SOMA: Namna BIBLIA ilivyotabiri kipigo cha GAZA na Majirani zake, na namna GAZA ilivyokuwa ikisurubiwa toka enzi za manabii

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Mimi kama muhaya, nshomile kutoka Uhayani Republic, imenibidi niingie chimbo kuleta maelezo kamili juu ya hii vita ya Israel na palestina ambayo kuna watu wanadhani Gaza inapigwa kwa bahati mbaya. Ukisoma maandiko ya agano la Kale (Old Testament) katika biblia na vitabu vya kiyahudi Torah na Tanakh. Utagundua kuwa Gaza ilitakiwa kubondwa tangu enzi na enzi kwa mujibu wa maandiko. Vita vya Israel na Palestina, vinaanza tangu enzi za zama za Wafilisti na Wana wa Israel, na chanzo kikuu cha vita ya waisraeli na wafilisti kugombana ilikuwa ni kwa sababu ya Ardhi, Rasilimali, na Ngome, na vita hivyo havikuwa na chanzo maalumu bali kugombania Ardhi na rasilimali. Vita vya hawa jamaa vimeorodheshwa kama ifuatavyo;


1. Vita ya Israel na Wafilisti ikiongozwa na Eli na watoto wake.
Ukisoma 1 Samwel 4:1-3, utaona namna vita vilipigwa baina ya wafilisti na waisraeli.

English
Kiswahili
UFAFANUZI: Miaka hiyo Eli na wanawawe, waliingia vitani na wafilisti, vita vikapigwa kweli kweli. Waisraeli wakiongozwa na Eli na wanawawe wawili wakashindwa vita. Watoto wakiume wa Eli ambao walikuwa mashujaa wakauwawa na wafilisti, Sababu za kushindwa kwa Eli ni kutokuwa na Imani thabiti. Vita vikaendelea kwa miaka mingi, waisraeli wakiendelea kuchezea kichapo. Mpaka ufalme wa Sauli.

2. MFALME SAULI, MWANAE JONATHAN na WAFILISTI
Baada ya muda mrefu, utawala wa Mfalme Sauli ukaingia. Vita bado vikaendelea kupigwa balabala baina ya waisraeli na Wafilisti; katika kitabu cha 1 Samwel mlango wa 14-15 tunaona.

1 Samwel 14:47-52
UFAFANUZI: Sauli na mwanaye wa kiume Jonathan waliendelea kupigana vita dhidi ya wafilisti. Na wakawa wanashinda kwa sababu walikuwa wanamtumikia Mungu. Vita viliendelea mpaka badae akaibuka Goliath.

3. DAUDI, GOLIATH na WAFILISTI
Katika kitabu cha 1 Samwel 17:1-53 Daudi ambaye alikuwa mchungaji wa mifugo anaonekana kwenda vitani kuwasalimia kaka zake, ndipo akamuoka Goliath ambaye ni mfilisti akiwadhiaki ndugu zake katika uwanja huo wa vita.

UFAFANUZI: Vita iliisha kwa daudi kuwa mshindi, na badae baada ya kifo cha mfalme Sauli, kwa mujibu wa unabii wa Samwel ilitakiwa Daudi ndio arithi ufalme huo kutokana na watoto wa Sauli wote kuuwawa vitani na wafilisti. David anafanikiwa kuwa mfalme ya Yuda, na badae biblia inaeleza David alikuwa nguli wa Vita, katika enzi za ufalme wake alizikunguta falme za Wafilisti vibaya mno na kufanikiwa kuteka maeneo yote ya Israel na kuziunganisha tawala zote kuwa chini yake, na Yerusalemu ndio ukawa mji mkuu. Tokea hapo wafilisti wakawa wanakula kichapo tu. Baada ya kifo cha Mfalme Daudi, mwanawe Sulemani alimrithi kwenye kiti cha enzi. Sulemani akawa mfalme wa tatu wa Israeli na akatawala kwa muda mrefu. Anajulikana kwa hekima yake, utajiri, na kwa kujenga Hekalu la Kwanza huko Yerusalemu. Utawala wa Sulemani mara nyingi huonekana kama kipindi cha ufanisi mkubwa katika historia ya Israeli.

4. UNABII WA AMOS dhidi ya GAZA na NCHI JIRANI.

Angalia maandiko ya Biblia hapo chini namna Nabii Amos anavyoishutumu Gaza kwa udhalimu wake na kuitabiria kuwa Gaza na Jirani yeyote atakaye endelea na ujinga ujinga basi atapokea kichapo kikali.

