Somo la kihistoria: Tanzania inawahitaji sana diaspora katika kuleta maendeleo

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,775
Reaction score
71,893
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI

Katika kusoma kwangu historia ya dunia, hasahasa ya miaka 300 iliyopita sijawahi kuona popote mabadiliko makubwa yamefanyika ndani ya nchi fulani bila msaada wa Diaspora.

Katika miaka 300 iliyopita, mapinduzi makubwa ya kisiasa ambayo ni somo kwa dunia nzima yalifanyika kwenye maeneo yafuatayo, na kote kulikuwa na ushirikishwaji mkubwa wa Diaspora:

1. Mapinduzi ya Marekani 1776-1783.
2. Mapinduzi ya Ufaransa 1789
3. Mapinduzi ya Urusi 1917
4. Mapinduzi ya Uchina 1949
5. Kuzaliwa kwa Israeli 1948

Mpaka leo hii, nchi kama Marekani, Ufaransa, Urusi, Uchina na Israeli zinategemea DIASPORA katika kutekeleza sera zao za mambo ya nje, sera za usalama na sera za kiuchumi. Kiufupi, kama kuna nchi inaamini inaweza kufanya jambo lolote kwenye dunia hii ya leo kwa kutegemea wasomi wa ndani peke yake inajidanganya mno.

Nguvu ya mataifa kama Israeli na Uchina, haipo kwa raia wake wanaoishi ndani bali nje. Leo hii, Israeli imefanikiwa mno kuweza kuinyamazisha dunia dhidi ya yale mauaji inayofanya GAZA kwasababu hakuna nchi kubwa duniani ambayo haina Wayahudi kwenye sehemu nyeti.

Prof John Mearsheimer aliandika kitabu kilichozua taharuki, "The ISRAEL LOBBY & US FOREIGN POLICY", kilichoelezea kwamba ndani ya Marekani kuna kundi lenye nguvu linalohakikisha sera za Marekani zinalinda maslahi ya Israeli. Hili kundi lina taasisi kama AIPAC, World Zionist Congress, ADL, Christians For Israel n.k ambazo huwa zinatumia fedha nyingi kuhakikisha wabunge wa Marekani, vyombo vya habari, taasisi za dini na vyuo vikuu vinakuwa na sera Pro-Israel.

Uchina ndiyo hatari kuliko hata Israeli. Diaspora wa Uchina wako kila sehemu hii dunia. Marekani wamejaa tokea mwaka 1815 ambako waliitwa kama wafanyakazi wa shughuli mbalimbali na wakabaki kule mpaka leo hii. Asia wamejaa kwenye nchi kama Singapore na Malaysia. Hapa Afrika ndiyo usiseme, mpaka sasa inasemekana bara zima limepokea zaidi ya DIASPORA wa kichina Milioni 1.

Kuna kitabu kimeandikwa na Howard W.Frech, kinaitwa "China's Second Continent: How A Million Immigrants Are Building A New Empire in Africa" ameelezea undani wa Diaspora wa kichina na mchango wao kwa maendeleo ya Uchina. Leo hii hakuna taifa la Afrika ambalo linaweza kupanga mkakati mkubwa wa maendeleo na kufanikiwa kuyakwepa makampuni ya kichina, iwe kwenye elimu, ujenzi au mikopo.

Nilikuwa nilikuwa nasikiliza Podcast ya Lex Friedman, akiwa anamhoji afisa wa shirika la ujasusi la Marekani Andrew Bustamente. Alimuuliza ni shirika gani la kijasusi lina nguvu duniani kwasasa, akajibiwa kwamba ni The Ministry of State Security (MSS) a.k.a The Guoanbu ya Uchina. Bustamente alimpa sababu kubwa kwamba, nguvu yake inatokana na DIASPORA wa Uchina waliosambaa duniani kote.

Akakazia na kusema kwamba, raia wa Uchina hata azaliwe Marekani, huwa haachi asili yake, ni lazima ajiite Mchina. Wengi wa hawa DIASPORA ndiyo wanatumiwa na Uchina katika kufanya kazi za ujasusi, uchumi na kiutamaduni. Mfano mzuri tu, Prof Huajian Gao.

Prof Gao alizaliwa Uchina na akaenda kuishi Marekani kwa miaka zaidi ya 30 akisoma Harvard University na kufundisha Stanford University, mambo ya Solid Mechanics, ambayo yanasaidia katika teknolojia ya ujenzi wa vitu vikubwa kama madaraja makubwa na maghorofa. Anapoenda Marekani na kuchukua uraia, wengi walimtukana kama msaliti akiwemo baba yake mzazi, lakini mwaka 2020 hii alirudi Uchina pamoja wanafunzi wenye PhD za Solid Mechanics zaidi ya 20.

