Songea: Sita jela miaka 50 kwa kutaka kuipindua Serikali ya Tanzania ili kuanzisha Taifa la Kiislamu

Songea: Sita jela miaka 50 kwa kutaka kuipindua Serikali ya Tanzania ili kuanzisha Taifa la Kiislamu

Polisi hawakosei
Fika Kibiti utaelewa
Acha tu..jamaa kituo chao kilikua moja ya misikiti hapo ikwiriri ndio walikua wakipata mafunzo na kuhifadhi silaha.

Ila walipoteza aseee..sahivi hali shwari na watu bado wapo kazini..hii nchi inalindwa asee.

Hao wapuuzi ukiwachekea wanajijenga wanapata nguvu na ufadhiri mwisho wasikua wanakua tatizo..hao niwakuwamaliza kimya kimya.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sita jela miaka 50 kwa kutaka kuipindua Serikali ya Tanzania

Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Dk. Yose Mlyambina kwenye Masijala Ndogo ya Songea.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Seif Chombo, Abdallah Chombo, Mohamed Kamala, Athumani Chombo, Omary Mbonani na Rashidi Ally.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Yose alisema washtakiwa wanatuhumiwa kati ya Januari Mosi 2014 na Julai 13, 2020, kwenye maeneo tofauti wilayani Tunduru mkoani Ruvuma na maeneo mengine nchini, kwa pamoja walikula njama ya kufanya ugaidi.

Wanadaiwa kula njama kuanzisha vita ya kidini vijulikanavyo Jihad na kuwashawishi vijana kuongeza nguvu kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanzisha Taifa la Kiislamu kwa kutumia nguvu na machafuko.

Alisema malengo yalikuwa kuongoza kwa kutumia sheria za Kiislamu, washtakiwa walipekelekwa nchi mbalimbali zenye uongozi wa Kiislamu kwa ajili ya mafunzo zaidi ya Jihad kinyume cha sheria na taratibu za Jamhuri Muungano wa Tanzania.

"Kitendo hicho hakihatarishi tu maisha ya watu wengine, bali hata wao wenyewe, ni hatari kwa maisha yao, " alisema Jaji Yose.

Washtakiwa walifikishwa mahakamani kwa makosa mawili ya kula njama kufanya ugaidi na kushiriki vikao vya kufanya ugaidi.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kwenye Kijiji cha Lumbukule na maeneo mengine wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ilidaiwa mahakamani huko kuwa washtakiwa kwa pamoja na wengine ambao hawakuwapo mahakamani, walishiriki kufanya kikao kinachohusiana na masuala ya ugaidi, kula njama ya kutaka kuanzisha Serikali ya Kiislamu kwa kutumia nguvu kwa malengo ya kuvuruga mfumo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo, lakini walikiri kukamatwa na waliposomewa hoja za awali, walizikana isipokuwa majina yao, wakazi wa Lukumbule, walikubali kwamba walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi na kwamba wanaujua msikiti wa Al Malidi na wanaishi kwenye kijiji hicho tangu mwaka 2017 mpaka 2020.

Katika kesi hiyo, Jamhuri iliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hebel Kihaka aliyesaidiana na Tulimanywa Majigo na Edgar Bantilaki.

Washtakiwa walikuwa wakiwakilishwa na Mawakili Naomi John, Nestory Nyoni Rafael Matola, Alex Nyoni, Razaro Simba na Denis Razaro.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne na vielelezo vitano.

Washtakiwa walijitetea wenyewe kwa kiapo na hakuna aliyekuwa na kielelezo chochote.

Miongoni mwa ushahidi uliotolewa ni kwamba serikali iliharibu kambi yao maeneo ya Lukumbule, Tunduru maeneo ya Magazini, Nanyumbu, Ntamba Swala mpakani mwa Msumbuji, Tandahimba, Newala na Masasi na Mtwara.

Ushahidi ulidai malengo ya washtakiwa yalikuwa uamuzi wote ufanyike chini ya misingi ya Quran Tukufu.

Inadaiwa viongozi wao wanaishi Ruvuma, Lindi, Mtwara na Pwani na kwamba viongozi wachache walikamatwa huku wengine wakifanikiwa kukimbilia Msumbiji.

