Somo kutoka Uchina, namna walivyoweza kuendeleza biashara ya Bandari

Tusilaumiane bali tujifunze na tutoe mustakabali wa Taifa letu kwa upendo tu....
naweka document ili tuendelee kujifunza.
Asante.

Kwa juu juu, nilichojifunza ni jinsi China ilivyoanza kuendeleza Bandari zake kwa mitaji ya wawekezaji wa nje.

Nanukuu na kuweka msisitizo kwa rangi nyekundu kinachokosekana kwenye makubaliano/mkataba wa ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai (IGA) unaomteua DPW na kumpa "exclusive rights" kuendeleza na kuendesha Bandari za Tanzania Bara. Mkataba ambao hautoi nafasi kwetu kuingia "Phase 2" ya kuendeleza na kuendesha Bandari zetu wenyewe kwa kuwa IGA haina muda wa kikomo (Ibara ya 23).

In 1984, China began decentralizing port governance by piloting a dual management principle of port governance at the Port of Tianjin, where both the central and municipal governments played a role. By 1989, most major ports were managed under this dual model. Provincial and city governments allocated land and provided tax advantages to stimulate port development. This period was characterized by initial steps toward the commercialization of port activities, such as allowing cargo owners to build their own facilities and permitting some foreign companies to operate container terminals, albeit under a tight regulatory framework.
 
Usisahau ukaweka jinsi watu wa ulaya, waingereza, wareno walivyoweza kujipenyeza na kuwatawala wachina kwa kutumia bandari zao wenyewe....na hatimaye kutawala Hongkong au bandari ya macau. Historia huwa inajirudia.

Haya ya Special economic zones wanazotaka katika mikataba hii, tunaweza kulinganisha na Canton systems
Watu wanawaza wizi tu huku..... Kikubwa kama muelekeo upo hakuna namna
 
Upinzani unaoendelea ni ule uliojaa machungu ya Kihistoria. Kutawaliwa na Waarabu n.k

Uchina, ukiangalia historia ya bandari zake, utaona kuna ufanano na yanayoonekana kufanyika kwetu leo hii. China nayo ilikuwa katika Umasikini, China nayo ilikuwa na Viongozi walioamua kwa nia njema kabisa(pamoja na rushwa) kufungua nchi, na walianza na Bandari! Canton... na Macau......yaliyowakuta ni historia iliyoandikwa.

Walikuja kushtuka baadae sana, na ukiangalia historia hio utaona ni machungu waliyopata ndio iliwapeleka kupata akili na kuwa na maono ya kuendeleza bandari zake wenyewe kama ilivyoletwa na mleta mada.....ndio ilikuwa njia pekee ya kuondokana na Umasikini, yaani kurudisha bandari hizo chini ya himaya zao. Matokeo yake tunayaona.

Tanzania, tunaweza kuyakataa haya mapema kabla mambo hayajaharibika. Watanzania wanao hoja halali kabisa ya kukataa Bandari yao kuachiwa kwa Waarabu. Hivi hujiulizi hata baada ya Miaka yote hiyo bado wana tuona mafirauni halafu sie ndio tuwaone wamebadilika?

Soma historia kama ilivyoletwa na mleta mada, ila usisahahu kurudi nyuma kidogo uone ni sababu zipi zilizowafanya wachina wawe kama walivyo sasa....Hatuna haja Watanzania kufika huko.
 
Asante.

Kwa juu juu, nilichojifunza ni jinsi China ilivyoanza kuendeleza Bandari zake kwa mitaji ya wawekezaji wa nje.

Nanukuu na kuweka msisitizo kwa rangi nyekundu kinachokosekana kwenye makubaliano/mkataba wa ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai (IGA) unaomteua DPW na kumpa "exclusive rights" kuendeleza na kuendesha Bandari za Tanzania Bara. Mkataba ambao hautoi nafasi kwetu kuingia "Phase 2" ya kuendeleza na kuendesha Bandari zetu wenyewe kwa kuwa IGA haina muda wa kikomo (Ibara ya 23).

In 1984, China began decentralizing port governance by piloting a dual management principle of port governance at the Port of Tianjin, where both the central and municipal governments played a role. By 1989, most major ports were managed under this dual model. Provincial and city governments allocated land and provided tax advantages to stimulate port development. This period was characterized by initial steps toward the commercialization of port activities, such as allowing cargo owners to build their own facilities and permitting some foreign companies to operate container terminals, albeit under a tight regulatory framework.
CCM do not want to learn how to formulate development strategies they are on rush to copy and paste without the knowledge of the aftermath of many projects and policies
 
Tusilaumiane bali tujifunze na tutoe mustakabali wa Taifa letu kwa upendo tu....
naweka document ili tuendelee kujifunza.
Hili swala la kubinafsisha kila kitu ni ukoloni mpya unaopigiwa chapuo na hizi nchi za magharibi, kwa sababu zinafaidika moja kwa moja na uwekezaji wa kinyonyaji na kufanya nchi hizi ziendelee kuwa tegemezi kwao miaka yote.

