Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Soma unaweza jifunza kitu: Jinsi graduate nilivyopoteza 1.8M niliyoitafuta kwa jasho

Wapo mkuu lakin upractive in a large scale.....yes hao wengjne ndo wanatajarika haswa...masuala ya kusema ulime 5 acres bora hela uiache bank..unahangaika wee.jnakuja pata faida 400k!arghhh
Ukitaka kupata hela kwenye kilimo, uwe mfanyabiashara au dalali. Kuwa mkulima maana yake unawatengezea watu hela kupitia wewe.
 
Kwenye harakati za utafutaji kupoteza ni sehemu ya maisha.

Jambo la msingi ni kupambana kupunguza risk za kupoteza.

Mimi nilifanya kazi za usiku, nikakusanya zaidi ya 1M nikaenda kulima mihogo huku Kibiti. Haikurudi hata 100.

So, ni kawaida tu.
Hata nashamba pwani kusafisha tu pori milioni ikapotea mda wa kupanda nimemaliza mvua ikakatia njiani hata kumi sikupata,hadi leo ni shamba pori nimeuza haliuziki atakale hata bure tampa ni heka 10.
Tunasaka pesa kwa mateso Sana lkn hazina huruma zipoteapo
 
Asante mkuu ,sitokata tamaa
Maisha ni harakati hata ukiacha kupambana utalazimishwa na nature kupambana.
Nimepoteza pesa nilichoambulia ni experience tu yaani kununua uzoefu wa maisha ya kupambana kwa milioni 200.Nabaki nayakumbuka tu maneno ya mzee wangu mwanangu jenga majumba ya kupanga tu hata kama za simpo simple utokosa wapangaji utolala njaa achana na mabiashara,leo ndo nayakumbuka huku pesa zimekata.
 
Tunatofautiana kiwango cha maumivu ndo utafutaji ulivyo hakuna apendae kupoteza pesa basi utokea tu.Mimi nimepoteza jumla ya milioni 200 kwa mda wa miaka 15 kwa aina 16 za biashara na bado sijafanikiwa sijatoka kimaisha lakini sijakata tamaa napambana.Huwa najuta heri ningefungulia zipu hizo pesa kuliko kujinyima Ili nitoke kwa ndoto za kuwa tajiri lakin ndo hivyo imegoma na age ndo inasonga.Biashara ni SAwa na ndoa ni Hadi uingie ndo utaona changamoto zake.
Nimefanya biashara ya daladala,ya roli,kupasua mbao,kuchimba madini, kununua viazi mbeya,kilimo,nk lkn kote haikuwa bahati yangu.
So usikate tamaa.
Aisee pole sana
 
Kwenye harakati za utafutaji kupoteza ni sehemu ya maisha.

Jambo la msingi ni kupambana kupunguza risk za kupoteza.

Mimi nilifanya kazi za usiku, nikakusanya zaidi ya 1M nikaenda kulima mihogo huku Kibiti. Haikurudi hata 100.

So, ni kawaida tu.
Mkuu ungefafanua kidogo hilo la mihogo kukupa hasara, ninavyojua mihogo ni zao linalolimika kwa wepesi kuliko mazao mengine, ila usioteshe tu kipindi cha kiangazi.
 
Nikirudi home madogo wanapenda sana kuniambia broo nunua pikipiki tukuletee hela. Nawaambia madogo mm sina kitu naunga unga maisha tu. Story zikinoga wanaanza kusimulia jinsi wanavyowaibia mabosi pikipiki wanazopewa mkataba. Ndio nikajisemea bora nifungue goli niuze matunda tu. Kiufupi usimpe kazi mtu ambaye sio mkeo, mwanao au mumeo
Hii sanaa tunatakiwa kujifunza. Ni ngumu lakini ni lazima uone jinsi ya kuweza kufanya. Unatakiwa ujifunze kuajiri watu wasio ndugu zako kwenye mishe zako. Wazungu wanasema OPT yaani other people time unatakiwa uweze ku laverage hii. This is an art worth to be known.
 
