Songea: Waumini wachoma Kanisa kwa hasira baada ya Padre kukataa kwenda kumzika muumini

Haulazimishwi kuwa Mkatoliki, na unaruhusiwa kuondoka muda wowote unapoona imani yako haifungamani na imani yetu.
Hivi wewe unajuwa imani ni nini? Unaweza kuniambia kwenye kanuni ya imani kuna huo upuuzi wenu?

Hawa mapadre wanaozaa mitaani na kulawiti vitoto vidogo wewe ndio unaona wako sahihi kwa kila jambo?

Tunawastahi tu wasipobadirika na makofi watayakoga.
 
Kwahiyo shida ni kutokuwa tayari kwako kuwajibika!!?

Ili uzikwe Kikatoliki kuna vigezo na masharti ya kuzingatia. Unaposhindwa it means haustahili.

Kama ambavyo wao hawakulazimishi kufuata sheria zao, na wewe usiwalazimishe wakuzike.

Kila mmoja ashinde mechi za

Kwahiyo shida ni kutokuwa tayari kwako kuwajibika!!?

Ili uzikwe Kikatoliki kuna vigezo na masharti ya kuzingatia. Unaposhindwa it means haustahili.

Kama ambavyo wao hawakulazimishi kufuata sheria zao, na wewe usiwalazimishe wakuzike.

Kila mmoja ashinde mechi zake.
Nilishatoka kwenye huo utumwa wa dini, kwani mtu akizikwa na padri ndio anakwenda mbinguni?
 
wamekosea sana kuchoma nyumba ya ibada.
maana hiyo sio nyumba ya Padre.
Ni kosa kujichukulia sheria mkononi.
ni bora wangemtenga Padre kwa kususia kwenda kanisani badala ya kuchoma.
Si walijenga wenyewe.Kwani alijenga Padre? Wamechoma jengo lao

Huyo aliyekataa kumzika yawezekana sabai kubwa alikuwa hatoi sadaka
 
Hivi wewe unajuwa imani ni nini? Unaweza kuniambia kwenye kanuni ya imani kuna huo upuuzi wenu?

Hawa mapadre wanaozaa mitaani na kulawiti vitoto vidogo wewe ndio unaona wako sahihi kwa kila jambo?

Tunawastahi tu wasipobadirika na makofi watayakoga.
Nina wasiwasi hata kama kweli unajua maana ya imani.

Waamini wanaozaa nje ya viapo vyao ni wengi tu, siyo makasisi pekee.

Ungeonekana muungwana kama ungekemea uovu wa kuzaa nje ya ndoa na vitendo vichafu kama kulawiti kwa Kanisa zima.

Acha unafiki.
 
Kristu unamsoma kwenye Qur'an
Sijui kuhusu Quran (na sihitaji kujua). Nijuacho ni kuwa kuna Ukristu bila Biblia lakini hakuna Ukristu bila Kristu.

Hebu tuthibitishie Ukristu kwa kutumia Biblia bila Kristu.
 
Ushahidi wa mazingira unaonesha hivyo, mtu mshenzi hawezi kutetewa kihivyo na umma.
Ishu ipo hivi..
Marehemu alizaa na mume w mtu... Lakini alikuwa anashiriki jumuiya. Wakati huo alikuwa anaishi kwake..!! Sasa kwa bahati mbaya akafariki. Ndugu wa marehemu wakajaza form za kuomba huduma ya mazishi, lakini hawakutamka juu ya yeye kuzaa na mume wa mtu. Wakapewa michango inayotakiwa kutolewa na mwisho wakapewa utaratibu wa mazishi.

Sasa ikatokea, mtu mmoja toka kwenye jumuiya yao, akaenda kwenye uongozi wa juu wa parokia na kutoa taarifa ya kwamba marehemu amezaa na mume wa mtu. Baadhi ya ndugu wakapewa taarifa hiyo na kwamba hakuna atakayetoka kanisani kwenda kuongoza ibada ya mazishi. Na fedha zikarudishwa. Bahati mbaya haya yanatokea kukiwa kumebaki muda mfupi sana muda wa mazishi ufike. Na wale ndugu waliopewa taarifa hawakulisema hilo, na wala hawakusema kwamba wamerudishowa fedha.