Watu hawakujua kumbe Prof Gao miaka yake yote 30, alikuwa na malengo mazito mno. Wanafunzi wote aliowafundisha kutoka Uchina alikuwa anawaambia fanyeni kazi kwa bidii lakini msibweteke na kujisahau mkidhania Marekani ni kwenu. Aliwaasa wapate ujuzi na warudi nyumbani. Wengi walirudi nyumbani na ndiyo wameifanya Uchina iwe kama ilivyo leo hii.

Nilisoma kitabu kingine kimeandikwa na Prof Chris Miller, kinaitwa "Chip War: The Fight For the World's Most Critical Technology", ambacho anawaelezea DIASPORA wa Uchina kama Morris Chang ambao walisaidia sana kwenye kuanzisha teknolojia ya SEMI-CONDUCTORS ambayo inategemewa na dunia nzima katika kuendesha karibia teknolojia zote muhimu.

Bwana Morris Chang ni raia wa Marekani lakini alianzisha moja ya kampuni kubwa duniani liitwalo la TSMC, ambalo alilipeleka kwa Taiwan, na kuifanya nchi ile iwe na teknolojia muhimu (Critical Technology) inayohitajika duniani kote, hasa na mataifa makubwa kwasasa. Bila Semi-Conductors huwezi kufanya lolote lile.

Mwingine ni Prof Qian Xuesen (Father of Chinese Rocket Science), mchina ambaye alienda kuishi Marekani miaka ya 1935 na kusoma MIT na kufundisha pia hapo. Akiwa Marekani alifanya CALTECH ambapo baadaye alikuwa ni moja kati ya waanzilishi wakubwa wa maabara ya NASA, Jet Propulsion Laboratory akiwa na wanasayansi wakubwa duniani kama Jack Parsons.

Mwaka 1955, Prof Xuesen alirudi Uchina na kupeleka ujuzi wake ambao ndiyo umeisaidia Uchina kufika hapa. Yeye ndiye aliyeanzisha The Chinese Space Program, na kufanikiwa kubuni kombora la masafa marefu aina ya Dongfeng, pamoja na satelaiti.

Mifano iko mingi sana, na nikisema nianze kuitaja nadhani hatuwezi kumaliza leo na nitatoka kabisa nje ya mada yangu ambayo nategemea kwa msaada wa MUNGU na bila Moderators wenye wivu wa kike kuharibu huu uzi kama wanavyofanya nyuzi zangu nyingine, naweza kuandika kwa kirefu kidogo maana mada hii inagusa sehemu kubwa ya maendeleo ya nchi. Kwasasa, naomba nimalize na huu mfano wa mwisho:

Prof Christopher Andrew, ni mwanazuoni nguli wa histioria, kutoka Cambridge University. Andrew ni mwanahistoria wa shirika la kijasusi la Uingereza, The Secret Intelligence Services (SIS) a.k.a MI6, ambapo kwenye kitabu chake kiitwacho "The Secret World: A History of Intelligence", anaelezea kwamba maendeleo ya Marekani na usalama wake yalichangiwa na diaspora.

Prof Andrew anasema, punde baada ya Marekani kupata uhuru nchi ilikuwa na maadui wengi wenye nguvu mno, kama The British Empire, The Spanish Empire, The Catholic Church na mataifa mengine ya Ulaya ambayo yaliona mapinduzi ya Marekani na mfumo wake wa utawala "Republicanism" ni tishio kwa tawala zao za kifalme, hivyo yalianza kufanya hujuma na uzandiki dhidi ya hili taifa changa.

General George Washington, baada ya kuona kwamba watazidiwa na taifa lao litapotea aliamua kufanya jambo gumu ambalo mpaka leo ndiyo limeisaidia Marekani kuwa taifa kubwa, alitumia DIASPORA. Washington alipitisha bajeti ya ujasusi wa nje kwa usiri mkubwa mno, ambapo asilimia 12% ya GDP ya Marekani ilitumika katika kufanya shughuli za ujasusi nje ya Marekani. Hii ni pesa kubwa mno kwa wale ambao wanaelewa uchumi.

Hizi fedha ndizo zilitumika kwenye shughuli za kuhakikisha wanashawishi mataifa mbalimbali kuitambua Marekani kama taifa huru, kushawishi wataalamu mbalimbali kutokea Ulaya kuhamia Marekani, na kufanya ujasusi wa kiviwanda ambao uliifanya Marekani kuwa taifa lenye teknolojia kubwa duniani.

Hili aliliandika Prof Andrews, linathibitishwa na mtu mwanazuoni mwingine, Prof Doron S. Ben Atar, katika kitabu chake maarufu kiitwacho "Trade Secrets: Intellectual Piracy and Origins of American Industrial Power", ambapo anamzungumzia DIASPORA wa Marekani Francis Cabot Lowell, muhitimu wa Harvard University, ambaye alienda kuishi na kusoma Uingereza mnamo mwaka 1810-1812 na kujifunza TEXTILE INDUSTRY na aliporudi kwao akaanzisha kampuni kubwa liitwalo WALTHAM.

