Sometime "Kataa ndoa" Uwa wana hoja

Sometime "Kataa ndoa" Uwa wana hoja

(A) โ€ข Waliopo kwenye ndoa, wanatamani kuachana na masuala ya ndoa

(B) โ€ข Ambao hawapo kwenye ndoa, wanatamani kufunga ndoa

"HII INAONESHA KUWA NDOA HAINA MAANA ๐Ÿค’๐Ÿค’..."
Ina maana ,maana kubwa ni uzazi tu, hayo mengine tunayoambiwa yanapatika humo kwa kiasi kikubwa ni kinyume chake
 
Hayo mambo yapo sana Afrika,jamii ya watu waliostarabika yapo kwa kiasi kidogo sana.
Na sababu kubwa Wanawake kwao ndoa ni kitega uchumi.
 
Wanapoendelea kukataa ndoa kwa muda mrefu hata kama wanatania baadae akili zao zitajengeka hivyo hivyo hakuna umuhimu wa ndoa. Wakija kushtuka utuuzima na uzee huu hapa.

Wengi wanaokataa ndoa, kisaikolojia hawapo sawa kwa sababu ya kushuhudia matatizo ya ndoa na kuyachukulia personally

Duniani kuna wawili wawili (ke na me) hata kwa wanyama na wadudu.

Ndoa ni tamu
 
Ina maana ,maana kubwa ni uzazi tu, hayo mengine tunayoambiwa yanapatika humo kwa kiasi kikubwa ni kinyume chake
Kama lengo ni Watoto Sawa.. But Waliopo kwenye NDOA Kwa maisha ya Sasa, wanapitia vipindi vigumu sana.
 
Wanapoendelea kukataa ndoa kwa muda mrefu hata kama wanatania baadae akili zao zitajengeka hivyo hivyo hakuna umuhimu wa ndoa. Wakija kushtuka utuuzima na uzee huu hapa...
Hakuna ndoa tamu huo ni uongo,ndoa ni tamu wanandoa wakisha fika uzee basi.

Ndoa 99% ni karaha & 1% ndio furaha.
 
Vijana wa kiume sasa hivi wamekuwa walaini sana kumuogopa mwanamke ambae ameumbwa kutoka kwa ubavu wake.

Sawa, hatukatai, ndoa zinachangamoto. Lakini ukweli kila kitu kinachangamoto dunia hii hata maisha yenyewe ni changamoto, shule ni changamoto na biasharani ni changamoto.

Dunia yenyewe imeumbwa katika mifumo ya changamoto na changamoto haziishi mpaka kufa kwako.

Kukimbia changamoto na kuzikataa inakufanya usikuwe kutoka nafasi moja kwenda nyengine na hata kiakili.

Vijana msikatae ndoa, kwa sababu wengine wanaeleza matatizo ya ndoa. Watoto msiwanyime haki yao ya kupata mapenzi ya baba na mama kwa u-selfish wako wa kutaka kuishi mwenyewe.
 
Ndio ni karaha na mateso.
Tembea uone, usikae maeneo ya aina moja au kama uliona ndugu au mzazi akiteseka kwenye ndoa haimaanishi na wewe utateseka.

Badilisha mtazamo wako upande mwengine ufungue ufahamu wako uone mengi mazuri ambayo yapo kwenye ndoa.

Ndoa ni maisha kama maisha mengine na wewe ndo dereva wa taasisi ya ndoa. Kama wewe ndo kichwa cha familia unamtazamo hasi utashindwa kuwaongoza mke na watoto.

Wewe kama baba/ mume ndo kila kitu. Sio wanawake wote wanaoolewa ni malaya, wengine wanahofu ya Mungu na wanaijua thamani yao.

Muombe Mungu akupe mke mwema, mwenye maadili atakaekuheshimu na kukutunzia thamani yako. Sio kila mke lazima achepuke, hapana.
 
Kama lengo ni Watoto Sawa.. But Waliopo kwenye NDOA Kwa maisha ya Sasa, wanapitia vipindi vigumu sana.
Sana ndugu yangu kati ya kumi wenye ndoa zaidi ya nusu wana lia sio wanaume tu hata wanawake, source ni matokeo yalio kinyume na matarajio.
 
Hakuna ndoa tamu huo ni uongo,ndoa ni tamu wanandoa wakisha fika uzee basi.

Ndoa 99% ni karaha & 1% ndio furaha.
Utamu wa kitu chochote ni kwa wewe mwenyewe mlaji unakichukuliaje na ladha yake umeielewa vipi. Hata vyenye chumvi, sukari, limao, uchungu na harufu kwa wengine ni vitamu.

Ili uone utamu wa ndoa inabidi akili yako ipokee mtazamo chanya kuhusu ndoa ndo utamu utauona.

Zipo familia zinaishi kwenye ndoa ambazo zina furaha na amani na utulivu wa hali ya juu. Tembea uone, ulizia na uambiwe ili upate kujifunza.

Kila kitu kina mapungufu na uzuri katika dunia hii, ni wewe mwenyewe uchague kuona mazuri au mabaya.
 
images (1).jpeg

Vikataa ndoa vyenyewe
 
Back
Top Bottom