Mkuu Acha aibu hii.. wacha kulilia 1.8M, anyways mara kibao huwa nakumbusha tu.. Boda sio Biashara ya kuwekeza.
Nna jamaa angu anafanya hii shughuli mwaka wa nne huu na ziko tano mpaka sasa. Kila kitu ni namna unavyokisimamia.
 
Ukipoteza milioni au milioni 10 kwenye biashara na unalia mtaa mzima.Kumbuka wapo waliopoteza zaidi ya milioni 200 ktk utafutaji na wapo happy tu wakiamini ipo siku zitarudi zote
 
Wapendwa wanajf habari za usiku,

Leo akili imetulia nimeona nitoe simulizi fupi ya jinsi nilivyoweza kupoteza tsh 1.8M.

Mara baada ya kugraduate pale SUA na (BSC GM) na kushindwa kupata tempo nilijichanga katika kazi mbalimbali kama nyuzi zangu baadhi za nyuma zilivyoelezea mishemishe zangu ikiwemo shughuli za mchanga, tofali na tuition centre.

Kwa mwaka 2020 nilifanikiwa kukusanya kiasi cha shil milion 2 na laki 4 na niliamua hii pesa isikae benk tu kwavile bado naendelea kufight na mambo mengine basi niliamua kufanya biashara ya bodaboda.

Nilinunua bodaboda iliyokaribia kuisha kwa mkataba kwa tsh. 1.8M na kumkabidh mtu aendeshe kwa makubaliano tuliyoafikiana. Nilikuwa namfahamu lakini nilikua simjui sana kiundani na ndugu zake sana nilikuwa siwafahamu sana.

Nadiriki kusema nimeweza kupewa mrejesho wa siku 10 pekee na muda huu navyoongea zimepita takribani wiki 3 sijaweza kuonana wala kuwasiliana na dereva wangu, polisi nimeripoti kwa kufata taratibu lakini sioni matumaini ya kupata chombo changu, sijui mwenzangu ni mzima au ameaga dunia, nimejarbu kufatilia watu wake imeonyesha ni mhamiaji katika maeneo ya mkoa niliopo.

Nawaza sana, nimeweza kupoteza pesa niliyoitafuta kwa jasho sana ndani ya mwaka mmoja, nikiri sikuweza kulala kwa siku 2 mfululizo, Nimeamini hii dunia haina huruma.

Kuna muda nawaza ile hela bora ningeweka tu, kuna muda nawaza sana nikiona mtu anaongelea pesa tu nawaza zile pesa zangu, nimebaki na kiasi cha laki 5 kwenye akaunti yangu nawaza lini nitafika tena kwenye milioni mbili na laki 4.

Kuna muda huwa nawaza sana nikifikiria njia ngumu nilizoweza kupata hii pesa na njia rahisi ilivyoweza kupotea hii pesa, kuna muda niliona haya maisha hayana maana na kupitia huu mkasa i was so harsh, niliweza hadi kuseparate na mtu wangu, Ok ni hayo tu nimeona nishare nanyi wakubwa.

Muwe na usiku mwema.
Siku nyingine mwanangu ukipata fedha usiwekeze kwenye vyombo tegemezi kama vyombo vya moto vya usafirishaji. Hebu fikiria una chombo chako trafiki anakigeuza chake kwa kukupiga mabao ukiachia mbali dereve kukuibia hata kwenye kukiktumia vibaya hata kuchomoa vifaa. Heri hiyo fedha ungelimia hata bamia ungerejesha fedha yako bila presha. Jifunzeni kuwa watukutu kidogo. Haya mabiashara ya kuigiziana wakati mwingine yana maumivu mwanangu. Kama imeshindikana si angalau ungeendesha lau mwenyewe ili ujue kiasi kinachoingia na challenge za biashara yenyewe kuliko kumwamini mjuba usiye hata mjua.
 
Asante mkuu
 
Mkuu ungefafanua kidogo hilo la mihogo kukupa hasara, ninavyojua mihogo ni zao linalolimika kwa wepesi kuliko mazao mengine, ila usioteshe tu kipindi cha kiangazi.
Kiangazi kilichangia, maana mihogo iliota hapa na pale sana.
 
Back
Top Bottom