Lowell anavyoondoka nchini Uingereza alipekuliwa sana na majasusi wa Uingereza na hawakukuta kitu kwasababu alikuwa amekariri mifumo yote kichwani kwasababu alikuwa na PHOTOGRAPHIC MEMORY.

Prof, Ben Atar anasema kwamba, waasisi wa Marekani kama Alexander Hamilton walikuwa wanawatia Wamarekani moyo waibe teknolojia kutoka kwa mataifa ya nje na kuilete Marekani, na kutoa amri kwamba watakaoleta teknolojia za wizi kutoka ulaya watapewa zawadi nono.

Majasusi wa uingereza mwaka 1796 baada ya kugundua hili la Industrial Espionage inayofanywa na DIASPORA wa Marekani waliandika hivi kwenye moja ya taarifa zao "Agents hovering like birds of prey on the banks of the Thames, eager in their search for such artisans, mechanics, husbandmen and laborers, as are inclinable to direct their course to America", Marekani alifanikiwa na anafanikiwa mpaka leo kwasababu ya matumizi ya DIASPORA.

SEHEMU YA PILI: SIASA ZA TANZANIA NA DIASPORA

Mwaka 2018, katika vikao vya kamati za bunge zilizokuwa zinafanya mjadala wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, moja ya wageni waalikwa alikuwa ni Mtemi, Mzee Andrew Chenge, aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania tokea mwaka 1993-2005.

Mzee Chenge alianisha moja ya makosa ambayo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania iliwahi kuyafanya na yanaligharimu taifa la Tanzania mpaka leo. Alisema kwamba serikali ya Tanzania ilipoacha kusomesha wanasheria wake Uingereza kama ilivyokuwa inafanya kipindi chote cha utawala wa Mzee Nyerere kimeligharimu taifa, kwenye baadhi ya elimu muhimu na uzoefu mkubwa ambao wanasheria wetu wangeupata kwenye mambo ya msingi.

Majaji wetu wa kwanza nchini Tanzania, kama Mzee Nyalali, Mzee Lugakingira na wenzake walikuwa DIASPORA. Mzee Nyerere alihakikisha kabla hawajakabidhiwa ofisi, vijana wake wanapata elimu na uzoefu bora kutoka kwa mataifa yaliyotangulia.

Majaji wetu wengi walisoma Bachelor of Arts, in Political Science kule Makerere University, na baada ya kuhitimu wakapelekwa Uingereza kusoma Bachelor of Laws, pamoja na kufanya kazi kule kwa muda. Hata wale ambao walisoma UDSM, Mzee Nyerere alihakikisha wanaenda nje kupata mafunzo na uzoefu. Mfano, Jaji Warioba na Jaji Samata.

Mwaka 1977, Tanzania ilianzisha NYUMBU PROJECT chini ya jeshi la Tanzania. NYUMBU PROJECT ilikuwa imejaa wataalamu wetu wazuri tu ambao walikuwa na ujuzi wa hali ya juu. Binafsi niliwahi kuona baadhia ya CV za waanzilishi na nikabaki nashangaa kwamba hawa watanzania mbona sijawahi kuwasikia hata siku.

Mwaka 1985, NYUMBU PROJECT ilibadilishwa na kuwa Tanzania Automative Technology Center (TATC) na mwaka 1993 walienda IKULU na kumuonyesha Raisi Mwinyi, Prototype ya injini ya ndogo ya ndege waliyoibuni ambayo ilifanya kazi vizuri mno na kumfurahisha Mzee Mwinyi.

Moja ya mainjinia waliosaidia kubuni hiyo injini, sitaweza kumtaja kwasababu sina ruhusa yake, lakini ni mtanzania ambaye amewahi kuajiriwa na serikali ya Marekani katika shughuli zake za utengenezaji wa silaha hasahasa magari. Binafsi niliangalia CV yake na nikabaki nashangaa tu, kwanini Tanzania iliacha kutumia DIASPORA kusaidia nchi ?

Ukienda Marekani, Uingereza, Uchina, Ufaransa na Afrika Kusini, utakutana na watanzania wenye utaalamu mkubwa mno, lakini wana kasumba moja tu. HAWAPENDI KABISA KUSIKIA AU KUJIHUSISHA NA TANZANIA. Sababu siyo za kiuchumi bali ni zile za kisiasa.

Mnamo tarehe 20 May 2025, Raisi Samia alizindua SERA YA MAMBO YA NJE ya (Foreign Policy) Tanzania, ambayo inachukua nafasi ya sera iliyotengenezwa mwaka 2001 chini ya Raisi Mkapa. Kuna mambo malengo mengi ambayo yameainishwa ndani ya hii sera, lakini ya msingi sana ni haya:

1. MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA DIPLOMASIA
2. USHIRIKISHWAJI WA DIASPORA KATIKA MAENDELEO YA NCHI

Nashangaa mno, jambo ambalo mataifa ya wenzetu kama Nigeria, Kenya, na Rwanda wamekuwa wakiyafanya tokea miaka ya 80's na 90's, sisi WAJAMAA WA TANZANIA, tunaamka leo na kuanza kuyafanya mwaka 2025 wakati tumeshachelewa mno.

