Songwe: Baba agoma kupeleka mwanaye kidato cha kwanza akidai hana akili na Shuleni Wanafunzi wanachapwa sana viboko

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mzazi mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga, kata ya Mlale, iliyopo wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe, amegoma kumpeleka mwanaye kujiunga na kidato cha kwanza akidai kuwa mwanaye hana akili na kwamba watoto wamekuwa wakichapwa tu wanapokuwa shuleni.

Mzazi huyo anayejulikana kwa jina la Anania Mdolo, ameyabainisha hayo wakati wa ziara ya mkuu wa wilaya ya Ileje, Joseph Mkude, akiwa katika operesheni ya kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanaripoti shuleni na ndipo alipobaini uwepo wa mtoto Happy Mdolo, aliyetakiwa kuripoti shule ya sekondari Mlele, akigomewa kuendelea na masomo na baba yake mzazi.

Awali akizungumza na kueleza sababu ya kuacha kumpeleka mwanaye shule, Mzee Mdolo, alidai kuwa sababu kubwa ni kwamba mwanaye hana akili za kuendelea na masomo.

"Nina watoto 9, Happy haaenda kujiunga na kidato cha kwanza niliona akili yake haifai kuendelea na masomo, alama zake ni ndogo alipata wastani wa C, shuleni watoto ni kuchapwa viboko tu kila siku wakati hana akili, akianza kuchapwa viboko kila siku mtanisaidiaje?", amesema mzazi huyo.

Licha ya vuta ni kuvute kati ya mkuu wa wilaya na mzazi huyo, hatimaye mkuu huyo wa wilaya akampa fomu ya maelekezo na mahitaji yote ya mtoto, huku akimtaka mzazi huyo kumpeleka mtoto shule mara moja.
 
Nina watoto 9, Happy haaenda kujiunga na kidato cha kwanza niliona akili yake haifai kuendelea na masomo, alama zake ni ndogo alipata wastani wa C, shuleni watoto ni kuchapwa viboko tu kila siku wakati hana akili, akianza kuchapwa viboko kila siku mtanisaidiaje?", amesema mzazi huyo
Kuna Logic kubwa sana! Angepelekwa hata VETA akajifunze painting, tailoring, etc. Sijui kwanini mfumo wetu uko hivi!
 
Hapana! Sio kweli
Ebu sema mfumo upi na unaweza chukua mda gan, mm nimesoma Arusha technical college, CNC machine moja,ya milling au lathe machine ya training in Tsh 300+ , we unahis n rahis kuweka system mpya haswa hiyo wanayosugest watu ya vyuo vya ufund it can take more than ten years, believe me or not
 
Huyo mzazi huenda kutokujua lakini alipaswa kuadhibiwa sababu sheria inasema kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne hiyo ni elimu ya msingi hivyo kila mtanzania ana wajibu wa kupata pasipo na kikwazo chochote kile.
 
Ebu sema mfumo upi na unaweza chukua mda gan, mm nimesoma Arusha technical college, CNC machine moja,ya milling au lathe machine ya training in Tsh 300+ , we unahis n rahis kuweka system mpya haswa hiyo wanayosugest watu ya vyuo vya ufund it can take more than ten years, believe me or not
Sijaelewa concern yako labda, maana vyuo si vipi tayari miaka na miaka? Achana na technical schools. Kuna Community Colleges na Rural Development Colleges (nadhani zinaitwa hivi), zipo zinatoa kozi za stadi za moja kwa moja! Kuna baadhi vimeshakufa na ndio hivyo hasa nilikua namaanisha including VETA. Yaani isiwe ni lazima kwenda secondary..... Nadhani tumeelewana
 
Vipo vingap🤔, na wahitm STD 7 wapo wangap🤔, Kama secondary tuu mwaka huu zimetapika madogo wa 4m 1 we unahis hzo zitaweza fikia hata 1/10 ya watakaotakiwa kwenda huko?
 
Sera mpya ya Elimu ya kuifanya Elimu ya Msingi kuwa ni Kidato cha nne, haina tija yoyote ile zaidi tu ya kuwapotezea muda watoto!

Haiwezekani mwanafunzi alazimishwe kukariri masomo yasiyo msaidia chochote kwa miaka 4 halafu anaishia tu kupata division zero!

Na wakati mtoto huyo huyo angepelekwa kwenye kipaji alicho bobea mfano uimbaji, ufundi, michezo, tehama, ubunifu, ujasiriamali, sanaa, nk. Angeweza kufanya mambo makubwa na yenye manufaa zaidi kwake, kwa jamii yake na pia kwa Taifa!

