๐ Kumbuka: Katika somo lililopita tuliongelea tarehe muhimu za kuzingatia wakati wa gawio.
Siku ya leo tutaangazia maswali muhimu ambayo inabidi ujiulize kabla ya kuwekeza.
Unajiuliza lini uanze kuwekeza? ๐ญ๐ฐ
Kabla hujachukua hatua ya kuwekeza, kuna mambo maswali muhimu inabidi ujiulize.
โJe, una emergency fund? ๐จ๐ผ
Kabla ya kuwekeza, hakikisha una akiba ya dharura ya miezi 3โ6 ya gharama za maisha. Hii ni ngao yako dhidi ya matatizo ya ghafla kama magonjwa au kupoteza kazi.
โJe, una madeni yenye riba kubwa? ๐ณ๐ฅ
Kama unadaiwa na riba ni kubwa ni bora kulipa kwanza kabla ya kufikiria kuwekeza.
โJe, utahitaji hiyo pesa muda wowote hivi karibuni? โณKama ndio, basi hujafikia muda sahihi wa kuwekeza. Hifadhi hiyo pesa kwa matumizi ya karibu.
โJe, unaelewa aina ya uwekezaji unayotaka kufanya? ๐๐
Usiwekeze tu kwa sababu watu wengine wanafanya hivyo. Jifunze vizuri na fahamu unachoweka pesa zako.
โ
Ukikidhi haya yote โ hongera! Uko tayari kuanza kuwekeza.
โLakini kama bado hujakamilisha haya mambo, usiwe na haraka! Anza kwa kuweka akiba, kulipa madeni, na kujifunza zaidi kuhusu uwekezaji.
Elimu ya fedha ni hatua ya kwanza ya uhuru wa kutilize.
Usikose somo lijalo ๐ซต
GODFREY DENIS
0763721523
Millennium Investors Community Co-founder