Somalia wapiga marufuku Sambusa

Somalia wapiga marufuku Sambusa

BADO NI DEFN YA ANAYEAMINI UPUUZI UNAOUAMINI

Acha ujanja janja wa kuhamisha hoja yangu.

Jibu swali nililokuuliza.


Soko la watumwa la zanzibar (stone town slave market) lilijengwa na kuendeshwa na nani?



Biashara Ya Watumwa Ya Afrika Ya Mashariki​


Kama ilivyokuwa Afrika ya Magharibi, biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki ilikuwa mashuhuri na ilianzishwa kikamilifu na kutokana na maendeleo na jitihada za nchi za Kikristo za Ulaya. Bwana E. A. Alpers anaandika kwenye “African Slave-Trade (Biashara ya Utumwa ya Afrika):

Ushahidi zaidi kwamba biashara ya watumwa kwa vyovyote vile ilikuwa mashuhuri katika Afrika ya Mashariki kabla ya karne ya kumi na nane, imeletwa na Wareno.

Hakika Wareno, wakiwa ndiyo waasisi (waanzilishi) wa Atlantic Slave-Trade, wangejaribu kuendeleza biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki kama wangeikuta tayari ipo na imekwisha shamiri. Lakini maandiko ya mwanzo ya Wareno yanataja tu biashara ya watumwa kwa kupitia tu.

Lililokuwa muhimu zaidi ni wale wafanyabiashara za dhahabu na pembe za ndovu walizipeleka Arabuni na India.

Wavamizi wa Kireno walielekeza juhudi zao kwenye bidhaa hizo wakati wa karne ya kumi na sita na kumi na saba, sio tu kwenye pwani ya Kenya na Tanzania, bali pia katika Msumbiji na Zimbabwe.

Hata nta na ambari zinaonyesha zilikuwa bidhaa muhimu zaidi kuzidi watumwa wakati mrefu sana wa kipindi hiki. Kwani tofauti na wakoloni katika nchi ya Amerika, Wareno kamwe hawakuanzisha uchumi wowote wa kilimo huko India.

Biashara ya watumwa ya Wareno kutoka Msumbiji kwenda India kwa nadra sana ili- fika idadi ya watu elfu moja katika kipindi cha mwaka mmoja wowote ule, na kwa kawaida ilikuwa chini ya nusu ya idadi hiyo.

Huko Brazil ilikuwa haramu kufanya biashara ya watumwa hadi mwaka 1645, na kamwe haikulitiliwa maanani hadi mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa. Hadi mwaka wa 1753, wakati misingi ya biashara mpya ya watumwa ilikuwa inawekwa Afrika ya Mashariki, palikuwepo na jumla ya watumwa 4399 tu wa Kiafrika katika India yote ya Wareno.

“Misingi hii ni ipi? Licha ya mahusiano ya muda mrefu baina ya Waarabu na Afrika ya Mashariki, biashara ya watumwa haikutiliwa matumaini na Wafaransa.

Kwa mujibu wa tarakimu rasimi, zaidi ya watumwa 1,000 walikuwa wanasafirishwa kila mwaka.

Wafaransa, wakifanya magendo kwa ajili ya kukwepa kodi ambazo zilitozwa Msumbiji, labda waliongeza idadi na kufika angalau 1,500.

Inawezekana ni idadi ile ile ilichukuliwa kutoka Ibo wakati wa muongo huu. Kwa hiyo Wareno kule Msumbiji na Ibo (na baadaye Quelimane, karibu na mdomo wa mto Zambezi unapoingilia baharini) walijishughulisha na sera ya biashara ya watumwa na hawakurudi nyuma, wakaendelea nayo hadi kukomeshwa kwake.

Biashara ya watumwa ilizidi kupamba moto mnamo miaka ya themanini, hasa zaidi baada ya kumalizika vita ya uhuru wan chi ya Amerika.

Katika miaka ya sabini, wafanya biashara ya utumwa wachache wa Kifaransa walichukua mizigo kutoka Msumbiji kwenda visiwa vya West-Indies, kwa sababu waliiona hasara ilikuwa inaongezeka katika wakati wa kutafuta bidhaa zao zinazohamashika kwenye pwani ya Guinea.

Sasa, wakati wa amani, kwa mashindano makubwa zaidi ya kutafuta watumwa katika Afrika ya Magharibi, ilifunguliwa njia kwa ajili ya upanuzi mkubwa wa biashara ya watumwa ya Waamerika kutoka Afrika ya Mashariki.