WORLD BANK inatoa ripoti kwamba, mwaka 2023 nchi ya Nigeria ilipokea kiasi cha dola za Kimarekani, Bilioni 19 kutoka kwa Diaspora wake, ambazo ni zaidi ya trilioni 50 za kitanzania, ambayo pia ni sawa na asilimia 6.1% ya GDP ya Nigeria. Hili kitaalamu ndiyo tunaita STRENGTH FROM ABROAD.

Kidiplomasia, siyo rahisi hata kwa Wazungu kuishambulia Nigeria kwasababu mchango wao ni mkubwa kwa mataifa kama Marekani na Uingereza. Binafsi naamini kabisa miaka ijayo, Marekani na Nigeria zitakuwa na viongozi wakubwa tu, wenye asili ya kinaija. Leo hii serikali ya nje haiwezi kuanzisha propaganda dhidi ya Nigeria halafu mambo yakaenda kirahisi tu, AU Serikali ya Raisi TINUBU ikaamua kutesa raia wake bila kuwajibishwa duniani kote.

Majuzi hapa, kama mwezi umepita, serikali ya Ubelgiji imepata joto baada ya DIASPORA wa Rwanda kuwaangua wanasiasa wake kama kipanga. Kuna mwandishi wa habari alikuja kulalamika Twitter/X kwamba wanyarwanda wamekuwa wakimtukana baada ya kukutana naye. Sasa Rwanda ni nchi ndogo mno, lakini inatumia DIASPORA wake vizuri.

Bahati mbaya sana TANZANIA haina DIASPORA wenye nguvu. Kama wana nguvu basi ni maadui wakubwa wa serikali ya CCM. Jambo ambalo ukiliangalia linaweza kuja kuwa na madhara makubwa mno kwa Tanzania huko mbeleni. Serikali haitakiwi kuwa na uhasama na DIASPORA, maana kuna siku itaweza kuwahitaji. Tusipowatumia sisi, watatumiwa na watu wengine hata wale wenye nia ovu na Tanzania.

Hili la kuwaona ni DIASPORA kwamba ni VIBARAKA wasiokuwa na umuhimu litatugharimu. Tuko radhi tuwape ardhi wageni tokea mbali, lakini watanzania wenzetu walioko nje tunaona ni shida na ghasia kuwaruhusu kutumia ardhi katika uwekezaji. Tumekomaa kabisa, NO DUAL CITIZENSHIP: YOU'RE EITHER TANZANIAN or AN ENEMY.

Kuna watanzania wana uraia wa nchi nyingine kwa kigezo cha kutafuta fursam siyo kwamba wanaichukia Tanzania. Wengine wako kwenye nafasi kubwa mno huko duniani. Serikali yetu inabidi ianzishe COMMUNICATION CHANNELS with these DIASPORA, siyo kuwageuza maadui, (A Threat to National Security), jambo ambalo kiukweli limepitwa na wakati.

Kwakuwa serikali imeliona hili tatizo, basi na mimi nitasaidia kutoa mapendekezo yangu ya kisheria na kisera ya jinsi gani tutatekeleza vizuri matumizi ya DIASPORA, na mabadiliko gani inabidi yafanyike kikatiba na kisheria ili tuweze kufikia malengo kama taifa.

Nitaendelea...............
​
 
Serikalini kuna watu wengiwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kutenda. Mimi binafsi naamini hakuna mtu anaichukuia nchi yake moja kwa moja kutokea moyoni kwake. Ukiona mtu anaichukuia nchi yake jua kuna yanayomkwaza.
Diaspora wa nchi ulizotaja feel proud kutokea hizo nchi. Sisi wengiwadiaspora sidhani kama wako proud kivile. Nchi yetu Ina mengi ya kufanya kumfanya diaspora awe proud kurudisha ujuzi au mitaji nyumbani.
Kwa Mimi naona kama la kuuanzia ni uraia pacha pia tutafakari wote kwa kina. Lakini naamini kikubwa ni mentality uraia ni formality maana hata hao wachina Wana uraia wa marekani lakini mawazo Yao kama ulivyosema ni kwao Uchina. Je diaspora wetu wanamawazo na kwetu? Unaweza kuwapa uraia na wasiwaze kwao? Lakini sijasema kama uraia pacha usizingatiwe. Namaanisha si uraia tu yapo mengi.
Tanzania haina tena ushawishi mkubwa kama zamani. Udktari wa WHO tu tunatumia nguvu kubwa sana. Tumeajiri mpka makampuni ya wazungu yatubrand huko duniani tunalipa pesa nyingi lakini nafasi nyingi zinaenda West Africa.
Naamini hta diaspora wetu wakipata nafasi hawajihusishi sana na Tz maana labda hawakupata msada sana ktk mapito yao huko nje.
Tumeona mara nyingi balozi zikilalamikiwa pale ambapo wa Tz wanapata matatizo huko nje.
Pia, Tz isomeshe siyo tu wanasheria kama ulivyosema hapo tunahitaji vijana bright ktk field mbalimbali wakasome nje ya nchi. Siyo tunapeleka watu wa kujiendeleza nooo vijana wakutika A level. Am sure tukipeleka 100 ndani ya miaka 10 lazima watakuwa ktk fields mbali mbali. Mfano mwangalie Fernandez alivyo ni jinsi elimuyawenzetu ilivyomtengeneza. Mtu kama huyu akirudi anarudi na ujuzi na uzoefu.
Nafatilia....
 
