUFULI baada ya kuchaguliwa na kuapishwa mwaka 2015 aliendesa nchi akiwa na Katibu mkuu Kiongozi tu Kwa zaidi ya Mwezi Mzima. Nchi ikatembea Mbele Leo Kila Siku wanaongeza Wizara na manaibu waziri na makatibu eti ndio ufanisi. Kumbe ni kupeana ulaji . Nchi ya kupeana ulaji haiwezi kamwe kusimama uchumi zaidi ya uchumi Wa marafiki Wachache .
Hapa Suala SIO watu Suala Hapa ni MTU.
 
 
Mbona MAGUFULI hakufanya Hivyo.?

MAGUFULI aliikarabati na kuongeza Barabara na Treni ya kisasa na miundo mbinu Ili aongeze uwezo Wa Bandari kutoa mizigo Kwa haraka .
Zaidí akawa anawadhibiti wanaojaribu kukwepesha mizigo iingie BILA kulipia Kodi.
Sasa miundo mbinu Imekua mizuri Akina Fulani wamepitisha pesa zao Kwa mgongo Wa Nyuma wanaojifanya ni DPW Ili waje kuchota pesa pale bandari mana mazingira ni Bora Sasa kutoa mizigo.

Ni kichaa pekee au MTU aliyehongwa atakubali nchi yake iwekeze kiwango kile Kwa Kodi za wananchi na Tozo na kikokotoo halafu apewe Mgeni kwa mkataba tata.
 
Kwahiyo kitachowauwa hawa jamaa ni kwasababu wameshatumia mamilioni ya shilingi kutengeneza ushawishi wa kuunga unga, lkn raisi wa nchi haonekani kujali, kusikia wala kuelewa porojo zao.
Makundi hayo yakifa hakuna atakayesikitika juu ya misiba yao.
Aliye yalea kwa muda mrefu bila ya kuyashughulikia na yeye anatakiwa aungane nayo katika vifo; kwa sababu hayo unayodhani wewe kayafanya kuondoa hayo makundi nayo yanatuingiza katika matatizo makubwa zaidi, pengine kuzidi yaliyosababishwa na hayo yanayokufa sasa..

Kwa hiyo, katika orodha yako ya vifo, ongeza na hawa wahujumu wanaoweka rehani mali za waTanzania.
 
Hizo ni fikra za kijinga.

Sheria ni pande mbili.

Hakuna mkataba wa uendeshaji bandari mpaka sasa. Ipo nia.

Si mwandike mkataba mnaoutaka uwe vipi? Mbona bungeni huwa kuna bajeti ya Serikali na bajeti ya upinzani inavyoona hivi ndiyo ilitakiwa iwe.

Au mseme kama mna shemeji yetu mwengine zaidi ya Mwarabu wa Dubai ndiyo mnataka apewe ulaji?
 
Kuna watu walishaandikiwa kuwa mbuzi wa kafara. Hata useme nini hawatokusikia. Ongezea wewe hiyo orodha.

Sikio la kufa halisikii dawa.


Miaka ijayo tutakuwa na Rais AI, ataendesha nchi kw akukusanya maoni ya JF na Twitter, sasa hivi bado tuna Rais binadam.
 
Binafsi siafiki Suala la kumpa MTU yeyote rasilimali zetu Kwa sababu tulikwisha afukuza Wageni kwenye nyanja za kumiliki uchumi na rasilimali zetu.

Tatizo la nchi yetu linatatulika kirahisi sana. Hakuna MTU jeuri Mbele ya Kufukuzwa KAZI na kufilisiwa. Wizi na ubadhirifu unafanyika kimtandao unaojiimarisha Ndani ya chama bila kujali kuwa Kuna Sheria za nchi.

