Soma kwa makini: Dalili zinaonesha kuwa huenda mkataba wa bandari ukasababisha vifo vya watu

Eti mtu aamke akute amekufa !!!?
Mtu amezoea kwenda bandarini na kurudi na milioni 2 au 3 za bure kila siku, huku mshahara wake akiutumia kwa ajili ya ulevi na kuonga wanawake, afu leo uje umnyang'anye ulaji wake wa bure na umwambie aishi kwa kutumia mshahara wake wa mwisho wa mwezi lazima apate mshtuko wa moyo na kufilia mbali.
 
Ubarikiwe mkuu kwa kuwa na uelewa mkubwa katika swala hili, na kukataa ofa za vocha wanazogawa wazee wa bandari.
 
Serikali ya ajabu sana hii. Kama watu hawataki mkataba si wauvunje kwann wanatumia nguvu kubwa kuwalazimisha watu.
 
Hilo neno pengine unaelewa maana yake. Maana yake ni kitu ambacho mtu anakihisi, ila Hana uhakika kama kipo au kitakuwepo.
Sasa basi wewe hapo umewaza tu kwa upande mmoja wa hasara ila haujawaza kwa upande pia wa faida. I mean sawa sawa na jaji kutoa hukumu kabla ya anaemhukuku hajafunguliwa kesi.

Ulitakiwa pia uandike na upande wa faida kwamba hao DPW huenda wakaleta ufanisi mkubwa bandarini na kusababisha wale wateja wetu kutoka Congo, Uganda, Rwanda, Zambia nk waliokuwa wanapanga kuanza kutumia bandari za Lamu na Mombasa za Kenya pamoja na ile ya Angola wakabadili mawazo na kuendelea kutumia bandari kama kawaida.

Wakenya wanatambua fika kwamba hawa jamaa wakianza kazi kwa kuondoa wizi, uvivu na ucheleweshaji wa mizigo pale bandarini basi zile bandari zao zitageuka masoko ya kuuzia samaki tu. Ndomaana na wenyewe wanaomba Mungu hili swala lisipitishwe na serikali.
 
Mama ashasema kuwa yeye ni dereva mwenye leseni. Anaangalia mbele tu ili afikishe abiria wake Salama.
Kamwe haangalii nyuma wala pembeni akaja kumwaga abiria.
 
Kundi la tano la machawa wa DP world...HIMARS, GUSSIE, choiceVariable, Faizafoxy, covax!!!
 
Lisu; Wanaotetea mkataba wa DPR World ni Hawana Akili(HAMNAZO) au WAMEHONGWA.
 
Mm na familia yangu pamoja na ukoo wangu tunataka bandari yetu tu.
 
Ulitakiwa pia uandike na upande wa faida kwamba hao DPW huenda wakaleta ufanisi
"Wewe ni Dudumizi" na ninakufahamu sana na takataka zako nyigi humu JF, ikiwa ni pamoja na hii.

Unapoona mimi kutumia neno, "pengine" na kuhoji maana niliyolenga; halafu katika pumzi ile ile na wewe kwa kukosa akili, unatumia neno kama lile lile "huenda"!

DP World kwa kazi atakayofanya kuendana na yaliyobainishwa kwenye IGA hana faida yoyote kwa Tanzania. Sasa wewe mtu mwenye akili za mdudu unataka kulazimisha nione faida huko?

Jaribu kutumia akili yako vyema katika maswala haya. Hapa hakuna cha malumbano, tunapigania haki ya nchi yetu na sisi wenyewe.

Ninasisitiza tena, makundi yanayotakiwa vifo viyaandame ni pamoja na hili linalotuingiza kwenye mikataba mibovu.
 
Imewakata wajinga wakijazwa upepo harafu Wanapokula wamejificha Twitter basi Wacha wale chuma kama kule Ngorongoro..
 
Emeritus Prof.Shivji,Warioba,kadinali Pengo,Padre Kitime wapo group gani hapo?
 
Inasikitisha kuona wazazi wako wamekuzaa alafu wanaharakati uchwara ndio wanaopata faida ya kukutumia bure bila malipo.

Nakushauri uendelee kupambana hapa hapa JF huenda wale wazee wa bandari wataona juhudi zako na kukufikiria kama wanavyowafikiria chawa wengine. Siku zote chizi hujiona ni timamu, na watu timamu ndio humuona kuwa ni chizi. Kwahiyo sishangai kwa wewe mwenyewe kujiona wewe ni timamu, huku sisi tukikuona ni chizi. Ukitaka kujua kuwa unatumiwa na wanaharati uchwara angalia uwasilishaji wa ulichoandika ni ule ule wanaoutumia wanaharakati uchwara kwa kuwahadaa watu kwamba mkataba una mapungufu, lkn hawauweki hapa ili wenye akili tuyaone hayo mapungufu.

Ila siwalaumu hao wanaharakati uchwara maana wao wapo kazini kupigania matumbo yao na ya familia zao, huku wewe ukitumiwa kama daraja ili wakukanyage wapite na kuelekea kule wanapotaka kufika kwa faida zao na mafanikio yao.

Wanaharakati uchwara wamekuwa wakitumia ujinga wenu kwa manufaa yao. Mfano mwaka 2008 hadi 2014 walitumia ujinga wenu kuwahadaa kisiasa mkaambiwa Lowasa fisadi na nyinyi mkapanua midomo wao wakaukwaa ubunge na kutafuna mamilioni ya ruzuku bila kuwasaidia chochote. Mwaka 2015 baada ya kugundua kwamba nyinyi ni misukule yao ambayo hamna uwezo wa kuhoji lolote kutoka kwao wakawageukia na kusema Lowasa sio fisadi nyumbu mkaingia tena barabarani kumpigia deki bila kuhoji lolote, jamaa wakakwaa tena viti vya wabunge kibao huku nyumbu mkikosa hata hela ya kununua sindano.

Sasa wamekuja tena na gia ya bandari nyumbu mmeingizwa tena mkenge kwa kelele tu bila kuoneshwa mkataba wenyewe.

Wao washavuta chao kutoka kwa wazee wa bandari, huku wewe ukiendelea kufanywa tena daraja. Mimi sidanganywi kizembe na hiyo ofa yao ya vocha mtaipiganie nyie ambao mpo tayari kuuza utu wenu sababu ya njaa zenu.
 
Inasikitisha kuona wazazi wako wamekuzaa alafu wanaharakati uchwara ndio wanaopata faida ya kukutumia bure bila malipo.
Sihangaiki tena na takataka hizi, nishajieleza vya kutosha kwako, na ninajua umenielewa barabara.

Hayo uliyoandika huko chini sina muda wa kupoteza nayo.
 
Lisu gani yule aliesema Lowasa fisadi anastahili kuwa jela, au yule aliesema kuwa Lowasa sio fisadi alafu akampigia deki apite?
Lisu; Wanaotetea mkataba wa DPR World ni Hawana Akili(HAMNAZO) au WAMEHONGWA.
 
WAATHIRIKA NI WENGI SANA MPAKA WENGINE WAPO KWENYE TAASISI ZA DINI , AMBAO BANDARI ILIKUWA KAMA CHAKA LAO WAJIANDAE KUUMBUKA MCHANA KWEUPE.
 
WAATHIRIKA NI WENGI SANA MPAKA WENGINE WAPO KWENYE TAASISI ZA DINI , AMBAO BANDARI ILIKUWA KAMA CHAKA LAO WAJIANDAE KUUMBUKA MCHANA KWEUPE.
Yani mkuu si unaona wanavyotatarika utafikiri nyoka kamwagiwa petroli πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…