Post #15 ndiyo jibu, enyi viumbe msiosikie wala kutaka kuelewa.....wakaidi.
Tusipoukubali ukweli huo zitashuka nyuzi humo za kuponda kila sehemu (ingawa najua kusini ndo wahanga no.1 wa hili......huwa wanapondwa mpaka na watu wanaotoka kwenye kata zilizosheni vibanda vilivyoezekwa na kinyesi cha ng'ombe, tena ndo wengi hao hatari. Nimemuona mmoja keshajitokeza hapo juu anasema yeye hata siku moja tu imemshinda kuishi lindi na hivyo yuko njiani anaelekea sehemu nyingine. Hahahahahaha, hongera yake!)
Haya, huyo mdau wa post hiyo alichoshwa na mbeya baada ya kukuta mambo tofauti na alivyokuwa anafikiria (bila shaka mitandaoni kama hivi). Sasa kutabaki wapi tena kusikopondwa ikiwa hata tunalojivunia kuwa ni jiji lina hali hiyo.
Kwa Tanzania hii, NJE YA DAR, sijaona tu sehemu yenye hadhi ya kutosha kuponda sehemu nyingine. Tunahangaika tu. Tuhamasishane kufanya kazi labda tutaendelea huko mbele....watoto, vijana, watu wazima na wazee kutoka pande zote za nchi hii, kila siku, wanakimbilia au wanaitamani dar.