Kuna Mtu aliwahi kuingiza magari sabini Bandarini lakini yaliyolipiwa ni ishirini tu.
Hapo takwimu itaonyesha kuwa magari yakiyoingia ni ishirini. Watadanganya kuwa watu wamehama Bandari.
Ukifuatilia utagundua kuwa Mkurugenzi amewekwa kimchongo, meneja kimchongo, watu Wa IT kimchongo, wakusanya mapato kimchongo, walinzi kimchongo. Ni watu Wale wanaoitwa ni Mwenzetu.
Sehemu ZOTE zenye maslahi Wanaweka watu wao Kama namna ya kutafutiana ulaji. Sasa Hapo panahitaji mgeni au Kukamata watu. ?
Hapo mgeni anapewa Ili iweje?
Mgani atakuja uchaguzi ukifika wanakwenda kumuomba pesa za kampeni Ili Chama kushinde mana watamuoogopesha kuwa wakija wapinzani akafukuzwa. Hapo ujanja ujanja lazima uanze Kama kule Geita na gesi Mtwara na kwingineko ikiwemo mifuko ya wafanyakazi. Shiria ni Nyepesi wakati uhuru Wa kuchagua watu WENYE uwezo haupo. Kinachofanyika ni ujanja.

Hakuna Mwekezaji Duniani anayehangaika na watu wasiojitambua. Kule Kongo wanaoivuruga nchi ni Wawekezaji Wa kifaransa . Wamefadhili mpaka Majeshi ya UN Ili kulinda maslahi Yao ya kuiba rasilimali na kuingiza Bunduki.

Nimekua nikiona viongozi mbalimbali Wa nchi wanaposafiri Kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo WENGI wao wakifika wanaokwenda wanaulizia mahali watakapopata wanawake na pombe . Watu Kama Hao ukiwapeleka Dubai watakutana na wanawake Daraja la kwanza Wa kihabeshi na hawana muda Wa kusoma kilichopo kwenye mkataba.
KAZI Yao ni Kuomba omba pesa Kwa wawekezaji .
Bila kushughulika na Hawa wahuni Wa Ndani Hata akipewa Malaika kuja kuwekeza kwenye Serikali iliyojaa wahuni hakuna kitakachofanyika.

Mh. Rais asafishe pale Bandarini BILA kuonea MTU aibu Kisha aajiri watu waadilifu ikiwezekana aweke Hata Jeshi la wananchi kudhibiti mianya ya wizi.
Mwanajeshi akishahakikishiwa Cheo basi anafanya Kati Hata kufa .
Bandari ifungwe kamera Kila Kona na ZOTE zisimeke Ikulu.
Kufunga mfumo Wa mapato Kwa pamoja ni Mpaka apewe Mgeni mradi wote aumiliki .? Anaajiriwa mtaalamu Kwa mkataba akishakamilisha kuweka mfumo anaondoka ZAKE wanadhibiti watu WENYE NAFSI ya kukinai.


Nina Imani Hata wewe FaizaFoxy ni mwadilifu.
Wapo watanzania WENGI waadilifu. Tuachane na ushabiki Wa kushabikia Vyama na watu hasa kwenye uchumi.
 
Wewe una akili kubwa na ni mmoja wa watu wachache ambao hatujashikiwa akili na mtu.

Big up san mkuu.
 
Hapa mwamba unachanganya madesa, ujuwe wakati wa Magu taifa ilikuwa ni kama nyumba ambayo inababa mkali akisema kitu ukipinga basi utaishia kwenye sandarusi of which yalikuwa nimaamuzi mabaya pia ila hatuna proof japo tulisema yeye alibariki pia. Kwa hili hata tufanyaje haliwezi kubadilika na kama unabisha basi we jitowe kwa niaba yetu shika bango nenda ikuli pale getini kazibe njia ili ufikishe ujumbe tuone kama mama atakusikia. Utakuwa umefanya jambo la maana sana. Pengine nikuulize kati ya mwarabu na mjerumani ungependa yupi arudi?
 
Sawa.


Basi tuwekee na faida za kimkataba zilizoandikwa kwa maandishi kwenye huo mkataba wa Mwarabu
 
Wazalendo kama wewe tunaotumia akili zetu, badala ya matumbo yetu ni wachache san.
Mm nilisha sahau hata swala la ajira hapa nyumbani pamoja na elimu na uzoefu wangu wote bora nikawanufaishe majirani hapa nyumbani nafurahia chakula,midomo na watu wamkumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…