Ndondocha mkuu sikia, pole sana ila:-
1. Usijaribu kukatia tamaa usafiri wako. Kusanya details muhimu za huyo boda, kama vile namba yake ya simu aliyokuwa akitumia, taarifa za watu wake wachache ambao ulikuwa ukiwafahamu au kuwaona naye, kama kuna makubaliano yoyote ambayo mliandikishana hakikisha unatunza vizuri kabisa, meseji yoyote ya miamala au za kawaida za mara ya mwisho kuwasiliana naye hifadhi mkuu.
2. Piga hesabu kwa miezi yote ambayo alikuwa na usafiri wako mpka kufikia siku ya mwisho ambayo alitoweka ni kiasi gani jumla ambacho angetakiwa kurejesha, pia muda ambao umemtafuta na gharama zote ulizoingia ziongeze kwenye hiyo 1.8M.
3. Usiwategemee sana polisi, japo umefanya vema kutoa taarifa polisi ila hii kitu ifikirie wewe vizuri kabisa namna unavyoweza mkamata na hatakama ikija mbinu ambayo kwa wakati huu huna uwezo nao kuutekeleza iandike sehemu. Tengeneza list ya mbinu zote ambazo utaona zitakufaa kumpata. Kama ni muhamiaji, fuatilia wapi alipotokea in short kuwa na details kamili.
3. Baada kukusanya taarifa na kuandaa hizo mbinu zote, now relax na uendelee na maisha yako kama kawaida, yaani awepo kwenye target ila mfanyie kazi taratibu na uwe na nia ya dhati kabisa kumpata.
4. Piga mishe zako ila endelea kumsaka. Ipo siku utakutana naye na utapata pesa zako zote kiulaini.
5. Katika maisha ups and down hazikwepeki ila hizi zinazosababishwa na mwanadamu mwenzio huwa naona ni makusudi na siyo za kukaa na kulalamika sana we mtafute mtu wako akupe chako. Ila zile ups and downs ambazo zinatokea kwasababu ya natural calamities hizo ni kumuomba Mungu akuepushe nazo maisha yaendelee.
Hii mbinu nimeitumia na naendelea kuitumia na yeyote anayejaribu nidhulumu haki yangu huwa zinarudi na faida juu.
Mwaka 2019 nililima na jamaa shamba heka mbili maharage jamaa kwakuwa yeye ndiyo alikuwa anafanya kila kitu akaamua baada ya mavuno auze kila kitu kisha anipige chini. Na alifanya hivyo, aliuza kisha akaniblock namba zote na sikujua wapi alipo. Nilitumia mbinu hizo hapo juu ukiongeza na knowledge ya ki-intelijensia niliyonayo hatimae nilifanikiwa kumpata na hakutegemea.
Kama kawaida nilipiga hesabu zangu zote na alilipa mwaka huu January tena miamala alikuwa anafanya mwenyewe kwa simu yake.
Chako ni chako ukiamua kukipotezea kinapotea kweli ila ukitambua mateso na shida ulizopitia wakati wa kuzitafuta huwezi acha chako kipotee kiurahisi hivyo.
Mkuu pambania mali yako hii dunia ndogo sana ukipania kumtafuta mtu. Mwanadamu kuna namna ya kuishi naye, usimuamini mtu hata mmoja.
Kila la kheri boss.