Kazakh destroyer
JF-Expert Member
- Nov 16, 2017
- 3,278
- 6,843
Huwezi kuita hoja zangu nyepesi wakati wewe hujaleta nzito kuzinyepesisha za kwangu, mimi ni muislamu tena ninayeuelewa uislamu nakueleza mambo hayo hayaruhusiwi kwenye uislamu unazipinga hoja zangu kwa kuniambia kuna mtu alikuwa anamchinja mtu mwingine huku anasema allah akbar hapa mwenye hoja nyepesi ni nani?.Una hoja nyepesi Sana Kama pamba.
Wale waislamu pale German wanaopigania Hali kwa kuandamana ili wanawake waruhusiwe kuvaa hijab sijui niqab (I don't know the difference,naomba unifafanulie,so wale siyo waislamu kisa wanafanya maandamano na maandamano Ni Haram kwenye dini ya uislamu?
Kuna mahali mnafeli na mna hoja nyepesi Sana. Mtu anaua huku anataja jina la Mungu wenu Allah Tena huyu mtu ni imam kwenye msikiti,na kipindi chote anatambulika Kama "muislamu safi" mnakuja kumkana.. eti huyo siyo muislamu kisa kafanya mauaji,muislamu hawezi kufanya kitu kama hiko..!! Hoja nyepesi sana mko nazo,Kama hizi ulizozimention huko juu!!
Okay ngoja nikupe faida moja, kuna watu wanaitwa makhawaarij hawa hawakuanza leo wameanza ufisadi wao tangu karne za mwanzo kabisa kwenye historia ya uislamu, watu hawa ndio waliowaua watu watukufu na waheshimiwa katika uislamu na wamezungumzwa zaidi kwenye uislamu kwa lugha mbaya kuliko hata hiyo unayoisema wewe, na wao ndio watu waovu zaidi wanaouwawa chini ya mbingu na ni haki yao kuuwawa kama mtawala akiweza kufanya hivyo, watu wabaya kabisa na watu wanaotembea na mifumo yao ni kama alqaeda, alshabaab, isis, islamic jihad, boko haram n.k hata hawa hapa capo delgado msumbiji ni mfano wao..
Sasa hawa ni extremists na wanayoyafanya hayahusiani na uislamu kama nilivyokueleza tangu mwanzo sema sina muda ningekunukulia hadithi nyingi tu kuwasema vibaya wao.
Kuhusu wale waislamu wa ufaransa ziko fataawa nyingi tu kuwataka watoke kwenye nchi ambazo wanashindwa kudhihirisha dini yao kwa uhuru na si vyema kukaa kati ya watu ambao wanawanyima uhuru wa kuabudu totally, allah anasema kuwahusu watu kama hawa katika quran.
"Hakika wale ambao wanafishwa na malaika hali ya kuwa wamezidhulumu nafsi zao, wakiwaambia mlikuwa katika hali gani? watasema "tulikuwa ni madhaifu katika ardhi" watawaambia: hivi haikuwa ardhi ya allah ni pana mkahamia humo? basi hao mafikio yao ni jahannam, na marejeo mabaya zaidi ni hiyo jahannam"
Quran 4:97
So hao watu hakuna sheria inayowaruhusu kuandamana kwani ni kinyume na misingi ya uislamu na miongozo inawataka kujiweka mbali na sehemu kama hizo, kuhusu wale wauaji nimekueleza hapo juu.