Wakati huo huo meli za Wareno pia zilianza sehemu ya kufaa (ingawa ilikuwa bado ni ya kufuata) katika biashara ya watumwa kwenda kisiwa cha Mascarene. Tarakimu rasimi kutoka Msumbiji peke yake zinaonyesha kwamba tangu 1781 hadi 1794 jumla ya watumwa 46,461 walipakiwa kwenye meli za Kireno na za kigeni, ambazo karibu zote zilikuwa za Wafaransa.

Ikijumlishwa na idadi ndogo ya magendo, angalau watumwa 4,000 lazima walikuwa wanaondoka Msumbiji wakati wa kipindi hiki kila mwaka.”1

Ilikuwa katika hali hii ambayo Waarabu walipanua msaada wao kuwasaidia hawa wafanyabiashara ya utumwa wa Kikristo. Mwandishi huyo huyo anasema: “Baada ya Waarabu wa Oman kuitika wito wa baadhi ya watawala wa Kiswahili wa miji ya pwani na kwa msaada wao waliwatoa Wareno kutoka Mombasa mnamo 1698 na sehemu zingine muhimu za mbali, wao wenyewe walikuwa wanyonge sana kushughulika na jambo lingine zaidi ya kuwasumbua na kuwaibia watu hao hao waliowaomba msaada wao; lakini baada ya familia ya Busaid ilipowapindua Yarubi na kuanzisha utawala wao katika Oman mnamo 1744, wali- weza kuanza unyonyaji wa kiuchumi wenye faida kutoka kwa watu wa Afrika ya Mashariki.

Kama walivyofanya wafanya biashara wote wa zamani sehemu ya pwani, lengo lao kubwa na la msingi ni kupata pembe za ndovu, lakini kuanzia hapo pia tunaweza kuona ongezeko katika biashara ya watumwa.

“Hata hivyo, hakuna takwimu sahihi zozote zile zenye kuonyesha kuhusu ukubwa wa biashara ya utumwa iliyofanywa na Waarabu katika karne ya kumi na nane. Dalili ya kwanza iliopo inatoka kwa mfanya biashara ya watumwa wa Kifaransa aitwaye Jean Vincent Morice, ambaye alifanya biashara Zanzibar na Kilwa, ambayo ilikuwa bandari muhimu ya watumwa katika pwani, mnamo miaka ya 1770. Mnamo tarehe 14, September, 1776, Morice alifanya mkataba na Sultani wa Kilwa kwa ununuzi wa angalau watumwa 1,000 kwa mwaka.

Katika misafara mitatu kabla ya kuutia sahihi mkataba huu, Morice alikwisha nunua watumwa 2325 kwa ajili ya kuwasafirisha nje. Morice hatuambii Waarabu walikuwa wakiwachukua watumwa wangapi kutoka pwani kila mwaka, lakini kwa wazi aliona kuwa ilikuwa biashara kubwa kwa viwango vya Kifaransa.

Inaonekana ni sawa kusema kwamba angalau watumwa 2000 walikuwa wanachukuliwa kwa mwaka katika kipindi hicho. Kwa hiyo, licha ya kwamba Wafaransa hawakutawala biashara ya watumwa hapa kama walivyofanya Msumbiji, walikuwa kichocheo kwa mahitaji ya soko la watumwa katika kipindi ambacho biashara ya Waarabu ilikuwa bado ndiyo inakua katika uchanga wake.

Juhudi za Ufaransa ziliendelea hadi miaka ya 1780, lakini mnamo mwishoni mwa karne hiyo, juhudi hizi zilionyesha zilikwisha pungua sana umuhimu wake kuliko biashara ya Waarabu.

Mambo kadhaa mapya yalisababisha kuongezeka mahitaji ya watumwa kutoka Afrika ya Mashariki wakati wa karne ya kumi na tisa. Katika eneo la mamlaka la pwani ya Ureno, palikuwepo na ongezeko la juu sana katika biashara ya utumwa kwenda Brazil. Hii ilisababishwa na kuondolewa kwa familia ya kifalme ya Kireno kutoka Lisbon kupelekwa Brazil wakati wa Vita za Napoleon. Ruhusa maalum zilitolewa kwa Wabrazil na mara biashara inayoshamiri katika watumwa ikawa inaendeshwa kupitia Rasi ya Tumaini Jema huko Afrika ya kusini.2

“Sasa ni ukweli unaokubalika miongoni mwa wataalam wa historia makini wa Afrika ya Mashariki kwamba njia ndefu za biashara kati ya bara na pwani zilianzishwa hasa zaidi kwa kutumia ujasiri na moyo wa kujituma wa Waafrika. Kwa maneno mengine njia za biashara zilibuniwa na Waafrika kutoka bara kwenda pwani, wala si Waarabu, au Waswahili, ambao walisafiri kutoka pwani kwenda bara kupitia sehemu zisizojulikana.

