Mada inazungumzia, kujifunza, wewe unajikita kwenye kulalama tu na kutoa tuhuma za kipropaganda...hebu jiridhie kilichowatokea wachina mpaka walipofikia hapo walipofikia! Jiulize, ni kwanini wachina wa leo hii wanasheria kali za Usaliti? Uhujumu Uchumi, Wizi wa Rasilimali za Taifa n.k kwanini?? Nikupe jibu jepesi tu...ni kwa sababu hayo yalikuwa yakitokea nchini mwao! Sasa kutuhumu tu kuwa kuna wizi huku na kwa lugha unayotumia ni kama nakusikia ukidai na kuashiria ndio hulka ya Mwafrika na ya Mtanzania wakati ukijuwa hulka za Binadamu zipo pale pale! Unakuwa hauitendei haki watu wa Afrika......Yaani hulka zinafanana, na ndio maana unaona Dini na madhehebu yote yanakataza vitu hivyohivyo....Kuua, Kuzini, Kuiba n.k ni dhambi tu.
Nakushauri, upitie Historia ya Macau na Hongkong ujue ni mikataba gani walikuwa nayo kwenye Bandari zao nyakati hizo na yaliyojiri baada ya hapo! Nakuhakikishia, huu wasiwasi na mashaka tuliyokuwa nayo is not in vain braza. Historia ndio inatufundisha hivyo! Utagundua mengi tu.