Ubalikiwe sana

Lakin wasukuma huwa wana msemo unasema

Kutwimela mboku kumala maswa

Kuganila njibhe kumala membo

Kiranga
 
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI

Katika kusoma kwangu historia ya dunia, hasahasa ya miaka 300 iliyopita sijawahi kuona popote mabadiliko makubwa yamefanyika ndani ya nchi fulani bila msaada wa Diaspora.

Katika miaka 300 iliyopita, mapinduzi makubwa ya kisiasa ambayo ni somo kwa dunia nzima yalifanyika kwenye maeneo yafuatayo, na kote kulikuwa na ushirikishwaji mkubwa wa Diaspora:

1. Mapinduzi ya Marekani 1776-1783.
2. Mapinduzi ya Ufaransa 1789
3. Mapinduzi ya Urusi 1917
4. Mapinduzi ya Uchina 1949
5. Kuzaliwa kwa Israeli 1948

Mpaka leo hii, nchi kama Marekani, Ufaransa, Urusi, Uchina na Israeli zinategemea DIASPORA katika kutekeleza sera zao za mambo ya nje, sera za usalama na sera za kiuchumi. Kiufupi, kama kuna nchi inaamini inaweza kufanya jambo lolote kwenye dunia hii ya leo kwa kutegemea wasomi wa ndani peke yake inajidanganya mno.

Nguvu ya mataifa kama Israeli na Uchina, haipo kwa raia wake wanaoishi ndani bali nje. Leo hii, Israeli imefanikiwa mno kuweza kuinyamazisha dunia dhidi ya yale mauaji inayofanya GAZA kwasababu hakuna nchi kubwa duniani ambayo haina Wayahudi kwenye sehemu nyeti.

Prof John Mearsheimer aliandika kitabu kilichozua taharuki, "The ISRAEL LOBBY & US FOREIGN POLICY", kilichoelezea kwamba ndani ya Marekani kuna kundi lenye nguvu linalohakikisha sera za Marekani zinalinda maslahi ya Israeli. Hili kundi lina taasisi kama AIPAC, World Zionist Congress, ADL, Christians For Israel n.k ambazo huwa zinatumia fedha nyingi kuhakikisha wabunge wa Marekani, vyombo vya habari, taasisi za dini na vyuo vikuu vinakuwa na sera Pro-Israel.

Uchina ndiyo hatari kuliko hata Israeli. Diaspora wa Uchina wako kila sehemu hii dunia. Marekani wamejaa tokea mwaka 1815 ambako waliitwa kama wafanyakazi wa shughuli mbalimbali na wakabaki kule mpaka leo hii. Asia wamejaa kwenye nchi kama Singapore na Malaysia. Hapa Afrika ndiyo usiseme, mpaka sasa inasemekana bara zima limepokea zaidi ya DIASPORA wa kichina Milioni 1.

Kuna kitabu kimeandikwa na Howard W.Frech, kinaitwa "China's Second Continent: How A Million Immigrants Are Building A New Empire in Africa" ameelezea undani wa Diaspora wa kichina na mchango wao kwa maendeleo ya Uchina. Leo hii hakuna taifa la Afrika ambalo linaweza kupanga mkakati mkubwa wa maendeleo na kufanikiwa kuyakwepa makampuni ya kichina, iwe kwenye elimu, ujenzi au mikopo.

Nilikuwa nilikuwa nasikiliza Podcast ya Lex Friedman, akiwa anamhoji afisa wa shirika la ujasusi la Marekani Andrew Bustamente. Alimuuliza ni shirika gani la kijasusi lina nguvu duniani kwasasa, akajibiwa kwamba ni The Ministry of State Security (MSS) a.k.a The Guoanbu ya Uchina. Bustamente alimpa sababu kubwa kwamba, nguvu yake inatokana na DIASPORA wa Uchina waliosambaa duniani kote.

