Songwe: Miaka 200 jela au faini Tsh Milioni 52 kwa makosa 60 ikiwemo kughushi nyaraka

Songwe: Miaka 200 jela au faini Tsh Milioni 52 kwa makosa 60 ikiwemo kughushi nyaraka

Bravo snr

Senior Member
Joined
Aug 16, 2020
Posts
182
Reaction score
477
Leo tarehe 07/05/2021 Mahakama ya wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe imemhukumu ndugu SEMENI GWEWA MSWIMA (Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mlowo) Kifungo cha miaka 200 au kulipa faini ya Tshs.52,000,000/= pamoja na kurejesha kiasi cha Tshs.30,850,000/= alichoiibia Halmashauri wilaya ya Mbozi.

Kesi hiyo ambayo ni Kesi ya uhujumu Uchumi Na.01/2021 ilifunguliwa leo na TAKUKURU Mkoa wa Songwe mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mh.Vitalis Changwe ambapo Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa sitini(60) ambapo ndani yake kuna makosa ya kutumia nyaraka za uwongo kinyume na vifungu vya 342 na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2019 na makosa ya wizi kwa Mtumishi wa Umma kinyume na vifungu vya 258(1) na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Mwaka 2019.Akisomewa Mashtaka hayo,

Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe Bwn Emanuel Ndembeka akisaidiana na Bi.Simona Mapunda,alieleza mahakamani hapo kwamba Mshtakiwa kwa tarehe tofauti tofauti kati ya tarehe 04/07/2019 hadi tarehe 08/05/2020 kwa kutumia hati za malipo na hundi zilizoghushiwa aliweza kutoa na kuiba fedha jumla ya Tshs.30,850,000/= toka katika akaunti Na.61210014674 ambazo ni mali ya Halmshauri ya wilaya ya Mbozi.

Mshtakiwa alikiri makosa yote 60 yaliyokuwa yakimkabili.

Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Changwe alimwamuru Mshtakiwa kulipa faini ya Tshs.800,000/= au kwenda jela miaka mitatu(3) kwa kila kosa la kuwasilisha nyaraka za uwongo,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa arobaini(40).

songwe-3.jpg

Hakimu huyo pia alimwamuru Mshtakiwa alipe faini ya Tshs.1,000,000/= au kwend jela miaka minne(4) kwa kila kosa la wizi kwa Mtumishi wa Umma ,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa ishirini(20).Pamoja na kulipa faini hizo,Mahakama ilimwamuru Mshtakiwa ajereshe katika halmashauri husika fedha alizoiba kiasi cha Tshs.30,850,000/=.Mshtakiwa alishindwa kulipa fedha.
 
Duh!miaka 200!!! umri wa kuishi binaaadamu umeshuka miaka 60, sasa miaka 200 ndio nini tena hicho? aise
Nadhani alishindwa tu kusema kifungo cha maisha, pia jamaa sijui alikuwa anafikiria nini kashitakiwa leo na kukubali makosa kirahisi na hukumu yake nzito 200yrs😭😭😭
 
Ukiangalia miaka hiyo inatisha. Ila ukiwaza kisheria kuwa inakwenda concurrently, haifiki hata kumi so to speak. Watu kama hawa ukitaka kuwakomesha tunga sheria isiyowataka kulipa faini hata shilingi au vifungo viende sambamba na faini. Vinginevyo wataendelea na michezo yao.
 
Mahakama zetu ni za kipuuzi sana ,sasa mtu ana 40+ halafu unampiga miaka 200 , are they serious?
Sheria haiangalii miaka yako mkuu. Hata kama una miaka 100 unaweza kupigwa mvua 80 nyingine kulingana na kosa ulilotenda.

Na kuna wakati unaweza kusikia mtu kafungwa vifungo viwili au vitatu vya maisha. Ndiyo sheria hiyo na siyo upuuzi wa mahakama!
 
Mbona Kigwangala hakamatwi?kina B Mramba walifungwa kifungo cha nje...kwl kuwa dagaa katikati ya samaki shida sana kila kitu ni shida.
 
Jamaa atakaa miaka chini ya minne tu jela, miaka ambayo pia au hata na zaidi angekaa Mahabusu kuruhusu upelelezi kukamilika
 
Ukiangalia miaka hiyo inatisha. Ila ukiwaza kisheria kuwa inakwenda concurrently, haifiki hata kumi so to speak. Watu kama hawa ukitaka kuwakomesha tunga sheria isiyowataka kulipa faini hata shilingi au vifungo viende sambamba na faini. Vinginevyo wataendelea na michezo yao.
Ni miaka saba mkuu
 
Jamaa atakaa miaka chini ya minne tu jela, miaka ambayo pia au hata na zaidi angekaa Mahabusu kuruhusu upelelezi kukamilika
Hapo unataka kutuambia jamaa ametumia mapungufu ya sheria? Ila huyu mtu jasiri sana kwa akili yake kaona 30m aibane ataitumia akitoka baada ya 4yrs
 
Ukiangalia miaka hiyo inatisha. Ila ukiwaza kisheria kuwa inakwenda concurrently, haifiki hata kumi so to speak. Watu kama hawa ukitaka kuwakomesha tunga sheria isiyowataka kulipa faini hata shilingi au vifungo viende sambamba na faini. Vinginevyo wataendelea na michezo yao.
Huyo kifungo chake ni miaka minne na ukitoa 1/4 inabaki mitatu.
 
Back
Top Bottom