Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duh!Huwezi kuchafua oil chafu itakuchafua, tayari chadema maji ya shingo .
Magufuli aliwagaragaza akiwa hai atawagaragaza akiwa mauti.
Takukuru na Mahakama zetu zinaonea gagaa wenye makosa makubwa hawaguswi wanyonge wakigusa pesa ndogo ndogo ndio Takukuru wanatangaza kwa mbwe mbweLeo tarehe 07/05/2021 Mahakama ya wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe imemhukumu ndugu SEMENI GWEWA MSWIMA (Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mlowo) Kifungo cha miaka 200 au kulipa faini ya Tshs.52,000,000/= pamoja na kurejesha kiasi cha Tshs.30,850,000/= alichoiibia Halmashauri wilaya ya Mbozi.
Kesi hiyo ambayo ni Kesi ya uhujumu Uchumi Na.01/2021 ilifunguliwa leo na TAKUKURU Mkoa wa Songwe mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mbozi Mh.Vitalis Changwe ambapo Mshtakiwa alikuwa akikabiliwa na makosa sitini(60) ambapo ndani yake kuna makosa ya kutumia nyaraka za uwongo kinyume na vifungu vya 342 na 337 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya mwaka 2019 na makosa ya wizi kwa Mtumishi wa Umma kinyume na vifungu vya 258(1) na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya Mwaka 2019.Akisomewa Mashtaka hayo,
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Mkoa wa Songwe Bwn Emanuel Ndembeka akisaidiana na Bi.Simona Mapunda,alieleza mahakamani hapo kwamba Mshtakiwa kwa tarehe tofauti tofauti kati ya tarehe 04/07/2019 hadi tarehe 08/05/2020 kwa kutumia hati za malipo na hundi zilizoghushiwa aliweza kutoa na kuiba fedha jumla ya Tshs.30,850,000/= toka katika akaunti Na.61210014674 ambazo ni mali ya Halmshauri ya wilaya ya Mbozi.
Mshtakiwa alikiri makosa yote 60 yaliyokuwa yakimkabili.
Akitoa hukumu hiyo,Hakimu Changwe alimwamuru Mshtakiwa kulipa faini ya Tshs.800,000/= au kwenda jela miaka mitatu(3) kwa kila kosa la kuwasilisha nyaraka za uwongo,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa arobaini(40).
![]()
Hakimu huyo pia alimwamuru Mshtakiwa alipe faini ya Tshs.1,000,000/= au kwend jela miaka minne(4) kwa kila kosa la wizi kwa Mtumishi wa Umma ,ambapo kulikuwa na jumla ya makosa ishirini(20).Pamoja na kulipa faini hizo,Mahakama ilimwamuru Mshtakiwa ajereshe katika halmashauri husika fedha alizoiba kiasi cha Tshs.30,850,000/=.Mshtakiwa alishindwa kulipa fedha.
Kuna habari huku jf kuhusu mwalimu wa kanisa kuhukumiwa miaka 30 kwa kulawiti mtoto ambaye alikuwa anawafundisha. Je hiyo miaka 30 atatumikia miaka mingapi?Hakuna kifungo cha miaka kinachozidi miaka 30 ktk sheria za Tz labda angekuwa ameua au kubaka , unaweza kuta huyo hakai zaidi ya miaka minne jela makosa yote atatumikia kwa pamoja