Ni sawa lakini kuna makatazo kwetu kutumia biblia kwasababu hatujui la usahihi na la uongo kwa kule kubadilishwa mno vitabu vilivyotangulia.
Tutosheke mkuu wangu na quran iliyohifadhiwa kutokana na mikono ya watu waovu.
Ni aya gani imetukataza kutumia biblia ?? Kwani biblia ni kitabu cha nani ?
Kuna njia mbili zinazoweza kupitiwa ili kuufikia utambulisho wa Yesu Kristo na yaliyomo katika ujumbe wake.
Ya kwanza inaangazia makusanyo ya rekodi za kihistoria za wanahistoria wa kisasa kutoka katika maandiko na masalio ya kipindi hicho na ya pili inaangazia ripoti zilizomo katika Maandiko ya ufunuo. Kwa ukweli, kuna ushahidi mchache mno unaotufahamisha kuwa Yesu alikuwa ni nani, au unaobainisha ujumbe wake ulikuwa ni nini.
Nyaraka rasmi za kihistoria za kipindi hicho kwa hakika hazina rekodi yoyote juu ya Yesu. Msomi wa Biblia, R.T. France, anaandika,
"Hakuna andiko lolote la karne ya kwanza linalomtaja Yesu na hakuna kitu chochote au jengo lolote lililobakia na ambalo lina uhusiano naye."
Ukweli huu umewafanya baadhi ya wanahistoria wa Kimagharibi kukosea na kudai eti Yesu Kristo wa hakika hajapatapo kuwepo.
Kwa hiyo, kimsingi, utafiti lazima uegemee maandiko matakatifu yanayoeleza haiba na kazi za Yesu Kristo.
Maandiko matakatifu yatakayoulizwa ni yale yanayotambulikana kirasmi na dini zote mbili Ukristo na Uislamu.
Hata hivyo, kuchambua barabara, maelezo yaliyomo katika maandiko ya kidini, ni jambo la msingi kuanzia na kupima usahihi wa maandiko hayo.
Je, vitabu vya dini ni vyanzo vya kuaminika kuwa nyaraka za ushahidi, au ni ubunifu wa simulizi za kibinadamu na visaasili, au ni mchanganyiko wa yote mawili?
Je, Biblia, Agano la kale na Jipya ni maandiko ya ufunuo wa Mungu?
Je, Quran (Kurani) ni sahihi?
Kwa Biblia na Quran ili ziwe maneno matakatifu ya Mungu, lazima ziwe hazina kujipinga zenyewe kusikofafanulika, na kusiwe na shaka juu ya yaliyomo ndani yao wala juu ya watunzi wake.
Ikiwa hii ndio kadhia, basi yale yaliyomo katika Agano la kale, Jipya na Quran, ndipo yatakapozingatiwa kuwa ni vyanzo aminika vya maelezo yanayohusiana na ujumbe Yesu Kristo na haiba yake.