Kila jambo tunalotakiwa kulifanya wenyewe, tunaambiwa tubinafsishe, huku kubinafsisha sasa imekuwa ni kichaa, na watu kama Samia hawajui jambo jingine lolote, bali kubinafsisha tu kila kitu!
Bora angekazania kuwajengea uwezo wananchi wetu ili waweze kuwa wawekezaji wa miradi hii mingi tunayohimizwa kubinafsisha, lakini hapana, ni watu toka nje ndio wenye sifa hizo

Tuna jua hapa na upepo tuliopewa na Mwenyezi Mungu, lakini tunahimizwa kutafuta watu waje watumie raslimali hiyo kujineemesha wao na mataifa yao kwa mgongo wetu

Badala ya kusimamia mashirika yetu yafanye vizuri, akina Samia wao wanaona kazi hiyo ni ngumu kuifanya kuliko kuleta watu toka nje.

Shirika la ndege Ethiopia linafanya vizuri, wao wana kitu gani kinachosababisha iwe hivyo, ambacho wa hapa kwetu Tanzania hawana?

Hayo mashirika ya China yaliyosambaa dunia nzima, ni mali za serikali ya China, wao walifanya nini wakafanikiwa hivyo badala ya kwenda kutafuta watu wengine wakawafanyie kazi hizo?

Sisi hata ule moyo wa kujitutumua umekwisha kabisa. Hawa wakoloni wametuingia kwelikweli akilini mwetu

Magufuli alikuwa na madhaifu mengi, lakini alikuwa na uthubutu wa kuamini kwamba kuna mambo tunaweza kuyafanya sisi wenyewe.
Kama hatujui, hata kujifunza kwa hao wanaojua sasa tumekata tamaa?
 
Upinzani unaoendelea ni ule uliojaa machungu ya Kihistoria. Kutawaliwa na Waarabu n.k

Uchina, ukiangalia historia ya bandari zake, utaona kuna ufanano na yanayoonekana kufanyika kwetu leo hii. China nayo ilikuwa katika Umasikini, China nayo ilikuwa na Viongozi walioamua kwa nia njema kabisa(pamoja na rushwa) kufungua nchi, na walianza na Bandari! Canton... na Macau......yaliyowakuta ni historia iliyoandikwa.

Walikuja kushtuka baadae sana, na ukiangalia historia hio utaona ni machungu waliyopata ndio iliwapeleka kupata akili na kuwa na maono ya kuendeleza bandari zake wenyewe kama ilivyoletwa na mleta mada.....ndio ilikuwa njia pekee ya kuondokana na Umasikini, yaani kurudisha bandari hizo chini ya himaya zao. Matokeo yake tunayaona.

Tanzania, tunaweza kuyakataa haya mapema kabla mambo hayajaharibika. Watanzania wanao hoja halali kabisa ya kukataa Bandari yao kuachiwa kwa Waarabu. Hivi hujiulizi hata baada ya Miaka yote hiyo bado wana tuona mafirauni halafu sie ndio tuwaone wamebadilika?

Soma historia kama ilivyoletwa na mleta mada, ila usisahahu kurudi nyuma kidogo uone ni sababu zipi zilizowafanya wachina wawe kama walivyo sasa....Hatuna haja Watanzania kufika huko.
Mchina alijipanga katika nyanja nyingi hasa human resource,,,, huku hamna hilo, wasomi wetu wanawaza wizi tu
 
Tusilaumiane bali tujifunze na tutoe mustakabali wa Taifa letu kwa upendo tu....
naweka document ili tuendelee kujifunza.
Hilo somo la College unawapa watu wa Primary School unadhani watalijua kweli? Wao wanataka maswali ya multiple choice (A,B,C,D) wakitegemea kubahatisha; ukiwaambia wasome na kuandika summary ya waliyosoma katika paragraph moja tu basi ujue watakuita wewe dikteta.
 
Tusilaumiane bali tujifunze na tutoe mustakabali wa Taifa letu kwa upendo tu....
naweka document ili tuendelee kujifunza.
Kabla ya hilo la Bandari lipi amabalo tumejifunza toka kwa hao wachina na wengine na tukaliendeleza? TAZARA Reli iko ohehahe sasa tunaweza kujifunza kweli kuhusu kuendesha Bandari?
 