Akakazia na kusema kwamba, raia wa Uchina hata azaliwe Marekani, huwa haachi asili yake, ni lazima ajiite Mchina. Wengi wa hawa DIASPORA ndiyo wanatumiwa na Uchina katika kufanya kazi za ujasusi, uchumi na kiutamaduni. Mfano mzuri tu, Prof Huajian Gao.

Prof Gao alizaliwa Uchina na akaenda kuishi Marekani kwa miaka zaidi ya 30 akisoma Harvard University na kufundisha Stanford University, mambo ya Solid Mechanics, ambayo yanasaidia katika teknolojia ya ujenzi wa vitu vikubwa kama madaraja makubwa na maghorofa. Anapoenda Marekani na kuchukua uraia, wengi walimtukana kama msaliti akiwemo baba yake mzazi, lakini mwaka 2020 hii alirudi Uchina pamoja wanafunzi wenye PhD za Solid Mechanics zaidi ya 20.

Watu hawakujua kumbe Prof Gao miaka yake yote 30, alikuwa na malengo mazito mno. Wanafunzi wote aliowafundisha kutoka Uchina alikuwa anawaambia fanyeni kazi kwa bidii lakini msibweteke na kujisahau mkidhania Marekani ni kwenu. Aliwaasa wapate ujuzi na warudi nyumbani. Wengi walirudi nyumbani na ndiyo wameifanya Uchina iwe kama ilivyo leo hii.

Nilisoma kitabu kingine kimeandikwa na Prof Chris Miller, kinaitwa "Chip War: The Fight For the World's Most Critical Technology", ambacho anawaelezea DIASPORA wa Uchina kama Morris Chang ambao walisaidia sana kwenye kuanzisha teknolojia ya SEMI-CONDUCTORS ambayo inategemewa na dunia nzima katika kuendesha karibia teknolojia zote muhimu.

Bwana Morris Chang ni raia wa Marekani lakini alianzisha moja ya kampuni kubwa duniani liitwalo la TSMC, ambalo alilipeleka kwa Taiwan, na kuifanya nchi ile iwe na teknolojia muhimu (Critical Technology) inayohitajika duniani kote, hasa na mataifa makubwa kwasasa. Bila Semi-Conductors huwezi kufanya lolote lile.

Mwingine ni Prof Qian Xuesen (Father of Chinese Rocket Science), mchina ambaye alienda kuishi Marekani miaka ya 1935 na kusoma MIT na kufundisha pia hapo. Akiwa Marekani alifanya CALTECH ambapo baadaye alikuwa ni moja kati ya waanzilishi wakubwa wa maabara ya NASA, Jet Propulsion Laboratory akiwa na wanasayansi wakubwa duniani kama Jack Parsons.

Mwaka 1955, Prof Xuesen alirudi Uchina na kupeleka ujuzi wake ambao ndiyo umeisaidia Uchina kufika hapa. Yeye ndiye aliyeanzisha The Chinese Space Program, na kufanikiwa kubuni kombora la masafa marefu aina ya Dongfeng, pamoja na satelaiti.

Mifano iko mingi sana, na nikisema nianze kuitaja nadhani hatuwezi kumaliza leo na nitatoka kabisa nje ya mada yangu ambayo nategemea kwa msaada wa MUNGU na bila Moderators wenye wivu wa kike kuharibu huu uzi kama wanavyofanya nyuzi zangu nyingine, naweza kuandika kwa kirefu kidogo maana mada hii inagusa sehemu kubwa ya maendeleo ya nchi. Kwasasa, naomba nimalize na huu mfano wa mwisho:

Prof Christopher Andrew, ni mwanazuoni nguli wa histioria, kutoka Cambridge University. Andrew ni mwanahistoria wa shirika la kijasusi la Uingereza, The Secret Intelligence Services (SIS) a.k.a MI6, ambapo kwenye kitabu chake kiitwacho "The Secret World: A History of Intelligence", anaelezea kwamba maendeleo ya Marekani na usalama wake yalichangiwa na diaspora.

Prof Andrew anasema, punde baada ya Marekani kupata uhuru nchi ilikuwa na maadui wengi wenye nguvu mno, kama The British Empire, The Spanish Empire, The Catholic Church na mataifa mengine ya Ulaya ambayo yaliona mapinduzi ya Marekani na mfumo wake wa utawala "Republicanism" ni tishio kwa tawala zao za kifalme, hivyo yalianza kufanya hujuma na uzandiki dhidi ya hili taifa changa.

General George Washington, baada ya kuona kwamba watazidiwa na taifa lao litapotea aliamua kufanya jambo gumu ambalo mpaka leo ndiyo limeisaidia Marekani kuwa taifa kubwa, alitumia DIASPORA. Washington alipitisha bajeti ya ujasusi wa nje kwa usiri mkubwa mno, ambapo asilimia 12% ya GDP ya Marekani ilitumika katika kufanya shughuli za ujasusi nje ya Marekani. Hii ni pesa kubwa mno kwa wale ambao wanaelewa uchumi.

