Hizo ni fikra za kijinga.
Sheria ni pande mbili.
Hakuna mkataba wa uendeshaji bandari mpaka sasa. Ipo nia.
Si mwandike mkataba mnaoutaka uwe vipi? Mbona bungeni huwa kuna bajeti ya Serikali na bajeti ya upinzani inavyoona hivi ndiyo ilitakiwa iwe.
Au mseme kama mna shemeji yetu mwengine zaidi ya Mwarabu wa Dubai ndiyo mnataka apewe ulaji?
Binafsi siafiki Suala la kumpa MTU yeyote rasilimali zetu Kwa sababu tulikwisha afukuza Wageni kwenye nyanja za kumiliki uchumi na rasilimali zetu.
Tatizo la nchi yetu linatatulika kirahisi sana. Hakuna MTU jeuri Mbele ya Kufukuzwa KAZI na kufilisiwa. Wizi na ubadhirifu unafanyika kimtandao unaojiimarisha Ndani ya chama bila kujali kuwa Kuna Sheria za nchi.
Kuna Mtu aliwahi kuingiza magari sabini Bandarini lakini yaliyolipiwa ni ishirini tu.
Hapo takwimu itaonyesha kuwa magari yakiyoingia ni ishirini. Watadanganya kuwa watu wamehama Bandari.
Ukifuatilia utagundua kuwa Mkurugenzi amewekwa kimchongo, meneja kimchongo, watu Wa IT kimchongo, wakusanya mapato kimchongo, walinzi kimchongo. Ni watu Wale wanaoitwa ni Mwenzetu.
Sehemu ZOTE zenye maslahi Wanaweka watu wao Kama namna ya kutafutiana ulaji. Sasa Hapo panahitaji mgeni au Kukamata watu. ?
Hapo mgeni anapewa Ili iweje?
Mgani atakuja uchaguzi ukifika wanakwenda kumuomba pesa za kampeni Ili Chama kushinde mana watamuoogopesha kuwa wakija wapinzani akafukuzwa. Hapo ujanja ujanja lazima uanze Kama kule Geita na gesi Mtwara na kwingineko ikiwemo mifuko ya wafanyakazi. Shiria ni Nyepesi wakati uhuru Wa kuchagua watu WENYE uwezo haupo. Kinachofanyika ni ujanja.
Hakuna Mwekezaji Duniani anayehangaika na watu wasiojitambua. Kule Kongo wanaoivuruga nchi ni Wawekezaji Wa kifaransa . Wamefadhili mpaka Majeshi ya UN Ili kulinda maslahi Yao ya kuiba rasilimali na kuingiza Bunduki.
Nimekua nikiona viongozi mbalimbali Wa nchi wanaposafiri Kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo WENGI wao wakifika wanaokwenda wanaulizia mahali watakapopata wanawake na pombe . Watu Kama Hao ukiwapeleka Dubai watakutana na wanawake Daraja la kwanza Wa kihabeshi na hawana muda Wa kusoma kilichopo kwenye mkataba.
KAZI Yao ni Kuomba omba pesa Kwa wawekezaji .
Bila kushughulika na Hawa wahuni Wa Ndani Hata akipewa Malaika kuja kuwekeza kwenye Serikali iliyojaa wahuni hakuna kitakachofanyika.
Mh. Rais asafishe pale Bandarini BILA kuonea MTU aibu Kisha aajiri watu waadilifu ikiwezekana aweke Hata Jeshi la wananchi kudhibiti mianya ya wizi.
Mwanajeshi akishahakikishiwa Cheo basi anafanya Kati Hata kufa .
Bandari ifungwe kamera Kila Kona na ZOTE zisimeke Ikulu.
Kufunga mfumo Wa mapato Kwa pamoja ni Mpaka apewe Mgeni mradi wote aumiliki .? Anaajiriwa mtaalamu Kwa mkataba akishakamilisha kuweka mfumo anaondoka ZAKE wanadhibiti watu WENYE NAFSI ya kukinai.
Nina Imani Hata wewe FaizaFoxy ni mwadilifu.
Wapo watanzania WENGI waadilifu. Tuachane na ushabiki Wa kushabikia Vyama na watu hasa kwenye uchumi.