SOMO LA BURE: Namna ya kuagiza bidhaa kutoka CHINA kwa ajili ya biashara (jumla) Kupitia Mtandao alibaba kwa kutumia simu yako

Mfano agent wa hii kitu nampataje
mkuu una uzoefu wa kuagiza bidhaa mtandaoni? kama hauna umeusoma huu uzi wangu vizur...
maana nimefafanua kila hatua kuanzia mwanzo mpka mwisho mpka namna ya kumpata agent...
Nakuuliza haya lengo ni kuweka tahadhari huko mbeleni usije kwama au kupotea kwenye process yako ya kupata bidhaa.
 
Kwenye uzi sijaona sehemu ulioelezea kuhusu kumpata agent
 

Attachments

  • Screenshot_20241219-200546.png
    203.4 KB · Views: 8
Kwenye uzi sijaona sehemu ulioelezea kuhusu kumpata agent
soma vzur sehemu ya mwisho ya uzi. maagent ni kampuni za kitanzania ambazo nyingi utazipata instagram na nikaorodhesha majina yao.

Ila kampuni yangu pendwa nikatuma na instagram account yao..
au unaweza watafuta kwa website yao shamwaa africa
 
Ili kujuabgharama za kusafirisha mzigo wako hadi unaipata Tanzania,baada ya final price ya manunuzi na supplier wako muulize muulize kuhusu CBM na Weight ya mzigo wako.

Then watafute mawakala wa usafirishaji toka China to Tanzania,uwaambie aina yako ya mzigo na details zake ambazo ni CBM kama kwa meli na KG kama kwa ndege.

Wao watakupatia bei za usafirishaji hadi Tanzania.kwa meli watakupa bei kuwa 1CBM ni USD flani,then wewe zidisha CBM zako na bei walokupa utapata bei ya usafirishaji hadi Dar es salaam

Mizigo ya loose cargo bei za CBM zinajumlisha na ushuru.Ukilipia bei za CBM hautalipa tena ushuru
 
Ahsante mkuu hapa nimeelewa vyema
 
daah wewe jamaa ubarikiwe pakubwa sana aisee.
siamini kama leo hii bado tuna watu wema hivi kama wewe.

ubarikiwe sana kiongozi. wewe una roho ya kizungu sana roho ya kitajiri. maana waafrika tumeshapoteana sana tumekengeuka sana tumekuwa wa hatari kuliko mbwa mwitu. ni ngumu mtu akupe madini mujarabh kama hivi.
 
🙏🙏🙏
 
wakuu.....hawa silent ocean wanacharge bei gani kwa cbm? make nawacheki hawarespond

mzigo wangu una 0.28cbm 56kg
 
wakuu.....hawa silent ocean wanacharge bei gani kwa cbm? make nawacheki hawarespond

mzigo wangu una 0.28cbm 56kg

Mkuu kuna options nyingi kama hujibiwi na Silent Ocean.Watu wengi wamekariri wapi wasafirishe mizigo,ila kuna options nzuri nyingi sana ukichukua muda kuangalia reviews za kampuni zingine huduma nzuri na bei nzuri.

Nakupa hii cheki kampuni inaitwa Simba cargo,fanya utafiti wako,wakikuridhisha wajatibu hao.Wako very cheap wanafanya 380$/CBM.

Mahesabu yako yatakiwa 0.28*380= 106$
 
Unakuta wameweka let's bidhaa inauzwa 2,000 per piece ukiwacheki wanakwambia $8 per piece hii imekaaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…