Pia ilidaiwa wahalifu hao waliua na kuharibu vijiji ambavyo viligoma kuungana nao, walichukua mali za watu zikiwamo fedha na kuharibu mali zisizohamishika.

Hata hivyo, washtakiwa wakati wa utetezi walikana kuhusika kufanya matukio hayo.

Mahakama baada ya kusikiliza shauri hilo, ilijiridhisha kwamba upande wa Jamhuri umeweza kuthibitisha makosa dhidi ya washtakiwa bila kuacha shaka.

"Mahakama ilijiridhisha kuwa washtakiwa wote walikula njama kutaka kuipindua serikali iliyoko madarakani na walipata mafunzo.

"Kutokana na ushahidi ulioko, mahakama ilizingatia maombi ya washtakiwa kupunguziwa adhabu lakini kutokana na makosa waliyotenda, mahakama inawatia hatiani na kuwapa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 20 kwa kosa la kwanza na miaka 30 kwa kosa la pili, adhabu zote zinakwenda kwa pamoja," alisema Jaji.

Mahakama iliwapa haki yao ya msingi kama hawakubaliani na adhabu wanaruhusiwa kukata rufani.

Chanzo: Nipashe
Kumbe jihad ni ugaid?
Mie nilikua sijui.
Kuna mtu alinidanganya nilipokuwa mdogo kwamba jihad ni vita takatifu ya kumpigania mungu.
 
Kumbe jihad ni ugaid?
Mie nilikua sijui.
Kuna mtu alinidanganya nilipokuwa mdogo kwamba jihad ni vita takatifu ya kumpigania mungu.

Hata kuiba kura ni ugaidi mkubwa
 
Sehemu wakijaa waislamu halafu wakawa wajinga yani hawana elimu..tarajia ma upumafu kama haya..acha wapate chamoto wameua sana askari na raia rufuji na kibiti na mpakani mwa mto ruvuma.

Kwa Intel iliyopo kila muhusika lazima akamatwe.

#MaendeleoHayanaChama
Chuki yako dhidi ya waislam ni dhahiri,pole Sana kijana,mpaka uingie kaburini kafiri wewe moyo utakua umechakaa Sana kwa chuki
 
Chuki yako dhidi ya waislam ni dhahiri,pole Sana kijana,mpaka uingie kaburini kafiri wewe moyo utakua umechakaa Sana kwa chuki
Kwani wewe hutaingia kaburini...acheni ugaidi hii dunia ni yetu sote tuishi kwa amani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sema nn wangekinukisha tu kwaNza maana nchi hii raia hatuthaminiwi kabSa

Kinukishe ndani ya familia yenu. Uko hapa unaandika Ni kwa kuwa kuna Wanaume na wanawake wanafanya kazi. Hapa tulipo bado tunakula na kinywa hata kama ni Ulanzi. Vita na fujo haviwezi kutupa hali hiyo. So hamia Somalia mkuu.
 
Mnakimbia Katiba nilikwenda huko Hao vijana wanataka demokrasia ya kweli nyinyi mnawapiga na kuwabambikizia kesi. Wekeni katiba mpya msilete upuuzi
Waambie Waunde chama cha upinzani ili wadai hiyo katiba katika mfumo sahihi.
Katiba haidaiwi msituni kwa Ufadhiri wa Nchi za Kiarabu ambazo wana wauwa watu kila siku kwa kudai haki zao.

Haki ya Katiba wangeruhusu IRAN kwanza.
Wafadhiri wakubwa wa UGAIDI.

Mwezi wa kwanza narudi Jeshini, na nataka niende kwenye kitengo cha Ugaidi.
Nitawachinja hadi wanye
 
Eeeeeh WATALEBAN Tena!yaani hiyo serikali yao Ni amri moja
 
Ulitaka kila jambo uletewe habari hapo kwenye kijiwe chako cha kahawa?

#MaendeleoHayanaChama
sasa habari kubwa kama hizo zinaendaje kimya kimya kama sio hila za makafir?

kama ni hivo wangewahukumu kimya kimya hivo hivo sasa
 
Back
Top Bottom