Wahudhuriaji wa msiba wakaamua kwenda wenyewe na walipotoka mazikoni, wakapitia parokiani na kuweka magogo mlango mkuu wa kanisa na geti la kuingilia nyumba ya padre.

Wakasema ndani asitoke mtu na atakayetoka wanamfanyia jambo baya. Kwa bahati nzuri, baada ya wao kumtafuta dereva na kumkosa, ilionekana alikuwa Songea mjini pamoja na paroko.

UZURI HAWAKUCHOMA MOTO KANISA KAMA INAVYORIPOTIWA

Sikiliza hii audio clip hapa chini
 
Attachments

Nina wasiwasi hata kama kweli unajua maana ya imani.

Waamini wanaozaa nje ya viapo vyao ni wengi tu, siyo makasisi pekee.

Ungeonekana muungwana kama ungekemea uovu wa kuzaa nje ya ndoa na vitendo vichafu kama kulawiti kwa Kanisa zima.

Acha unafiki.
Unajuwa wewe unajichanganya mwenyewe, hapa tunakemea tabia mbaya ya hao viongozi wa kiroho kukataa kutowa huduma za kiroho then wewe unatetea halafu unanifundisha jinsi ya kukemea?

Wakati Vaticano walikuwa wakiamini Juwa linaizunguka dunia, Galileo aliwapa fact Vaticano kwamba Dunia ndio inalizunguka juwa, kanisa lilimpinga na kumtenga na kuteswa sana, laakini baadaye scientifically proof ikaja kuthibitika Galileo alikuwa sahihi na alikuwa amedhafariki, kanisa alikupata nafasi ya kumuomba radhi Galileo.

Sasa na wewe acha kuwa mtumwa wa kifikra kwa vitu unaona siyo sahihi lakini bado unaunga mkono ni ujinga uliotukuka.

Mungu amempa kila binadamu akili ila kuzitumia ni utashi wako mwenyewe.
 
Ishu ipo hivi..
Marehemu alizaa na mume w mtu... Lakini alikuwa anashiriki jumuiya. Wakati huo alikuwa anaishi kwake..!! Sasa kwa bahati mbaya akafariki. Ndugu wa marehemu wakajaza form za kuomba huduma ya mazishi, lakini hawakutamka juu ya yeye kuzaa na mume wa mtu. Wakapewa michango inayotakiwa kutolewa na mwisho wakapewa utaratibu wa mazishi.

Sasa ikatokea, mtu mmoja toka kwenye jumuiya yao, akaenda kwenye uongozi wa juu wa parokia na kutoa taarifa ya kwamba marehemu amezaa na mume wa mtu. Baadhi ya ndugu wakapewa taarifa hiyo na kwamba hakuna atakayetoka kanisani kwenda kuongoza ibada ya mazishi. Na fedha zikarudishwa. Bahati mbaya haya yanatokea kukiwa kumebaki muda mfupi sana muda wa mazishi ufike. Na wale ndugu waliopewa taarifa hawakulisema hilo, na wala hawakusema kwamba wamerudishowa fedha.

Wahudhuriaji wa msiba wakaamua kwenda wenyewe na walipotoka mazikoni, wakapitia parokiani na kuweka magogo mlango mkuu wa kanisa na geti la kuingilia nyumba ya padre.

Wakasema ndani asitoke mtu na atakayetoka wanamfanyia jambo baya. Kwa bahati nzuri, baada ya wao kumtafuta dereva na kumkosa, ilionekana alikuwa Songea mjini pamoja na paroko.

UZURI HAWAKUCHOMA MOTO KANISA KAMA INAVYORIPOTIWA
Ni ujinga mtupu, hakuna sababu yoyote ya kumnyima huduma za kiroho hapo, hilo ni swala la marehemu na Mungu wake.

Halafu makanisa ya katoliki kuna vitubio, kama huyu bibie ametubu dhambi zake na Mungu amemsamehe hawa binadamu dhaifu wao ni nani?

