Pac the Don
JF-Expert Member
- Feb 17, 2021
- 6,170
- 7,710
Kwamba kuweka sheria kali dhidi ya wabadhirifu na mafisad ni za kuchomekachomeka? NB; ili Taifa lisonge mbele kimaendeleo ni lazima kuwepo na sheria kali dhidi yao na ziwe active kwa kiongoz yeyote au raia yeyote!! Tutajidanganya san tu kupata maendeleo ya kweli huku tuki bless ufisadi!!!Je unakubali mapigo ya "Simba wa Yuda" na kama unakubali hizo sheria kali unajua zilikuwa zipo ukingoni tu,? na kama hukubali ujiulize ni kwanini...? haukubali....tafadhali ondoa sababu za kuchomekachomeka.
Hatahivyo naunga mkono huo mtazamo wako.
Andika hata page 100 wabongo wanachojua ni wizi na kujazana kwenye Vitengo basMada inazungumzia, kujifunza, wewe unajikita kwenye kulalama tu na kutoa tuhuma za kipropaganda...hebu jiridhie kilichowatokea wachina mpaka walipofikia hapo walipofikia! Jiulize, ni kwanini wachina wa leo hii wanasheria kali za Usaliti? Uhujumu Uchumi, Wizi wa Rasilimali za Taifa n.k kwanini?? Nikupe jibu jepesi tu...ni kwa sababu hayo yalikuwa yakitokea nchini mwao! Sasa kutuhumu tu kuwa kuna wizi huku na kwa lugha unayotumia ni kama nakusikia ukidai na kuashiria ndio hulka ya Mwafrika na ya Mtanzania wakati ukijuwa hulka za Binadamu zipo pale pale! Unakuwa hauitendei haki watu wa Afrika......Yaani hulka zinafanana, na ndio maana unaona Dini na madhehebu yote yanakataza vitu hivyohivyo....Kuua, Kuzini, Kuiba n.k ni dhambi tu.
Nakushauri, upitie Historia ya Macau na Hongkong ujue ni mikataba gani walikuwa nayo kwenye Bandari zao nyakati hizo na yaliyojiri baada ya hapo! Nakuhakikishia, huu wasiwasi na mashaka tuliyokuwa nayo is not in vain braza. Historia ndio inatufundisha hivyo! Utagundua mengi tu.
Wasomi ila bado wanajikomba wapate ulaji kitengo,,, sasa kwa akili hizi ndo uziweke ziendeshe bandariProfesa kabudi badala ya kufanya KAZI Kwa weledi yeye anasema ametolewa jalalani
Hapo hakuna kiongozi atakayekubali kumfanyia kazi hiko kipengeleChina imekua reference san kwa viongoz wetu ni jambo zuri sana, lakn kwann hawataki kufuata reference za China ku apply sheria kali dhidi ya wabadhirifu na mafisad kama uchina?
Na hapo ndipo panapofanya kupata maendeleo Nchi hii itakua ngumu sana!Hapo hakuna kiongozi atakayekubali kumfanyia kazi hiko kipengele
Tena michina ni mijizi kwelikweli, lakini wakiwa huko kwao hawathubutu kuiba wakijua watakipata cha moto.China imekua reference san kwa viongoz wetu ni jambo zuri sana, lakn kwann hawataki kufuata reference za China ku apply sheria kali dhidi ya wabadhirifu na mafisad kama uchina?
Upo sahihi ingawa zigo hili la ufisadi tusimtwishe Samia cz ni mfumo uliooza wa kifisadi tang miaka ming san. Solution ya kweli ni revolution ya katiba!!Tena michina ni mijizi kwelikweli, lakini wakiwa huko kwao hawathubutu kuiba wakijua watakipata cha moto.
Hapa kwetu ni rahisi sana kuvidhiti hivi vijizi vyetu uchwara tukipata viongozi wasiovumilia upumbavu huu unaozidi kuimarika sasa hivi.
Kwa bahati mbaya kabisa, Samia ni kama ndiye mlezi mkuu wa hivi vijambazi vyetu hapa!
Sisi tatizo letu ni viongozi majizi tulio naoUpinzani unaoendelea ni ule uliojaa machungu ya Kihistoria. Kutawaliwa na Waarabu n.k
Uchina, ukiangalia historia ya bandari zake, utaona kuna ufanano na yanayoonekana kufanyika kwetu leo hii. China nayo ilikuwa katika Umasikini, China nayo ilikuwa na Viongozi walioamua kwa nia njema kabisa(pamoja na rushwa) kufungua nchi, na walianza na Bandari! Canton... na Macau......yaliyowakuta ni historia iliyoandikwa.
Walikuja kushtuka baadae sana, na ukiangalia historia hio utaona ni machungu waliyopata ndio iliwapeleka kupata akili na kuwa na maono ya kuendeleza bandari zake wenyewe kama ilivyoletwa na mleta mada.....ndio ilikuwa njia pekee ya kuondokana na Umasikini, yaani kurudisha bandari hizo chini ya himaya zao. Matokeo yake tunayaona.
Tanzania, tunaweza kuyakataa haya mapema kabla mambo hayajaharibika. Watanzania wanao hoja halali kabisa ya kukataa Bandari yao kuachiwa kwa Waarabu. Hivi hujiulizi hata baada ya Miaka yote hiyo bado wana tuona mafirauni halafu sie ndio tuwaone wamebadilika?
Soma historia kama ilivyoletwa na mleta mada, ila usisahahu kurudi nyuma kidogo uone ni sababu zipi zilizowafanya wachina wawe kama walivyo sasa....Hatuna haja Watanzania kufika huko.
Hawa ndilo tatizo letu kubwa. Sijui tufanyeje kuondokana na hali hii!Sisi tatizo letu ni viongozi majizi tulio nao