Somalia kuwa mwanachama wa Afrika Mashariki

Somalia kuwa mwanachama wa Afrika Mashariki

Messenger RNA

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
1,411
Reaction score
3,712
Somalia iliwasilisha ombi la kuwa mwanachama wa Afrika Mashariki katika kikao cha wakuu wa nchi walipokaa kumuidhinisha Congo D.R kuwa mwanachama kamili wa Jumuiya hiyo.

Stay tuned.
 
Migogoro ipo Burundi, DrC na Rwanda, Rwand na Uganda...

Mgogoro huu hautakuwa wa kwanza na wamwisho, pia kuna migogoro Sudan Kusini lakini kapewa uanachama...

Kwann Somalia wasipewe?

Migogoro ya Burundi na Rwanda siyo ya kidini.
Ila migogoro ya Somalia ni migogoro ya kidini.
Na ukumbuke dini yao wanataka kila mtu afuate sheria zake.
Sikatai Somalia kujiunga EAC ila nimetoa mawazo tu kulingana na komenti yako.
 
Maswala ya dini ni maswala yao ya ndani...

China kafungua ubalozi Somalia pamoja na mambo yao ya kidini lakini mchina huyo huko China ana deal na waislamu mpaka wanaomba pooo...

Rwanda wamekataza adhana lakini sijui kama wamekataza kengere makanisani (ni maswala yao ya ndani)

Hutakiwi kuingilia maswala ya ndani ya nchi, kuna taratibu zake kufanya hivyo...

Heshimu uhuru wa taifa husika na watu wake... kuingilia uhuru wa watu ambao sio wako ni kukiuka maswala ya kidiplomasia na mashirikiano baina ya nchi

Pia kujiunga kuna kupa fursa kushiriki na kusaidia kutatua hizo changamoto

Zenji wana udini mwingi na wana makatazo mengi hasa kipindi cha mfungo, je hawa nao tuwa fanyaje? Wana ajira zao na ardhi yao je tuwa fanyaje?
 
Hkn wakatengeneze jumuiya yao
Dada punguza makasiliko... na aliye pendekeza kujumuishwa kwa Somalia ktk Jumuiya ni Kenya ambayo yeye yupo krb nao zaidi na migogoro anayo yeye kwa ukaribu

Kwann sisi watanzania tuogope... Uganda nae akapendekeza.... na ndio maana walialikwa ktk kikao cha kumkaribisha DRC

Sisi waoga, subirini mambo ya kuondoa mipaka na ajira za pamoja... mchangamke vizuri wakenya wame kuja kununua na kufanya ufugaji wa kuku na maguruwe pamoja na mashamba ya miti na maparachichi

Nyie pigeni kelele tu ambazo hazina mashiko
 
L
Migogoro ipo Burundi, DrC na Rwanda, Rwand na Uganda...

Mgogoro huu hautakuwa wa kwanza na wamwisho, pia kuna migogoro Sudan Kusini lakini kapewa uanachama...

Kwann Somalia wasipewe?
Level ya migogoro hizo nchi ulizotaja zinaendeka kwa urahisi hata kibiashara
 
Back
Top Bottom