Tukemee kwa nguvu zote tabia hizi za kihuni.
 
Unaweza ukalitazama kwa namna hiyo, lakini kanisa lina taratibu zake... Hata sisi tulio wazima tunajuwa ukifanya hivi, kinatokea kile... Umefanya na wao wakafanya then unalalamika..!!
 
Tunaita dini kimazoea tu, Ukristo siyo dini.
Ukristo ni IMANI.
Kumkiri na kufuata matendo ya Kristo unakuwa tayari ni mfuasi wa Kristo. (MKRISTO) mean mfuasi wa Kristo.
 
Ivo ivo!!! Tuliwahu kujibiwa nyodo na padri mmoja tulipokwenda kuomba misa ya kumzika jirani yetu, na ni hapa hapa mjini daslam! , Hakuishia hapo alipiga marufuku yoyote kuongoza misa hiyo, akapiga marufuku hadi viongozi wa jumuiya kujishugulisha na msiba huo , yani viti meza , vyombo vya jumuia vilioigwa marufuku kutumika kwemye msiba huo kwa maelekezo kutoka kanisani , then wakawekwa mamluki msibani kuhakikisha maelekezo hayo yanatekelezwa na mtua anayeyakiuka!!

Jirani ilibidi azikwe na misa ya kilokole.
Nina uzoefu nao.
 
Yeah thats how they operate! Yani kanisa limeajiri chawa kwa ajili ya kupeleka maneno ya umbea wa waumini kwa mapadre, huku nilipo kuna jamaa alikua muumini mzuri tu na michango anatoa , ila alipata bahati mbaya ya kufiwa na mke wake , huku na kule akaamua kuvuta mke mpya wa kiislam , umbea ukafika kwa baba paroko, siku alipofariki kanisa halikujigusa
Sisi tulimsamehe yeye anaona yupo sahihi, wakati anakula kimasihara Ndugu yetu wa kike, na baada ya kuzika tuliomba misa za kumuombea marehemu kila siku asubuhi na pesa walipokea na akawa anasalisha kila tunapoenda.
 
Hao waumini akili haina akili
kabisa.Unachoma.moto kanisa!!.Sasa subiri pigo takatifu.Nyumba ya ibada siyo ya kuchezea.
 
Unajuwa wewe unajichanganya mwenyewe, hapa tunakemea tabia mbaya ya hao viongozi wa kiroho kukataa kutowa huduma za kiroho then wewe unatetea halafu unanifundisha jinsi ya kukemea?

Wakati Vaticano walikuwa wakiamini Juwa linaizunguka dunia, Galileo aliwapa fact Vaticano kwamba Dunia ndio inalizunguka juwa, kanisa lilimpinga na kumtenga na kuteswa sana, laakini baadaye scientifically proof ikaja kuthibitika Galileo alikuwa sahihi na alikuwa amedhafariki, kanisa alikupata nafasi ya kumuomba radhi Galileo.

Sasa na wewe acha kuwa mtumwa wa kifikra kwa vitu unaona siyo sahihi lakini bado unaunga mkono ni ujinga uliotukuka.

Mungu amempa kila binadamu akili ila kuzitumia ni utashi wako mwenyewe.
Watu mnaokemea uzinzi wa makasisi na wakati nyie wenyewe na watu wenu wa karibu ni wazinzi wa kutupwa na hamjali wala kukemeana ni wanafiki wa kiwango cha juu.

Kushiriki tendo la ndoa nje ya ndoa na nje ya utaratibu ni dhambi inayopaswa kukemewa kwa nguvu zote bila kujali imetendwa na waliopo kwenye ndoa au nje ya ndoa. Acha unafiki wako.

Viongozi wa kiroho hawajakataa kutoa huduma za kiroho, lakini kuna haja gani kumpa huduma za kiroho marehemu ambaye wakati wa uhai wake hakuzihitaji?

Kwahiyo wewe ni Galileo? Kuacha kumzika mtu ambaye aliukana Ukatoliki na hakutaka kuuishi enzi za uhai wake ni scientific fact? Unaelewa hata maana ya sayansi?

Unajiaibisha.
 
Back
Top Bottom