Wafanya biashara wa Kiswahili walianza tu kutelekeza usalama wa pwani mnamo nusu ya pili ya karne ya kumi na nane, na walisafiri kufuata njia safi ambazo ziliendelezwa kwa miongo mingi kabla yake. Ni baada tu kuanza karne ya kumi na tisa ndipo wafanya biashara wa Kiarabu walijasiri kufuata njia hiyo.” 3

Wayao ambao walikuja kuwa wafanya biashara makini sana wa Kiafrika wa biashara ya watumwa katika Afrika ya Mashariki, hivyo walikuwa na desturi ya muda mrefu ya kubeba pembe za ndovu na bidhaa zingine halali kwenda pwani miongo mingi kabla ya mahitaji ya pamoja ya Wafaransa na Waarabu kutaka watumwa yalipoeleweka.”4

“Katika Afrika Magharibi njia hizi ziliendeshwa kwenda bara kutoka pwani na Waafrika ambao kazi yao hasa ilikuwa kutafuta watumwa. Watumwa walitawala biashara ya Afrika ya Magharibi tangu mwanzo. Katika Afrika ya Mashariki wala hapakuwepo na hali zilizolingana na hiyo. Biashara ya watumwa lazima ionekane kuwepo katika mazingira ya mapema zaidi, iliyokwishajengeka kwa umakini, na biashara yenye faida ya masafa marefu ambayo chimbuko lake ilikuwa ubebaji wa pembe za ndovu. Hii ni muhimu kukumbuka hasa kwa mikoa ya kusini ambalo kila mara ilikuwa hazina kuu ya “Biashara ya Utumwa katika Afrikamashariki.”5

Bwana Alpers anahitimisha, “lazima iwe wazi sasa kwamba fikira ya zamani inayotamkwa kiholela kwamba wengi wa watumwa walikamatwa na wafanya biashara wanyang’anyi wa Kiarabu na Kiswahili ni moja wapo ya mambo ya kubuniwa na ngano tu ambazo zimekuzwa kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika mashariki. Lakini lazima tuwe waangalifu tusifanye kosa la kutoa tathmini potofu kuhusu mchango waliotoa watu hawa kwenye biashara hii.” 6

Kwa mara nyingine, lazima nisisitize kwamba lengo langu si kudhihaki juhudi za kundi dogo la waadilifu ambao walikuwa wanashughulika na propaganda dhidi ya utumwa. Ninachotaka kuonyesha ni kwamba juhudi zao hazikufaulu (na hazingefaulu) hadi pale shinikizo la kiuchumi lilipoilaz- imisha kwanza Uingereza ilipolazimika kufuatana na matatizo ya kiuchumi kuanza kuzuia utumwa, biashara ya utumwa na halafu kukomesha utumwa.

Kwa kweli, Uingereza ilipojitokeza kwa ajili ya kutaka kukomesha utumwa haikusimama kwenye mapaa ya nyumba na kutangaza kwamba ilikuwa inakomesha utumwa kushindana dhidi ya wenye viwanda wa Kifaransa. Uingereza ililigeuza jambo hili kuwa suala la kimaadili na kiunyofu kabla haijatumainia kushinikiza serikali zingine kufuata mpango wake. Na ilifanya hivyo. Tunatambua jinsi Uingereza ilivyoanzisha vita si kwa lengo la kulinda maslahi ya himaya yake kiuchumi na kisiasa, lakini ilifanya hivyo ili “kulinda Uhuru wa Watu.”

Ndivyo ilivyokuwa kuhusu vita yake dhidi ya utumwa. Murua na maadili mema lilikuwa suala la waadilifu wachache tu ambao hawakuwa na uwezo. Suala halisi, kama serikali mbali mbali na walowezi na wakoloni walivyohusika, lilikuwa kuhusu uchumi.
  • 1. Alpers, op. cit., uk. 5-6
  • 2. Ibid uk. 7-8.
  • 3. Ibid, uk. 13.
  • 4. Bid, uk. 14.
  • 5. Ibid uk. 15.
  • 6. Ibid uk. 24.
 