Ila kwa sababu ya sera za Wasomi wetu, zimewafanya hao watoto wanaoshindwa kukariri hayo masomo ya msingi na sekondari na hivyo kufeli mitihani, waonekane kuwa hawana akili! Jambo ambalo siyo sahihi kabisa! Na mbaya zaidi na jamii nayo akiwemo huyo mzazi, imeingia kwenye mtego wa kuamini hivyo.

Kuna ulazima
 
ikipewa kipaumbele hakuna kinachoshindikana ikiwa kila leo zinakuja streamliner mkuu
Ebu sema mfumo upi na unaweza chukua mda gan, mm nimesoma Arusha technical college, CNC machine moja,ya milling au lathe machine ya training in Tsh 300+ , we unahis n rahis kuweka system mpya haswa hiyo wanayosugest watu ya vyuo vya ufund it can take more than ten years, believe me or not
 
Kuna Logic kubwa sana! Angepelekwa hata VETA akajifunze painting, tailoring, etc. Sijui kwanini mfumo wetu uko hivi!
Unafahamu huo umri aliomaliza nao?? Fikilia awe amemaliza std 7 na miaka 13, huyu ataweza kusukuma chelehani au anaweza kubeba tofali au kusukuma landa au msumeno?? Watoto wanamaliza na umri mdogo saanaa. Na hili suala wizala ya elimu walitizame upyaa.
 
Sera mpya ya Elimu ya kuifanya Elimu ya Msingi kuwa ni Kidato cha nne, haina tija yoyote ile zaidi tu ya kuwapotezea muda watoto!

Haiwezekani mwanafunzi alazimishwe kukariri masomo yasiyo msaidia chochote kwa miaka 4 halafu anaishia tu kupata division zero!

Na wakati mtoto huyo huyo angepelekwa kwenye kipaji alicho bobea mfano uimbaji, ufundi, michezo, tehama, ubunifu, ujasiriamali, sanaa, nk. Angeweza kufanya mambo makubwa na yenye manufaa zaidi kwake, kwa jamii yake na pia kwa Taifa!

Ila kwa sababu ya sera za Wasomi wetu, zimewafanya hao watoto wanaoshindwa kukariri hayo masomo ya msingi na sekondari na hivyo kufeli mitihani, waonekane kuwa hawana akili! Jambo ambalo siyo sahihi kabisa! Na mbaya zaidi na jamii nayo akiwemo huyo mzazi, imeingia kwenye mtego wa kuamini hivyo.

Kuna ulazima
Acheni kukurupuka kwa kuiga mambo ya mabeberu na kutaka na sisi tuwafuate. Hayo unayoyadai hayafai kabisa hapa kwetu Africa . na hakuna ata nchi moja ya Africa inayoweza kuadapt hiyo miongozo.
 
Akishasema bosi wenu, hata kama ni ujinga! Basi ni lazima muunge mkono! Unataka uniambie Watanzania wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali mfano michezo, sanaa, uimbaji, ufundi, nk wamesoma mpaka kidato cha nne na kuendelea?

Au hayo mafanikio yao yametokana na hii elimu yetu ya kukaririshana? Mbona nyinyi watu ni wakaidi sana? Au mna ajenda yenu ya siri ya kutaka kuendelea kuwatawala Watanzania kupitia mfumo wenu mbovu wa elimu?
 
Watu wengi ktk jamii wameamua kuamini kuwa waalimu ndo wanafelisha..na hali watoto hawana uwezo wa kuhimili masomo..tukumbuke masomo ya sekondari sy kukariri tu bali..yanahitaj na akili ya kujenga hoja pia.. huyo mzaz yuko sahihi sana..hongera mzazi..simamia msimamo wako
 
Akishasema bosi wenu, hata kama ni ujinga! Basi ni lazima muunge mkono! Unataka uniambie Watanzania wote waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali mfano michezo, sanaa, uimbaji, ufundi, nk wamesoma mpaka kidato cha nne na kuendelea?

Au hayo mafanikio yao yametokana na hii elimu yetu ya kukaririshana? Mbona nyinyi watu ni wakaidi sana? Au mna ajenda yenu ya siri ya kutaka kuendelea kuwatawala Watanzania kupitia mfumo wenu mbovu wa elimu?
Ili mwamba wenu wa ufipani ndiye anayewaamlisha mkopi na kupest hizo janjajanja za ma beberuu wenuuu?? Pelekeni huko hukoo
 
Mzee mwenyewe huyu hapa wakati anabishana na DC

Back
Top Bottom