Songea boys, shule kongwe iliyosahaulika

Songea boys, shule kongwe iliyosahaulika

Shule nyingi zilikua na haya magari
Nimekumbuka aina ya gari hiyo tulikuwa nayo pale Iyunga Technical secondary School miaka ya 96 tukianza form one tuliikuta na kuitumia. Shule za Serikali zilizokuwa na gari hizo ni Chache Sana enzi zile.
 
Hizi shule karibia zote zilifanyiwa ukarabati...

Imekuaje hio ikasahaulika,, Shule niliyosoma miaka hio Kwiro boys nilipata taarifa imekarabatiwa inapendeza japo ni kitambo kirefu sana sijaiona...

Jengeni kwanza familia zenu,, hio shule ni jukumu la serikali... ila ikiwapendeza mkaiweke sawa tu
Unamjua Dickson Chiduo?
 
Hivi hawa songea girls kwann tulkua tunawaita TAMSALA
Jina TAMSALA, kwa historia niliyoipata nikiwa Box 2, limetokana na ufupisho wa shule za sekondari walipotolewa wanafunzi wa kwanza wa shule hiyo ilipoanzishwa/ilipoanzisha kidato cha tano na sita. Yaani, wakati uanzishwaji huo ukifanyika, wanafunzi walitolewa kutoka shule mbalimbali ili kuletwa pale Songea Girls. Kwenye TAMSALA kuna Tabora Girls, Msalato na Loleza.
 
Kwanini msianzishe page yenu ya WhatsApp ili nyie Allumn muisaidie shule yenu, hususan ujenzi wa vyoo ambavyo ni vya shimo na vimechoka Sana!
 
Wazee wa "vyamafuta na mayao" dom langu lilikuwa whitehouse karibu na "ulokoni"! nawakumbuka walimu wangu babu wa mats(rip) na maps wa chem(rip) walikuwa wazee wa tungi hatari! bila kumsahau teacher deo wa adv phyz!
 
Back
Top Bottom