Ukisoma kitabu cha Amosi 1:6-8 (Amos 1:6-8)

English



Kiswahili

UFAFANUZI: Amosi analaani mji wa Gaza kwa vitendo vyake vya zamani, hususani kwa kuteka jamii nzima na kuziuza kwa Edomu. Unabii huo unatabiri adhabu ya Mungu kwa namna ya adhabu ya moto (sijui ndio haya mabomu) juu ya kuta na ngome za jiji hilo kama adhabu matendo yao. Hii ni sehemu ya mfululizo wa unabii katika Amosi 1 unaozungumzia mataifa mbalimbali jirani, ukigusia udhalimu na vitendo vyao viovu na kadhia watakayokumbana nayo kutokana na mipango yao dhidi ya Israel. Ndio maana mwaka 1948 Israel ilizikunguta nchi zote za kiarabu zilizoungana kumshambulia hapa nazungumzia Misri, Lebanon, Syria, na zote zilizoshiriki katika vita hile ya mwaka 1948 inayoitwa Israel-Arab war. Unabii bado unaendelea.

5. MFALME HEZEKIA kuwatandika wafilisti na kuchukua eneo la GAZA

Vile vile ukisoma tena kitabu cha; 2 Wafalme 18:8 (2 Kings 18:8)
English

Kiswahili
7. Naye Bwana akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia.

8. Akawapiga Wafilisti mpaka Gaza na mipaka yake, tangu mnara wa walinzi hata mji wenye boma."

UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya simulizi la kihistoria la Mfalme Hezekia wa utawala wa Yuda na kampeni zake za kijeshi. Inataja kutekwa kwa eneo la Wafilisti, na eneo la mji wa Gaza, na Mfalme Hezekia. Muktadha mpana wa tukio hili ni kwamba Mfalme Hezekia wa Yuda alitafuta kuimarisha na kulinda ufalme wake. Gaza ulikuwa mji katika eneo la Wafilisti, ambao walikuwa adui wa muda mrefu wa Waisraeli na Wayuda. Kampeni ya kijeshi ya Mfalme Hezekia katika eneo hilo, ambayo ilijumuisha Gaza, inaweza kuwa sehemu ya juhudi pana za kulinda mipaka ya ufalme wake na kudhibiti udhibiti wa eneo hilo. Sababu maalum au vitendo vilivyosababisha kampeni hii hazijaelezewa kwa kina katika maandishi ya kibiblia.

6. SAMSON na GAZA
Vilevile tunaona kwenye kitabu cha waamuzi wafilisti wa mji wa Gaza wakipokea kichapo kutoka kwa Samson, baada ya kupata mwanamke katika mji huo.

Waamuzi 16:1-4 (Judges 16:1-4)

English

Kiswahili

UFAFANUZI: Mstari huu ni sehemu ya hadithi ya Samsoni, mmoja wa Waamuzi wa Israeli, na inasimulia ziara yake katika jiji la Gaza. Waamuzi 16, inatajwa kwamba Samsoni alienda Gaza, na huko akamwona kahaba. Akiwa Gaza, alijihusisha na matukio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kubeba milango ya jiji hadi juu ya kilima. Matendo yake huko Gaza ni sehemu ya simulizi kubwa zaidi la maisha ya Samsoni na kukutana kwake na Wafilisti, ambao walikuwa maadui wa Waisraeli wakati huo. Safari ya mwisho ya Samsoni lilifanyika huko Gaza. Alifia huko Gaza, karibu na mahali alipokuwa ametekwa na Wafilisti. Kifo cha Samsoni kinafafanuliwa katika Waamuzi 16:21-30, ambapo aliangusha hekalu la mungu wa Wafilisti Dagoni, akiwaua Wafilisti wengi, akiwemo na yeye mwenyewe, katika mchakato huo.

HITIMISHO: Mji wa kale wa Gaza ulikuwa katika eneo linalolingana na sehemu ya Gaza ya hivi leo. Kwa maelfu ya miaka, jiji na mazingira yake yamekumbwa na mabadiliko na maendeleo mengi, lakini marejeo ya kibiblia ya Gaza kwa ujumla yanarejelea mji wa kihistoria na eneo pana zaidi la mji huo mkongwe. Gaza ya leo iko katika eneo la linalosemekana ndio lililokuwa jiji la kale la Gaza, na miunganisho ya kihistoria na maandiko ya Biblia inasalia katika muktadha huo wa kijiografia kuwa Gaza ya leo ndio Gaza ya Kale.

Wafilisti wa nyakati za kale si sawa na Wapalestina wa leo. Neno "Wafilisti" linarejelea watu wa kale walioishi katika eneo la Kanaani, ambalo liko karibu na eneo la Israeli ya kisasa na maeneo ya Palestina, na vile vile sehemu za Gaza ya leo, maeneo haya waliishi wafilisti. Walitajwa katika Biblia ya Kiebrania na walijulikana kwa migogoro yao ya muda mrefu na Waisraeli wa kale.

