Ijumaa, 25 Novemba 2022
JAJI KIONGOZI AWATAKA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUHAKIKI TAARIFA ZA MAHAKAMA
· Azitaka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Mahakama kuwasilianaNa Lydia Churi-Tume ya Utumishi wa Mahakama, Simiyu
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Mustapher Siyani ametoa rai kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhariri na kuhakiki taarifa zinazohusu Mhimili wa Mahakama kabla hazijawafikia wananchi ili kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama.
Akizungumza na wadau wa utoaji haki jana mkoani Simiyu, Jaji Kionggozi amesema wahariri wana nafasi kubwa ya kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama lakini pia wanayo nafasi kubwa ya kuvunja au kubomoa imani hiyo kwa chombo chao.
“Matarajio ya Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mahakama ya Tanzania ni kuona wahariri wanatambua kuwa wao ni wadau muhimu hivyo watambue wajibu wao wa kuhakikisha habari zinazotolewa kuhusu Mahakama zinahaririwa na kuhakikiwa vizuri na habari hizo ni za kweli na siyo za upande moja”, alisema.
Alisema hakuna mtu au chombo chochote kile kinachoweza kuaminika kutoa haki kama pande mbili za mgogoro hazina imani na mtu au chombo hicho”, alisema Jaji Kiongozi.
Alisema habari zikiandikwa kishabiki au zikatengenezewa vichwa vya habari vyenye kusudio la kuvuta watu wazisome au kuzisikiliza kwa makusudio yoyote yale zinaweza kuupotosha Umma na kuondoa imani iliyonayo kwa Mahakama.
“Endapo wananchi watakosa Imani na Mahakama hawataitumia kutafuta haki, na Imani kwa Mahakama ndiyo msingi wa haki hivyo uwezekano wa wananchi kujichukulia sheria mkononi utakuwa ni mkubwa”, alisisitiza.
Jaji Kiongozi alisema kila Mdau wa Mahakama anao wajibu wa kuhakikisha vyombo vya Serikali ikiwemo Mahakama vinafanya kazi iliyokusudiwa. Aliongeza kuwa Tume na Mahakama pia inatarajia kuwa wahariri watashiriki katika maboresho yanayoendelea yenye lengo la kujenga na kukuza Imani ya wananchi kwa Mahakama kupitia habari zinazotolewa na vyombo vyao bila kuathiri wajibu na msingi wa kazi ya uandishi wa habari wa kuelimisha, kuhabarisha, kukosoa, kufichua na hata kuburudisha.
MwanaJF, soma hukumu nzima ya kurasa 100 upate undani wa case hii ilivyounguruma uielewe :
Court name
High Court of Tanzania
Registry
High Court Songea Registry
Case number
Economic Case 4 of 2022
Republic vs Seif Abdallah Chombo and 5 Others (Economic Case 4 of 2022) [2022] TZHC 15198 (16 December 2022);
Media neutral citation
[2022] TZHC 1519
Soma kwa urefu kurasa zote 100 :
Source : Republic vs Seif Abdallah Chombo and 5 Others (Economic Case 4 of 2022) [2022] TZHC 15198 (16 December 2022); | Tanzlii