SOMA: Namna BIBLIA ilivyotabiri kipigo cha GAZA na Majirani zake, na namna GAZA ilivyokuwa ikisurubiwa toka enzi za manabii

huyo jamaa amemsikia netanyahu akitoa historia ya mzozo wao tangu zama na zama? Huyo jamaa anaijua historia ya gaza na ashdodi katika mapigano? Watu wengine ni wabishi kwa kuwa hawasomi mambo muhimu hata ya dini zao wanabishana na uhalisia wa mambo ya kweli
 
Mimi sijakataa... Bali nimesema kwa jamii ya sasa uwezi kusema moja kwa moja kuwa hao ndio wafilisti, japo maeneo, utamaduni na baadhi ya vitu vinafanana...
 
Mmeambiwa Mungu, Miislam haikuba hilo kabisa la yesu kuwa ni Mungu, wewe ulisikia kuna Mungu anaitwa Issa?
Yesu sio MUNGU, yesu ni mwana wa MUNGU... wewe uelewi nini hapo. Yupo MUNGU mkuu
 
Huyo Mungu wa wayahudi aliyeua kila mzaliwa wa kwanza huko Misri ndo huyu anayehalalisha mauaji ya wapalestina? Mleta uzi bora ungekaa kimya kuliko kutetea upumbavu
 
Vita hii vitaisha baada ya Armageddon War au nyie mnaita "Al-Malhama Al-Kubra... Ambapo atatokea Masiah wa uongo, mpinga kristo nyie mnamuita Dejjal.

Hivi vitu ni unabii, ila wengi tunaona ni ngonjera tu.
 
Hawa watu wanashangaza kweli kweli
 
Una mawazo na fikra za hovyo sana.

Biblia ime kupumbaza haswa
 
Yesu sio MUNGU, yesu ni mwana wa MUNGU... wewe uelewi nini hapo. Yupo MUNGU mkuu
Kumbe, au mmetofautiana madhehebu? Kuna wakristo wanamini Yesu ni mungu?

Wewe huwmini kuwa yesu ni mungu, hunw tofwuti na Waislqk hapo.

Wewe unaamini huyo mwana wa mungu ni myahudi, au siyo?
 
Wataalamu wa mambo wanakwambia ni heri uamini yupo alafu husimkute, hiyo haitakuwa kesi kwa sababu umeamini alafu ukumkuta.
Hao wataalamu ni kina nani?

Wataalamu hao walifahamu vipi Mungu huyo yupo?

Wataalamu hao wana uthibitisho upi wa uwepo wa Mungu?
Kesi ni hiyo Usiamini alafu umkute kwa sababu tu umekataa kuamini, utaelewa cha mtema kuni
Mungu kama anataka aaminike, Alishindwaje kuumba Binadamu wema watakao mwamini na kumtii siku zote?

Mungu huyo kwa nini ajifiche huko halafu anataka aabudiwe na kuaminiwa?
 
Huyo Mungu wa wayahudi aliyeua kila mzaliwa wa kwanza huko Misri ndo huyu anayehalalisha mauaji ya wapalestina? Mleta uzi bora ungekaa kimya kuliko kutetea upumbavu
Mungu gani aliyeua wazaliwa wa kwanza wa misri? Yani ulivyokuwa Lodi Lofa unaandika hata kitu ambacho ukijui... Yani nimekuandika kuwa Israeli imebarikiwa na kupendwa na Mungu kuliko mataifa yote bado uelewi.

Ngoja nikupe shule sasa.

Kwanza Misri chini ya Pharaoh walikuwa hawamwabudu MUNGU walikuwa na miungu yao na uchawi wao. Waisraeli walikaa muda mrefu utumwani, na Mungu alisikia kilio chao cha muda mrefu, akamtuma Musa kwenda kumwambia Pharaoh awaachie Waisrael, ila pharaoh akakataa, akafanya kila njia lakini Pharaoh bado akawa kichwa ngumu, ndipo MUNGU akapiga pigo la kuwachukua wazaliwa wa kwanza hili kumuonesha nani ni mkuu zaidi. Ndipo Pharaoh kupigwa hilo tukio akawaachia waisraeli.

Fahamu fika huo uhai wako ni mali ya MUNGU, kuuchukua sio shida kwake. Hivyo kuwachukua wazaliwa wa kwanza ni kama kuchukua mali yake tu.

Hakuna anayehalalisha vita, kabla ya kuropoka elewa neno unabii au prophecy... Vitu vilikuwako na vitaendelea kutokea....ungesoma maandiko ungeacha maswali ya kijinga
 
Kwa hiyo wewe inaamini mungu yupo lakini unataka asijifiche?
 
Wewe unaamini huyo mwana wa mungu ni myahudi, au siyo?
YESU alizaliwa katika ya jamii ya wayahudi, automatically ni myahudi.... Swali gani hilo unauliza au unataka niseme YESU ni muarabu... YESU alikuja Duniani kupitia mwanamke aliyekuwa myahudi na alikuja kukamilisha Torati, ambayo ilikuwa chini ya wayahudi, na yeye kakua kwenye mikono ya wayahudi... na ilibidi aje katika mwili wa binadamu ili iwe rahisi kuketi miongoni mwa wanadamu, na unabii kutimia
 
Mungu huyo kwa nini ajifiche huko halafu anataka aabudiwe na kuaminiwa?
Hawezi kuwepo kwa sababu hataki mti amri zake kinafiki... Akiwepo utatii amri sio kwa sababu unataka, la hasha bali ni kwa sababu ya hofu kwamba anakuona na wewe unamuona... ili ajue watu wake wa kweli ni wapi, basi ni lazima ajitenge nao
 
Mungu kama anataka aaminike, Alishindwaje kuumba Binadamu wema watakao mwamini na kumtii siku zote?
Alikuwa na nia njema tangu mwanzo, ndio maana akawaumba Adam na Hawa ambao walikuwa hawajui dhambi yoyote, ila shetani akatumia nguvu yake ya ushawishi walaghai wale tunda la ujuzi wa mema na mabaya. Hapo ndipo dhambi zikaanza na dhambi ya kwanza ni Kaini kumuua Abel kisa wivu.... Hapo mlaumu shetani kwa nguvu yake ya ulaghai
 
Wataalamu hao walifahamu vipi Mungu huyo yupo?

Wataalamu hao wana uthibitisho upi wa uwepo wa Mungu?
MUNGU alijidhihirisha kupitia mitume na manabii ambapo aliwapa maagizo na kutenda miujiza kudhihirisha ukuu wake. Mfano Lutu pale Sodoma na Gomorrah, Nuhu na mafuriko, Musa na kutawanyisha bahari, na Yona kumezwa na samaki na mambo kadha wa kadha
 
Kwa hiyo wewe inaamini mungu yupo lakini unataka asijifiche?
Mimi si amini kwenye ku amini.

Sina imani.

Najua Mungu hayupo.

Ninyi hamjui kama Mungu yupo, ila mna imani tu, Ya kwamba Mungu yupo.
 
Hawezi kuwepo kwa sababu hataki mti amri zake kinafiki... Akiwepo utatii amri sio kwa sababu unataka, la hasha bali ni kwa sababu ya hofu kwamba anakuona na wewe unamuona...

ili ajue watu wake wa kweli ni wapi, basi ni lazima ajitenge nao
Ina maana Mungu mnayedai ni mjuzi wa vyote, Hajui watu wake wa kweli ni wapi?

Kwamba hadi ajitenge ndio awajue?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…