Wapalestina wa kisasa ni wakazi wenye asilimia ya Kiarabu wanaoishi katika eneo hilo linalojumuisha Ukingo wa Magharibi (West Bank), Ukanda wa Gaza (Gaza strip), na sehemu za Israeli. Neno "Wapalestina" kimsingi linamaanisha wakazi wa Kiarabu wa maeneo haya. Ingawa majina yanafanana kwa kiasi fulani kutokana na eneo la kijiografia, mazingira ya kihistoria na kiutamaduni ya Wafilisti na Wapalestina wa kisasa ni tofauti. Wafilisti walikoma kuwepo kama watu wanaotambulika zamani, jamii yao ilipotea, wakati Wapalestina wa kisasa ni watu tofauti wenye historia na utambulisho wao wa kiarabu.
 
Hao waisrail ni shwayne tu, wangekua ni watu wamaana wasingemdhalilisha huyo Mungu, kwa kumning'iniza pale msalabani, tena na kichupi tu.

Ninacho jua mimi (na Dunia yote inajua) kua waisrail ni mashoga, kwani ndio wanao tetea huo upuuzi kwa vitendo.

Ni shoga tu ndio atakae shupaza shingo na kuwatetea.
 
Kumbe hako kaeneo la Gaza Damu imeanza kumwagika siku nyingi sana.

My Take,hiyo ni vita ya hao Jamaa na dini zao na Mungu wao.na tamaduni zao,ni utaahira Kwa mtu wa Tandahimba kukomaa na Israel na Wapalestina na kulazimisha dini na tamaduni zao ziwe za kwetu.
 
Inakuaje shoga anawachakaza wasio mashoga ninavyojua mashoga hua watu legelege

Sent from my PRA-LA1 using JamiiForums mobile app
 
Ofisa huo ulikuwa ni unabii, na Yesu hakuja kula bata Duniani bali alikuja kuhitimisha unabii juu ya ujio wake na kusurubiwa kwake;

Ukisoma Yohana 3:16 unaelezea namna Mungu alivyomtoa mwanae kipenzi dhidi ya wanadamu.

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

Na baada ya Yesu kuja Duniani alijua kazi gani iliyomleta na mwisho utakuwa hupi... Ukisoma Mathayo 16:21 anawaambia kuwa inatakiwa aende Yerusalemu akasurubiwe.

"Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka."

Na pia Yesu alisema maneno hayo katika Injili ya Mathayo, katika Mathayo 26:2

"Kama mjuavyo, Pasaka inafika baada ya siku mbili, Mwana wa Adamu atakabidhiwa ili asulubiwe."

Hapa, Yesu anatabiri kuhusu kifo chake cha msalabani, akitumia jina "Mwana wa Adamu" kujieleza mwenyewe. Kifo chake msalabani kilikuwa moja ya tukio muhimu katika maisha yake na kwa imani ya Kikristo.

Na huu ulikuwa ni mpango wa MUNGU. Na sio wa mwanadamu
 
Kwa hiyo Mungu huyo ana operate adhabu zake hapo Gaza tu?

Kwamba hao Gaza ndio wakosefu sana sana dunia nzima?

Biblia ni andiko moja la kipumbavu sana.
Sio GAZA, bali ni ardhi ya Israel imebarikiwa... ndio maana muisrael akiwa nyumbani ni anakuwa na nguvu sana...

Baraka juu ya Israeli zimetajwa katika sehemu kadhaa katika Biblia, hasa katika Agano la Kale. Kifungu kimoja kinachojulikana sana ambapo baraka za Mungu juu ya Israeli zinatamkwa kinapatikana katika kitabu cha Hesabu 6:24-26 (NIV):

"Bwana akubariki na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuelekeze uso wake, na kukupa amani."

Hii mara nyingi inajulikana kama "Baraka ya Haruni" au "Baraka ya Kuhani," na ni baraka muhimu na ya moyo juu ya watu wa Israeli. Ni kifungu kinachojulikana na kuthaminiwa sana katika mila za Kiyahudi na Kikristo.

Pia kuna vifungu vingine vingi katika Biblia vinavyozungumzia baraka, ulinzi, na ahadi za Mungu kwa watu wa Israeli, zikiwemo zile zinazopatikana katika Zaburi, Manabii, na katika Agano lote la Kale.
 
Inastaajabisha kuona muisrael wa buza na mpalestina wa Tandahimba nao wanaandamana, wakati vita haiwahusu
 
Katika uzi wako umesahau kuwaongeza na waarabu wanawabaka sana shangazi zako wanaokwenda kufanya kazi za ndani huko pande za uarabuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…