Hili swala la kubinafsisha kila kitu ni ukoloni mpya unaopigiwa chapuo na hizi nchi za magharibi, kwa sababu zinafaidika moja kwa moja na uwekezaji wa kinyonyaji na kufanya nchi hizi ziendelee kuwa tegemezi kwao miaka yote.

Kila jambo tunalotakiwa kulifanya wenyewe, tunaambiwa tubinafsishe, huku kubinafsisha sasa imekuwa ni kichaa, na watu kama Samia hawajui jambo jingine lolote, bali kubinafsisha tu kila kitu!
Bora angekazania kuwajengea uwezo wananchi wetu ili waweze kuwa wawekezaji wa miradi hii mingi tunayohimizwa kubinafsisha, lakini hapana, ni watu toka nje ndio wenye sifa hizo

Tuna jua hapa na upepo tuliopewa na Mwenyezi Mungu, lakini tunahimizwa kutafuta watu waje watumie raslimali hiyo kujineemesha wao na mataifa yao kwa mgongo wetu

Badala ya kusimamia mashirika yetu yafanye vizuri, akina Samia wao wanaona kazi hiyo ni ngumu kuifanya kuliko kuleta watu toka nje.

Shirika la ndege Ethiopia linafanya vizuri, wao wana kitu gani kinachosababisha iwe hivyo, ambacho wa hapa kwetu Tanzania hawana?

Hayo mashirika ya China yaliyosambaa dunia nzima, ni mali za serikali ya China, wao walifanya nini wakafanikiwa hivyo badala ya kwenda kutafuta watu wengine wakawafanyie kazi hizo?

Sisi hata ule moyo wa kujitutumua umekwisha kabisa. Hawa wakoloni wametuingia kwelikweli akilini mwetu

Magufuli alikuwa na madhaifu mengi, lakini alikuwa na uthubutu wa kuamini kwamba kuna mambo tunaweza kuyafanya sisi wenyewe.
Kama hatujui, hata kujifunza kwa hao wanaojua sasa tumekata tamaa?
Mkuu umeandika mengi tena kwa uchungu lakini sasa kuna vitu Tanzania haviwezekani .Hatujawahi kuandaa rasilimali watu wakuja kufanya kazi kama mashine za kutusaidia,hata hao wasomi waliobahtika kukanyaga shule hakuna lolote wanalolifahamu kwa aababu ya miraala walioisoma ambayo haiwaandai kupata tafakuri na kuweza kuchambua vitu vingi kwa umakini. Mfano kama huyo Samia ni msomi wa masters lakini tafakuri yake ni ndogo ,hao sijui maprofesa sijui madaktari ndoo hakuna kitu kabisaaa.
 
Mchina alijipanga katika nyanja nyingi hasa human resource,,,, huku hamna hilo, wasomi wetu wanawaza wizi tu
Mada inazungumzia, kujifunza, wewe unajikita kwenye kulalama tu na kutoa tuhuma za kipropaganda...hebu jiridhie kilichowatokea wachina mpaka walipofikia hapo walipofikia! Jiulize, ni kwanini wachina wa leo hii wanasheria kali za Usaliti? Uhujumu Uchumi, Wizi wa Rasilimali za Taifa n.k kwanini?? Nikupe jibu jepesi tu...ni kwa sababu hayo yalikuwa yakitokea nchini mwao! Sasa kutuhumu tu kuwa kuna wizi huku na kwa lugha unayotumia ni kama nakusikia ukidai na kuashiria ndio hulka ya Mwafrika na ya Mtanzania wakati ukijuwa hulka za Binadamu zipo pale pale! Unakuwa hauitendei haki watu wa Afrika......Yaani hulka zinafanana, na ndio maana unaona Dini na madhehebu yote yanakataza vitu hivyohivyo....Kuua, Kuzini, Kuiba n.k ni dhambi tu.
Nakushauri, upitie Historia ya Macau na Hongkong ujue ni mikataba gani walikuwa nayo kwenye Bandari zao nyakati hizo na yaliyojiri baada ya hapo! Nakuhakikishia, huu wasiwasi na mashaka tuliyokuwa nayo is not in vain braza. Historia ndio inatufundisha hivyo! Utagundua mengi tu.
 
China imekua reference san kwa viongoz wetu ni jambo zuri sana, lakn kwann hawataki kufuata reference za China ku apply sheria kali dhidi ya wabadhirifu na mafisad kama uchina?
Je unakubali mapigo ya "Simba wa Yuda" na kama unakubali hizo sheria kali unajua zilikuwa zipo ukingoni tu,? na kama hukubali ujiulize ni kwanini...? haukubali....tafadhali ondoa sababu za kuchomekachomeka.
Hatahivyo naunga mkono huo mtazamo wako.
 
Back
Top Bottom