Hizi fedha ndizo zilitumika kwenye shughuli za kuhakikisha wanashawishi mataifa mbalimbali kuitambua Marekani kama taifa huru, kushawishi wataalamu mbalimbali kutokea Ulaya kuhamia Marekani, na kufanya ujasusi wa kiviwanda ambao uliifanya Marekani kuwa taifa lenye teknolojia kubwa duniani.

Hili aliliandika Prof Andrews, linathibitishwa na mtu mwanazuoni mwingine, Prof Doron S. Ben Atar, katika kitabu chake maarufu kiitwacho "Trade Secrets: Intellectual Piracy and Origins of American Industrial Power", ambapo anamzungumzia DIASPORA wa Marekani Francis Cabot Lowell, muhitimu wa Harvard University, ambaye alienda kuishi na kusoma Uingereza mnamo mwaka 1810-1812 na kujifunza TEXTILE INDUSTRY na aliporudi kwao akaanzisha kampuni kubwa liitwalo WALTHAM.

Lowell anavyoondoka nchini Uingereza alipekuliwa sana na majasusi wa Uingereza na hawakukuta kitu kwasababu alikuwa amekariri mifumo yote kichwani kwasababu alikuwa na PHOTOGRAPHIC MEMORY.

Prof, Ben Atar anasema kwamba, waasisi wa Marekani kama Alexander Hamilton walikuwa wanawatia Wamarekani moyo waibe teknolojia kutoka kwa mataifa ya nje na kuilete Marekani, na kutoa amri kwamba watakaoleta teknolojia za wizi kutoka ulaya watapewa zawadi nono.

Majasusi wa uingereza mwaka 1796 baada ya kugundua hili la Industrial Espionage inayofanywa na DIASPORA wa Marekani waliandika hivi kwenye moja ya taarifa zao "Agents hovering like birds of prey on the banks of the Thames, eager in their search for such artisans, mechanics, husbandmen and laborers, as are inclinable to direct their course to America", Marekani alifanikiwa na anafanikiwa mpaka leo kwasababu ya matumizi ya DIASPORA.

SEHEMU YA PILI: SIASA ZA TANZANIA NA DIASPORA

Mwaka 2018, katika vikao vya kamati za bunge zilizokuwa zinafanya mjadala wa mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, moja ya wageni waalikwa alikuwa ni Mtemi, Mzee Andrew Chenge, aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Tanzania tokea mwaka 1993-2005.

Mzee Chenge alianisha moja ya makosa ambayo ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania iliwahi kuyafanya na yanaligharimu taifa la Tanzania mpaka leo. Alisema kwamba serikali ya Tanzania ilipoacha kusomesha wanasheria wake Uingereza kama ilivyokuwa inafanya kipindi chote cha utawala wa Mzee Nyerere kimeligharimu taifa, kwenye baadhi ya elimu muhimu na uzoefu mkubwa ambao wanasheria wetu wangeupata kwenye mambo ya msingi.

Majaji wetu wa kwanza nchini Tanzania, kama Mzee Nyalali, Mzee Lugakingira na wenzake walikuwa DIASPORA. Mzee Nyerere alihakikisha kabla hawajakabidhiwa ofisi, vijana wake wanapata elimu na uzoefu bora kutoka kwa mataifa yaliyotangulia.

Majaji wetu wengi walisoma Bachelor of Arts, in Political Science kule Makerere University, na baada ya kuhitimu wakapelekwa Uingereza kusoma Bachelor of Laws, pamoja na kufanya kazi kule kwa muda. Hata wale ambao walisoma UDSM, Mzee Nyerere alihakikisha wanaenda nje kupata mafunzo na uzoefu. Mfano, Jaji Warioba na Jaji Samata.

Mwaka 1977, Tanzania ilianzisha NYUMBU PROJECT chini ya jeshi la Tanzania. NYUMBU PROJECT ilikuwa imejaa wataalamu wetu wazuri tu ambao walikuwa na ujuzi wa hali ya juu. Binafsi niliwahi kuona baadhia ya CV za waanzilishi na nikabaki nashangaa kwamba hawa watanzania mbona sijawahi kuwasikia hata siku.

Mwaka 1985, NYUMBU PROJECT ilibadilishwa na kuwa Tanzania Automative Technology Center (TATC) na mwaka 1993 walienda IKULU na kumuonyesha Raisi Mwinyi, Prototype ya injini ya ndogo ya ndege waliyoibuni ambayo ilifanya kazi vizuri mno na kumfurahisha Mzee Mwinyi.