Waislamu wengi wa kiafrika hawaijui Quran wala lugha inayotumika kwenye Quran.
Hawawezi kuweka aya za Quran hapa kwasababu hajui Quran wala hajui lugha ila atakimbilia kwenye Biblia kwasababu anaielewa.
Huyu ukimwambia akuhubirie ili uslimu 99% ya maneno yake yatatoka kwenye Biblia na 1% yatatoka kwenye Quran ndiyo maana waislamu wengi wapo hasa kwa sehemu alizokaa mwaarabu. Na umeshindwa kusambaa kwasababu maneno yote atakayohubiria 99% yatatoka kwenye Biblia.
Hapa angeweka aya za Quran zinazopinga itumwa ningemwelewa sana.

wewe unayeijua Quran mbona unayayatika tu huweki kitu ??
 
wewe unayeijua Quran mbona unayayatika tu huweki kitu ??
Naona maneno yote yanatoka kwenye Biblia kuliko Quran.
Hapa ungeshusha nondo za kwenye Quran ningeona umeiva sana kwenye Uislam. Ila naona umeiva sana kwenye Biblia.
Hii mada ilikuwa ya darasani ( elimu dunia) tulikuwa tunazungumzia kuhusu waraabu na biashara ya utumwa hapo ungeongezea biashara ya utumwa ya wazungu kupeleka watu Marekani na Mauritius.
Dini tuliletwa wafrika na tulikuwa na dini yetu. Tulikuwa hatuabudu imani moja Afrika nzima kila ukoo au kabila ilikuwa na imani yake.
Tulikuwa tunaamini wazee au watu waliokufa wenye nguvu ndiyo maana kulikuwa na matambiko.
 
Naona maneno yote yanatoka kwenye Biblia kuliko Quran.
Hapa ungeshusha nondo za kwenye Quran ningeona umeiva sana kwenye Uislam. Ila naona umeiva sana kwenye Biblia.
Hii mada ilikuwa ya darasani ( elimu dunia) tulikuwa tunazungumzia kuhusu waraabu na biashara ya utumwa hapo ungeongezea biashara ya utumwa ya wazungu kupeleka watu Marekani na Mauritius.
Dini tuliletwa wafrika na tulikuwa na dini yetu. Tulikuwa hatuabudu imani moja Afrika nzima kila ukoo au kabila ilikuwa na imani yake.
Tulikuwa tunaamini wazee au watu waliokufa wenye nguvu ndiyo maana kulikuwa na matambiko.

Baadhi ya mafundisho kutoka kwa Mtume Muhammad (rehema na amani ziwe juu yake):

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie) akisema: “Mja wa yeyote miongoni mwenu atakapomuandalia chakula na akamhudumia baada ya kukaa karibu na joto na moshi, basi naye (mtumwa) aketi pamoja naye na mle (pamoja naye), na ikiwa chakula kinaonekana kupungua, basi amwekee sehemu fulani (kutoka katika sehemu yake) - (msimulizi mwingine) Dawud akasema: "i. e. tonge moja au mbili". 4097. (Tafsiri ya Sahih Muslim, Kitabu cha Viapo (Kitab Al-Aiman), Kitabu 015, Namba 4096)"

Amesimulia Al-Ma'rur: "Katika Ar-Rabadha nilikutana na Abu Dhar ambaye alikuwa amevaa kanzu, na mtumwa wake pia alikuwa amevaa nguo kama hiyo. Niliuliza juu ya sababu yake. Akajibu: "Nilimtukana mtu. kwa kumwita mama yake kwa majina mabaya." Mtume akaniambia, 'Ewe Abu Dhar! Je, ulimtukana kwa kumwita mama yake kwa majina mabaya Bado una baadhi ya sifa za ujinga. Waja wako ni ndugu zako na Mwenyezi Mungu amewaweka chini amri yako.Basi aliye na ndugu chini ya amri yake amlishe anachokula na amvishe anachovaa.Usiwaombe (watumwa) kufanya mambo yaliyo nje ya uwezo wao (uwezo) na ukifanya hivyo basi saidia. wao.' (Tafsiri ya Sahih Bukhari, Imani, Juzuu 1, Kitabu cha 2, Namba 29)"

