Katekista wa Kanisa Katoliki, Vincent Mwenda amepoteza maisha kwa kushambuliwa na watu ambao utambulisho wao haujajulikana Mjini Tunduma.
Diwani wa Kata ya Kaloleni, Mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe, Hamis Chuma amesema kiongozi hiyo wa Dini alifariki Mei 10, 2025 baada ya kushambuliwa akiwa nyumbani kwake na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana ni kina nani.
Ibada ya kumuaga marehemu imefanyika katika Porokia ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Tazara Jimbo la Sumbawanga.