Moja ya mainjinia waliosaidia kubuni hiyo injini, sitaweza kumtaja kwasababu sina ruhusa yake, lakini ni mtanzania ambaye amewahi kuajiriwa na serikali ya Marekani katika shughuli zake za utengenezaji wa silaha hasahasa magari. Binafsi niliangalia CV yake na nikabaki nashangaa tu, kwanini Tanzania iliacha kutumia DIASPORA kusaidia nchi ?

Ukienda Marekani, Uingereza, Uchina, Ufaransa na Afrika Kusini, utakutana na watanzania wenye utaalamu mkubwa mno, lakini wana kasumba moja tu. HAWAPENDI KABISA KUSIKIA AU KUJIHUSISHA NA TANZANIA. Sababu siyo za kiuchumi bali ni zile za kisiasa.

Mnamo tarehe 20 May 2025, Raisi Samia alizindua SERA YA MAMBO YA NJE ya (Foreign Policy) Tanzania, ambayo inachukua nafasi ya sera iliyotengenezwa mwaka 2001 chini ya Raisi Mkapa. Kuna mambo malengo mengi ambayo yameainishwa ndani ya hii sera, lakini ya msingi sana ni haya:

1. MATUMIZI YA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA DIPLOMASIA
2. USHIRIKISHWAJI WA DIASPORA KATIKA MAENDELEO YA NCHI

Nashangaa mno, jambo ambalo mataifa ya wenzetu kama Nigeria, Kenya, na Rwanda wamekuwa wakiyafanya tokea miaka ya 80's na 90's, sisi WAJAMAA WA TANZANIA, tunaamka leo na kuanza kuyafanya mwaka 2025 wakati tumeshachelewa mno.

WORLD BANK inatoa ripoti kwamba, mwaka 2023 nchi ya Nigeria ilipokea kiasi cha dola za Kimarekani, Bilioni 19 kutoka kwa Diaspora wake, ambazo ni zaidi ya trilioni 50 za kitanzania, ambayo pia ni sawa na asilimia 6.1% ya GDP ya Nigeria. Hili kitaalamu ndiyo tunaita STRENGTH FROM ABROAD.

Kidiplomasia, siyo rahisi hata kwa Wazungu kuishambulia Nigeria kwasababu mchango wao ni mkubwa kwa mataifa kama Marekani na Uingereza. Binafsi naamini kabisa miaka ijayo, Marekani na Nigeria zitakuwa na viongozi wakubwa tu, wenye asili ya kinaija. Leo hii serikali ya nje haiwezi kuanzisha propaganda dhidi ya Nigeria halafu mambo yakaenda kirahisi tu, AU Serikali ya Raisi TINUBU ikaamua kutesa raia wake bila kuwajibishwa duniani kote.

Majuzi hapa, kama mwezi umepita, serikali ya Ubelgiji imepata joto baada ya DIASPORA wa Rwanda kuwaangua wanasiasa wake kama kipanga. Kuna mwandishi wa habari alikuja kulalamika Twitter/X kwamba wanyarwanda wamekuwa wakimtukana baada ya kukutana naye. Sasa Rwanda ni nchi ndogo mno, lakini inatumia DIASPORA wake vizuri.

Bahati mbaya sana TANZANIA haina DIASPORA wenye nguvu. Kama wana nguvu basi ni maadui wakubwa wa serikali ya CCM. Jambo ambalo ukiliangalia linaweza kuja kuwa na madhara makubwa mno kwa Tanzania huko mbeleni. Serikali haitakiwi kuwa na uhasama na DIASPORA, maana kuna siku itaweza kuwahitaji. Tusipowatumia sisi, watatumiwa na watu wengine hata wale wenye nia ovu na Tanzania.

Hili la kuwaona ni DIASPORA kwamba ni VIBARAKA wasiokuwa na umuhimu litatugharimu. Tuko radhi tuwape ardhi wageni tokea mbali, lakini watanzania wenzetu walioko nje tunaona ni shida na ghasia kuwaruhusu kutumia ardhi katika uwekezaji. Tumekomaa kabisa, NO DUAL CITIZENSHIP: YOU'RE EITHER TANZANIAN or AN ENEMY.

Kuna watanzania wana uraia wa nchi nyingine kwa kigezo cha kutafuta fursam siyo kwamba wanaichukia Tanzania. Wengine wako kwenye nafasi kubwa mno huko duniani. Serikali yetu inabidi ianzishe COMMUNICATION CHANNELS with these DIASPORA, siyo kuwageuza maadui, (A Threat to National Security), jambo ambalo kiukweli limepitwa na wakati.

Kwakuwa serikali imeliona hili tatizo, basi na mimi nitasaidia kutoa mapendekezo yangu ya kisheria na kisera ya jinsi gani tutatekeleza vizuri matumizi ya DIASPORA, na mabadiliko gani inabidi yafanyike kikatiba na kisheria ili tuweze kufikia malengo kama taifa.

Nitaendelea...............
​
Umesahau kutuletea muendelezo
 
Back
Top Bottom