Imesimuliwa na Anas: "Mtume alisema, 'Hatokuwa na imani yeyote miongoni mwenu mpaka amtake ndugu yake (hii ni pamoja na watumwa, kwani mtumwa anahesabiwa kuwa ni ndugu kama ilivyoonyeshwa hapo juu] kile anachopenda kwa ajili yake." (Tafsiri ya Sahih Bukhari, Imani, Juzuu 1, Kitabu cha 2, Namba 12)"

Amesimulia Abu Musa: "Baadhi ya watu walimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu, 'Uislamu wa nani ni bora zaidi? Alijibu, 'Mtu anayeepuka kuwadhuru Waislamu (Isaya 56:5: Mwislamu ni jina la waumini wa siku zijazo. Majina ya wana na binti hayatakuwa "tena") kwa ulimi na mikono yake.' (Tafsiri ya Sahih Bukhari, Imani, Juzuu 1, Kitabu cha 2, Namba 10)"

Imesimuliwa na Abdullah bin Amr: "Mtu mmoja alimuuliza Mtume, 'Ni aina gani ya matendo au (sifa gani za) Uislamu ni nzuri?' Mtume akajibu, 'Kuwalisha (maskini) na kuwasalimu wale mnaowajua na msiowajua.' (Tafsiri ya Sahih Bukhari, Imani, Juzuu 1, Kitabu cha 2, Namba 11)"
 
Al Shabab wamepiga marufuku kutengeneza na kula sambusa - Somalia.

Hii ni kutokana ina shape ya pembe tatu, yaani ni kiwakilishi cha Ukristo (Utatu Mtakatifu/Trinity)

Hichi kitu kimenishangaza kwa nini kisibadilishwe umbo la duara au mstatili, badala ya kuwanyima watu kitafunwa wanachokipenda kisa ujinga walio nao kichwani.

Au ndio udogo wa kufikiri?
View attachment 2473792
Ni udogo wa akili tu wa hao jamaa
 
Hahaha hili nalo neno, hawa jamaa si wana elimu yao wanayoipa kipaumbele ambayo ni tofauti kabisa na Western system.
Sio kweli kabisa nilienda somalia miaka ya nyuma sana
Elimu yao ni hiyo uliyosoma tu tena wanaongea lugha 4 Italian, English na France na Arabic

Uislam ni mfumo wao wa maisha ila elimu zipo
 
Sio kweli kabisa nilienda somalia miaka ya nyuma sana
Elimu yao ni hiyo uliyosoma tu tena wanaongea lugha 4 Italian, English na France na Arabic

Uislam ni mfumo wao wa maisha ila elimu zipo

Hiyo Somalia wanayofundishwa MAKANISANI NI NYENGINE KABISA

waangalie Somali hii

 
Hiyo Somalia wanayofundishwa MAKANISANI NI NYENGINE KABISA

waangalie Somali hii


Ebanaee kweli nimeshangazwa. Sasa ni kipande gani ambacho Kenya Defence Force wapo kwaajili ya peace keeping mission?
Sasa nitaanza kuifuatilia Somalia, inawezekana We are being lied kuhusu hali ya Somalia kiujumla.
 
Sio kweli kabisa nilienda somalia miaka ya nyuma sana
Elimu yao ni hiyo uliyosoma tu tena wanaongea lugha 4 Italian, English na France na Arabic

Uislam ni mfumo wao wa maisha ila elimu zipo
Ok, ni tofauti na habari zinazosambaa sana kuhusu Somalia.
 
Hiyo Somalia wanayofundishwa MAKANISANI NI NYENGINE KABISA

waangalie Somali hii

Hiyo Mogadishu na ndio wanaoongea Italian ya zamani
I was there in 1987 ilikuwa hata hela yao ipo juu kuliko EA zote

Na hii video nimeiona imekaa vizuri sana kuliko wanaoweka somalia ya kuuwana tu kila kukicha

Daa kama jiji limerudi hivyo acha nikatembee beach yao ya Lidho
Asante kwa video hiyo
 
Hiyo Mogadishu na ndio wanaoongea Italian ya zamani
I was there in 1987 ilikuwa hata hela yao ipo juu kuliko EA zote

Na hii video nimeiona imekaa vizuri sana kuliko wanaoweka somalia ya kuuwana tu kila kukicha

Daa kama jiji limerudi hivyo acha nikatembee beach yao ya Lidho
Asante kwa video hiyo


na kuna nyumba zinauzwa Mogadishu fresh tu

 
Back
Top Bottom