Songwe: Katekista wa Kanisa Katoliki auawa kikatili nyumbani kwake

Songwe: Katekista wa Kanisa Katoliki auawa kikatili nyumbani kwake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Katekista wa Kanisa Katoliki, Vincent Mwenda amepoteza maisha kwa kushambuliwa na watu ambao utambulisho wao haujajulikana Mjini Tunduma.

Diwani wa Kata ya Kaloleni, Mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe, Hamis Chuma amesema kiongozi hiyo wa Dini alifariki Mei 10, 2025 baada ya kushambuliwa akiwa nyumbani kwake na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana ni kina nani.

Ibada ya kumuaga marehemu imefanyika katika Porokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Tazara Jimbo la Sumbawanga.
Video: NVP MEDIA

Pia soma ~ Polisi Songwe: Mauaji ya Katekista wa Kanisa Katoliki yametokana na wivu wa mapenzi, alituhumiwa kutembea na mke wa mtu
 
Duh! Upendo unazidi kupungua kati yetu. 😥
 
Poleni wafiwa, je kuna uhusiano wowote na mambo ya mchungaji na mbunge gwajima?
 
Back
Top Bottom